Shirika la Afya Duniani WHO limetoa wito wa kuongezwa
ushuru tumbaku ili kupunguza uvutaji sigara ambao umebainika
kusababisha vifo ya vya watu milioni sita kila mwaka.
Katika taarifa iliyotolewa 'Siku ya Kutokuvuta Tumbaku Duniani', WHO imesema hatua
za kisera zinahitajika ili kupunguza matumizi ya tumbaku na hivyo kuokoa
uhai wa waathirika wa bidhaa hiyo.
WHO inasema kuwa uvutaji tumbaku unaweza kuua zaidi ya watu
milioni nane kila mwaka ifikapo mwaka 2030 na hivyo sasa inapendekeza
uongezwe ushuru wa bidhaa hiyo . Tayari katika baadhi ya nchi za barani
Afrika hatua za kisera zimechukuliwa ili kupunguza ushawishi wa matumizi
ya tumbaku kwa binadamu. Takwimu zinaonyesha kuwa ongezeko la kodi kwa
asilimia 50 litapunguza wavuta sigara na tumbaku milioni 49 duniani
ndani ya miaka mitatu na hivyo kuokoa uhai wa watu milioni 11. WHO
imesema kuwa kati ya watu milioni sita ambao hufa kutokana na uvutaji
sigara asilimia 80 ni kutoka nchi masikini duniani. Aidha WHO imesema
watu laki sita hupoteza maisha kutokana na kuvuta moshi wa wanovuta
sigara jambo ambalo linaashiria ulazima wa uvutaji sigara kupigwa
marufuku katika maeneo ya umma.
No comments:
Post a Comment