
Kitendo hicho kilielezwa kuwa ni kuwazuia
waandishi wa habari kutuma taarifa za ajali hiyo kwenye vyombo vyao vya
habari. Mzozo mkali uliibuka kwa waandishi wa habari wa Shirika la
Utangazaji Tanzania (TBC), kituo cha Televisheni cha ITV na Redio One na
mwandishi wa Redio Standard waliokuwa kwenye msafara huo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, (SACP), Geofrey
Kamwela alipotafutwa ili aelezee tukio, alisema hana taarifa kamili na
kutaka apewe muda ili afutilie suala hilo aeleze ajali hiyo. Hata hivyo
baadaye alipotafutwa jioni alipotafutwa alisema kuwa atatolea taarifa
suala hilo leo.
Ajali hiyo iliyohusisha magari matatu ilitokea
katika Kijiji cha Kirumbi, Wilaya ya Sikonge, mpakani mwa mikoa ya
Tabora na Singida ikiwa ni siku ya kwanza ya mbio za Mwenge huo
ulioingia mkoani Singida ukitokea Mkoa wa Mbeya.
Mashuhuda wa ajali hiyo, walisema kuwa ilitokea
muda mfupi baada ya Mwenge kupokewa katika Kijiji cha Rungwa kilichopo
Kata na Tarafa ya Itigi. Ilielezwa kuwa gari moja la polisi lililokuwa
kwenye msafara lilipasuka gurudumu na kusimama pembeni mwa barabara.
Gari jingine la polisi lililokuwa kwenye msafara
lilisimama ghafla kutaka kufahamu kilichowapata wenzao, ndipo gari la
Ofisi ya Afya ya Mkoa likiwa na wahudumu wa afya, lililigonga kwa nyuma
gari hilo.
Kwa kuwa kila gari lilikuwa kwenye mwendo wa kasi
ili kuendana na gari la Mwenge lililokuwa limetangulia, gari jingine
lililokuwa na askari waliokuwa wamening’inia juu nalo lililigonga gari
hilo la afya kwa nyuma na kusababisha askari hao kuumia.
Katika tukio hilo, hakuna hata mmoja kati ya
wahudumu wa afya aliyeumia, lakini ajali hiyo ilisababisha askari mmoja
kuvunjika mguu, mwingine kuvunjika mkono huku wawili hali zao zikiwa
nzuri na mwingine alikuwa mahututi.
Baada ya tukio hilo, waliwahishwa kwenye Hospitali ya Misheni ya St. Gasper iliyopo Itigi kwa matibabu zaidi.
No comments:
Post a Comment