Kocha mpya wa Yanga sc, Mbrazil Marcio Maximo ameanza kazi leo kwa kufanya mazungumzo na baadhi ya wachezaji wa klabu hiyo .
Mkutano huo umefanyika makao makuu ya klabu ya Yanga, makutano ya Twiga na Jangwani, Kariakoo, jijini Dar es salaam.
Maximo
alipata nafasi ya kuwaeleza mipango yake ya kazi na kuwataka wachezaji
waelewe umuhimu wao katika kujenga mafanikio ya Yanga.
Kocha
huyo aliyewahi kufanya kazi nchini kwa kuifundisha timu ya Taifa ya
Tanzania, Taifa stars, baada ya kukutana na wachezaji leo hii, sasa yuko
tayari kuanza mazoezi ya kujiwinda na msimu mpya wa ligi kuu soka
Tanzania bara unaotarajia kuanza mwezi agosti mwaka huu.
No comments:
Post a Comment