Tuesday, February 18, 2014

MAHABUSU AJINYONGA NA KUFARIKI DUNIA WILAYANI MOMBA.




Mnamo tarehe 17.02.2014 majira ya saa 06:00hrs asubuhi mahabusu aliyefahamika kwa jina la Vumi Elias (30) mkazi wa mtaa wa Maporomoko Tunduma wilaya ya Momba alifariki dunia muda mfupi baada ya kufikishwa kituo cha afya tunduma baada ya kujaribu kujinyonga akiwa ndani ya mahabusu katika kituo cha polisi Tunduma. Marehemu aliingia katika choo cha mahabusu kilichopo ndani ya mahabusu hiyo majira ya saa 04:30hrs usiku na kutaka kujinyonga kwa kutumia tambala la kupigia deki. Marehemu aliokolewa na askari waliokuwa zamu chumba za mashitaka na kukimbizwa kituo cha afya kwa matibabu akiwa katika hali mbaya na hawezi kuongea baada ya kupata taarifa kutoka kwa mahabusu wengine walioingia chooni humo. awali mnamo tarehe 14.02.2014 marehemu alikamatwa kwa kosa la unyang’anyi wa kutumia nguvu. chanzo kinachunguzwa, mwili wa marehemu umehifadhiwa katika kituo hicho cha afya.




No comments:

Zilizosomwa zaidi