Sunday, December 27, 2015

BUNJUBURA:MAZUNGUMZO YA AMANI KUANZA MAPEMA WIKI HII

Mazungumzo ya kusuluhisha mzozo wa Burundi yataanza tena kesho mjini Kampala, chini ya usimamizi wa rais Yoweri Museveni wa Uganda.
Museveni aliteuliwa na Jumia ya Afrika Mashariki kuongoza mchakato wa amani ya Burundi, kufuatia machafuko yaliozushwa na uamuzi wa rais Pierre Nkurunziza kupigania muhula wa tatu, kinyume cha maana ya mapatano ya Arusha na katiba ya Burundi inayoruhusu mihula miwili.
Mamia ya raia wa Burundi wanasemekana kuuawa na maelfu kukimbia makwao.
Makundi 14, yakiwakilisha masilahi mbalimbali ya raia wa Burundi yatashiriki katika mkutano huo.

No comments:

Zilizosomwa zaidi