Tuesday, December 29, 2015

JUMLA YA WAANDISHI WA HABARI 110 WAMEUAWA MWAKA HUU

Symbolbild Pressefreiheit
Picha ikionyesha ukatili dhidi ya waandishi wa habari
Jumla ya waandishi wa habari 110, wameuawa duniani kote katika kipindi cha mwaka 2015, hiyo ikiwa ni kwa mujibu wa ripoti ya shirika la maripota wasio na mipaka (RSF) .
Kwa mujibu wa ripoti hiyo ya RSF waandishi wa habari 67 waliuawa wakati wakitekeleza wajibu wao wa kazi katika kipindi cha mwaka huu, na wengine 43 waliuawa katika mazingira ambayo hayajaeleweka. Waandishi wengine wa habari 27 wasio na taaluma kamili ya uandishi wa habari na wafanyakazi wengine 7 kutoka katika vyombo vya habari nao pia waliuawa.
Idadi hiyo kubwa ya vifo vya waandishi wa habari imeelezwa kuchangiwa zaidi na ukatili unaofanywa dhidi ya waandishi hao wa habari wakati wanapokuwa wakitekeleza wajibu wao wa kazi. Hali hii inaashiria kushindwa kwa hatua za kuwalinda waandishi wa habar. 
Chanzo: DW

No comments:

Zilizosomwa zaidi