Friday, August 22, 2014

HATARI:MAMA ADAIWA KUMCHANA MWANAYE VIWEMBE SEHEMU ZA SIRI!


Na Gladness Mallya na Shani Ramadhani 
Inauma sana! RB namba KMR/RB/7911/2014-KUJERUHI iliyopo kwenye Kituo cha Polisi cha Mbezi-Kwayusuph jijini Dar, inamshikilia mama aliyetajwa kwa jina moja la Schola , mkazi wa Kibanda cha Mkaa, Mbezi kwa shitaka la kumchana kwa viwembe mwanaye Mwajuma (6) aliyezibwa usoni kwa sababu ya kukojoa kitandani.GPL. (P.T)

Mtoto Mwajuma aliyechanjwa viwembe sehemu za siri na mama yake.
Akizungumza kwa uchungu, shangazi ambaye ndiye mlezi wa mtoto huyo, mama Msonde alisema baada ya kujifungua mtoto huyo, Schola alikwenda kumkabidhi akawa anamlea hivyo amekuwa akifika hapo nyumbani mara kwa mara ambapo anakaa kwa muda wa siku tano au wiki mbili na kuondoka.
Alisema kuwa Jumatatu asubuhi mwanamke huyo alifika nyumbani na kukuta kitenge chake kimelowa kwa mkojo ambapo alimhoji mwanaye kama anakojoa kitandani au la.Alisema kuwa mwanaye alipomjibu ni kweli alikuwa amekojoa kitandani, alimwambia kwamba akiendelea kesho yake angempa adhabu kali.

Mama aliyetajwa kwa jina moja la Schola anayetuhumiwa kwa ukatili dhidi ya mwanaye.
Alieleza kuwa siku iliyofuata, mama huyo alimkuta mwanaye huyo amekojoa kitandani akampeleka nyuma ya nyumba bila mtu yeyote kumuona na kumtuma akanunue viwembe dukani, alipomletea alimchana navyo sehemu za siri kisha akampaka pilipili na chumvi.
Shangazi huyo aliendelea kusema kuwa wakati mwanamke huyo akiendelea na zoezi hilo, mpangaji mmoja alitoka nje akiwa na shughuli zake na kumkuta mama huyo akimsulubu mwanaye ndipo akaenda kuwaeleza watu waliokuwa ndani.
Alisema walipofika walimkamata na kumpeleka polisi kwenye Kituo cha Mbezi-Kwayusuph, Dar ambapo alifunguliwa jalada hilo huku mtoto huyo akipatiwa matibabu kwenye Zahanati ya Mbezi.

No comments: