Mamlaka ya dawa Tanzania yabaini dawa bandia za ARVs
MAELFU
ya watu walioathirika kwa ugonjwa wa Ukimwi ambao kwa sasa wanaotumia
Dawa za Kurefusha Maisha (ARVs) nchini wapo hatarini kufupisha maisha
yao baada ya kubainika kuwa toleo mojawapo la dawa hizo la Machi, 2011
ni bandia.
Uchunguzi wa Mwananchi unaonyesha kuwa dawa hizo
zilizosambaa katika Mikoa ya Dar es Salaam, Tanga na Mara zilianza
kusambazwa tangu Mei mwaka huu na hadi sasa bado zipo sokoni, jambo
lililoilazimu Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA) kuagiza
zirudishwe Bohari Kuu ya Dawa (MSD).
No comments:
Post a Comment