Friday, July 4, 2014

NEYMAR KUZIKOSA MECHI ZILIZOBAKI KOMBE LA DUNIA

Neymar baada ya kuumia
Nyota wa timu ya soka ya Brazil Neymar hatoshiriki tena katika michuano ya kombe la dunia baada ya mfupa wake unaoshikana na uti wa mgongo kuvunjika katika mechi ya ushindi wa mabao mawili dhidi ya Colombia.
Neymar aligongwa upande wake wa nyuma dakika tano tu kabla ya mchuano huo wa robo fainali kukamilika.
Alibebwa na kutolewa nje akiwa katika machela lakini ametolewa hospitalini baada ya kufanyiwa matibabu.
Brazil pia itaendelea kushiriki katika mashindano hayo bila nahodha wake Thiago Silva katika mchuano wa nusu fainali dhidi ya Ujerumani baada ya mchezaji huyo kupewa kadi ya pili ya Njano.
Kabla ya habari hizo za Neymar kutolewa raia wa Brazil walifurika katika barabara za taifa hilo kusherehekea ushindi wa timu yao.
Katika robo fainali ya kwanza Ujerumani iliishinda ufaransa kwa bao moja kwa bila .

No comments:

Zilizosomwa zaidi