Rais wa Bayern Munich, Uli Hoeness na Mwenyekiti wa klabu hiyo, Karl-Heinz Rummenigge, wamemshambulia kocha wa Chelsea, Jose Mourinho, kutokana na kitendo chake cha kuitetea rafu ya kiungo wake, Ramires, dhidi ya Mario Gotze.
Mourinho alimlaumu mwamuzi wa pambano hilo, Jonas Eriksson, akdiai kwamba hakustahili kumpatia Ramires kadi ya pili ya njano kwa rafu hiyo, lakini Bayern wanaamini kwamba mwamuzi alikuwa sahihi.
“Nadhani kauli ya Mourinho ni aibu. Baada ya rafu mbaya kama ile, Mario inabidi ajichukulie mwenye bahati. Angeweza kuumia vibaya zaidi,” alisema Rummenigge.
Naye Hoeness alisikika akisema: “Ile ni kadi nyekundu iliyowahi kuwa wazi zaidi katika soka. Kama kocha kama Mourinho anaongelea kuwa ni maamuzi mabovu, nina wasiwasi labda alihudhuria mechi nyingine.”
No comments:
Post a Comment