Sunday, December 1, 2013

KATIBU WA CHADEMA WILAYA YA CHUNYA AJIUNGA NA CCM

    1
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahmani Kinana akifafanua jambo wakati alipokuwa akiuliza swali alipokagua ujenzi wa barabara ya Mbeya Chunya yenye kilomita 36 inayogharimu kiasi cha shilingi bilioni 56 za kitanzania , Barabara hiyo inajengwa na kampuni ya kichina ya China Communication Construction Company, Kinana yuko katika ziara ya kikzani ya mikoa mitatu Ruvuma, Mbeya na Njombe akiongozana na Katibu wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi Ndugu Nape Nnauye na Dr. Asha Rose Migiro Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kiamataifa leo amemaliza ziara katika jimbo la Lupa na kesho anaendelea na ziara katika jombo la Songwe wilayani China, kulia ni Mh. Abbas Kandoro Mkuu wa mkoa wa Mbeya na katikati ni Dr. Asha Rose Migiro.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-LUPA-CHUNYA)
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahmani Kinana akipiga makofi wakati Braison Mwasimba aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha CHADEMA wilaya ya Chunya aliporejesha kadi yake ya chama hicho na kujiunga na chama cha Mapinduzi CCM katika mkutano wa hadhara uliofanyika kata ya Lupa.3
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahmani Kinana akipiga makofi wakati Braison Mwasimba aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha CHADEMA wilaya ya Chunya alikionyesha kadi yake ya chama cha Mapinduzi CCM baada ya kukabidhiwa katika mkutano wa hadhara uliofanyika kata ya Lupa. 5
Mbunge wa jimbo la Songwe na Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Mh Philip Mulugo akimvisha shati la CCM Bw. Braison Mwasimba aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha CHADEMA wilaya ya Chunya aliporejesha kadi yake ya chama hicho na kujiunga na chama cha Mapinduzi CCM katika mkutano wa hadhara kata ya Lupa.(P.T)
6
Nape Nnauye Katibu wa NEC Siasa , Itikadi na Uenezi akimuangalia Bw. Braison Mwasimba aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha CHADEMA wilaya ya Chunya wakati akihutubia aliporejesha kadi yake ya chama hicho na kujiunga na chama cha Mapinduzi CCM katika mkutano wa hadhara kata ya Lupa. 7
Mkuu wa mkoa wa Mbeya Mh. Abbas Kandoro akikabidhi mashine ya kufyatulia matofali kwa kikundi cha Power Group. 8
Mkuu wa mkoa wa Mbeya Mh. Abbas Kandoro akikabidhi mashine ya kufyatulia matofali kwa kikundi cha Nguvu kazi. 9
Mkuu wa wilaya ya Chunya Deodatusi Kinawiro akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika kata ya Lupa Tingatinga leo. 10
Kutoka kulia ni Naibu waziri wa Elimu na Mbunge wa jimbo la Songwe Philip Mulugo, Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana, Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mbeya na Mbunge wa jimbo la Mbozi Mashariki na Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi wakielekea katika eneo la Mkutano uliofanyika Kata ya Lupa Chunya. 11
Baadhi ya wachimaji wadogo wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM wakati akizungumza nao. 12Mkurugenzi wa Kituo cha mafunzo kwa vitendo ya uchimbaji na uchenjuaji wa dhahabu Matundasi RSM Development Company Limited Chunya Paul Gongo kulia akizungumza na Dr. Asha Rose Migiro Katibu wa Siasa na Uhusiano wa Kiamataifa wakati kinana na ujumbe wake walipkagua shughuli za kituo hicho. 13Wachimaji wadogo wakimsikiliza Kinana 14Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Mkurugenzi wa Kituo cha mafunzo kwa vitendo ya uchimbaji na uchenjuaji wa dhahabu Matundasi RSM Development Company Limited Chunya Paul Gongo wakati alipokagua shughuli za kituo hicho wilayani chunya leo. 15Wananchi wa mjini Chunya wakimshangilia Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana hayupo pichani wakati alipozungumza nao mara baada ya kuwasili wilayani humo leo. 16Msafara wa Kinana ukielekea Chunya 17Mkuu wa wilaya ya Chunya Deodatusi Kinawiro akizungumza na wananchi katika kijiji cha Chalangwa wakati wa mapokezi ya katibu mkuu wa CCM.

No comments:

Zilizosomwa zaidi