Okwi akitambulishwa rasimi na mwenyekiti wa kamati ya usajiri ya Simba Pope |
Mwenyekiti
wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Pope amesema kwamba
wamemsaini mchezaji huyo mganda Emmanuel Arnold Okwi baada ya kupitia kwa kina suala lake na Yanga
SC na kugundua haki ipo upande wa mchezaji
“Baada ya kulipitia suala lake na Yanga kwa undani kabisa na
vielelezo ambavyo mchezaji mwenyewe ametupatia, tumejiridhisha tuko
sahihi kumsaini ili acheze mpira kunusuru kipaji chake kipindi hiki
ambacho ana matatizo na Yanga SC,”amesema Poppe
Tayari Simba SC imetuma jina la mchezaji huyo katika usajili wake TFF
na ataungana na mganda mwenzake, Joseph Owino, Warundi Pierre Kwizera
na Amisi Tambwe na Mkenya, Paul Kiongera katika wachezaji watano wa
kigeni
“Tumewaandikia barua TFF kuomba kumtumia mchezaji huyu kwa muda
wakati kesi yake na Yanga inaendelea, tumeambatanisha na barua yake
ambayo yeye anatuomba kucheza kwetu kulinda kipaji chake,”amesema Poppe.
Kwa upande wake Okwi ambaye ameahidi makubwa msimu huu mara baada ya
kurejea hii leo alianza kuichezea Simba kwa mara ya kwanza akiwa kinda
wa miaka 17 akitokea Sports club Villa ya Uganda mnamo mwaka 2009 kabla
ya Januari mwaka jana kuuzwa kwa dola za Kimarekani 300,000 Etoile du
Sahel ya Tunisia
Etoile haikulipa fedha hizo Simba SC na baadaye ikaingia kwenye
mgogoro na Okwi, aliyedai hakulipwa pia mishahara yake kwa miezi mitatu
na hivyo Okwi akawafungulia Etoile kesi FIFA na akaomba wakati mgogoro
wao unaendelea, aruhusiwe kuchezea timu yoyote kulinda kipaji chake,
ndipo akajiunga na SC Villa ya kwao
Akiwa SC Villa ndipo aliposaini Yanga Desemba mwaka jana na pamoja na
mapingamizi yaliyoanzia ndani, na baadaye klabu yake, Etoile- lakini
Okwi aliidhinishwa kuichezea timu hiyo ya Jangwani
Okwi aliichezea Yanga SC mechi 11 na kuifungia mabao matano- lakini
kuelekea mechi tano za mwisho za Ligi Kuu msimu uliopita akaingia kwenye
mgogoro na klabu hiyo
Okwi alisusa kushinikiza amaliziwe fedha zake za usajili na mgogoro
wao umeendelea huku mchezaji huyo akiwa amesusa tangu mwezi Machi, ikiwa
ni miezi minne tangu asajiliwe.
Lakini majaliwa ya mshambuliaji huyo mwenye kasi ya kutisha na uwezo
wa kufumania nyavu kuichezea Simba kwa sasa yako mikononi mwa TFF na
FIFA.
Emmanuel Okwi baada ya kukabidhiwa jezi ya wekundu wa Msimbazi |
No comments:
Post a Comment