Mchungaji Kadani Limbu ambaye ni Katibu
wa Kanisa la EAGT Makao Makuu (Ujenzi) akisoma wasifu wa marehemu
Askofu Kulola aliyezaliwa 1928 katika Kijiji cha Nyang’honge Wilayani
Kwimba Mkoani Mwanza na kujaliwa kupata elimu ya msingi (Middle School)
na sekondari ya Bwiru Boys Mwanza kati ya mwaka 1946 hadi 1949 kuendelea
na masomo na kupata Civil Technician.
Baada ya kumaliza na kupata utaalamu
huo na kuajiliwa kuwa mtumishi wa serikali katika Halmashauri ya Mji wa
Mwanza kama Mhandisi wa Mchoraji wa Ramani za majengo na Barabara wakati
wa uhai wake aliamua kuacha kazi na kuanza utumishi wa mungu akifanya
kazi kwa kutembea kila mahali akihubiri Injili kwa watu mbalimbali.
Wasifu huo ulimwelezea Askofu Kulola
wakati wa utumishi wake wa kiroho alikuwa akitembea kwa miguu kuanzia
mwaka 1962 baada ya kuacha kazi za serikali mwaka 1951 alipatwa na
matatizo na kuwahi kufungwa gerezani na kupigwa na bwana jela na
kuumizwa vibaya muguu wake wa kushoto na kupelekea kupata kilema na
kuwekewa mguu wa bandia.
Marehemu Askofu Kulola ameacha mke na
watoto 10 wajukuu 42 vitukuu 16 na amekuwa mutumishi wa kiroho kwa
kuanzia akiwa na umri wa miaka 18 na jana amezihilisha kutokana na umati
mkubwa uliofika kumuaga kwenye uwanja wa michezo wa kirumba Jijini
Mwanza.
No comments:
Post a Comment