Monday, June 30, 2014

TAZAMA PICHA JINSI WANAFUNZI WA UDOM WALIPOKUWA WANAGOMBANIA USAFIRI WA KURUDI KWAO BAADA YA CHUO KUFUNGWA

 Askari polisi anayelinda usalama wa abiria na mali zao katika kituo cha mabasi yaendayo mikoani akijalibu kutoa maelekezo kwa wanafunzi wa UDOM waliofika kutafuta usafiri kituoni hapo na kukuta hali ya usafiri hailidhishi kutokana na uchache wa Mabasi.

 Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) wakigombania kulipa nauli kwa ajenti wa Basi la Urafika linalofanya safari zake kuelekea Iringa  baada ya baadhi ya Vyuo kufungwa kwa pamoja na hivyo kufanya idadi ya abiria wa mikoani kuwa wengi kuliko mabasi yaliyopo.
Baadhi ya Abiria wakitafakari na mabegi yao baada ya kufika kituo cha mabasi ya kwenda mikoani na kujikuta wakikosa usafiri kutokana na uchache wa mabasi ulisababishwa na vyuo vilivyopo mkoani Dodoma kufungwa kwa wakati mmoja.

No comments:

Zilizosomwa zaidi