Nyota
wa nyimbo za Injili Bongo, Bahati Lusako Bukuku ameumia mgongo na
maeneo kadhaa ya mwili (nusu kifo) kiasi cha kushindwa kukaa, kusimama
wala kutembea kufuatia ajali mbaya ya gari iliyotokea kwenye eneo la
Ranchi ya Narco wilayani Kongwa, Dodoma saa tisa usiku wa kuamkia
Jumamosi, Ijumaa Wikienda lina undani wa mkasa mzima.
Kwa mujibu wa chanzo makini, katika ajali hiyo ambayo Bahati alikuwa
akienda Kahama, Shinyanga kwenye mkutano wa Injili, dereva wa gari
alilokuwa akisafiria aina ya Toyota Nadia lenye namba za usajili IT
7945, Edison Mwakabungu ‘Eddy’ (31) aliumia sana kwenye vidole vya miguu
na hawezi kutembea.
Muonekano wa gari hilo kwa ubavuni kulia.
Wengine waliokuwemo kwenye ajali hiyo ni wacheza shoo wa Bahati, Frank
Muha (20) na mwenzake ambaye jina lake halikupatikana mara moja.
Habari zilidai kuwa gari hilo halikuwa na
matatizo hivyo kumfanya dereva wake kukanyaga mafuta kwa wastani wa
kilometa 120 kwa saa.“Sasa walipofika eneo la Kibaigwa, walikutana na
lori likitokea Dodoma kwenda Morogoro, wakavaana kwa mbele. Nadia
likatoka barabarani hadi porini likiwa limeharibika kuanzia kwenye shoo
ya mbele, injini na siti za mbele halafu lori hilo likakimbia.
“Nadia ilipotulia, Bahati alijikuta hawezi kufanya chochote, dereva wake
naye ameumia kwenye vidole vya miguu. Wale wawili waliokuwa siti ya
nyuma, wote walijeruhiwa lakini mmoja si sana. Ilibidi yeye abaki pale
na gari ili majeruhi wengine wakimbizwe Hospitali ya Wilaya ya Kongwa,
Dodoma kwa matibabu,” kilisema chanzo hicho.
Gari alilopata nalo ajali mwimbaji wa nyimbo za Injili, Bahati Bukuku aina ya Toyota Nadia lenye namba za usajili IT 7945.
No comments:
Post a Comment