Thursday, August 29, 2013

HII NI TAARIFA YA ASKOFU MOSES KULOLA KUFARIKI

Askofu Mkuu wa Evangelistic Assemblies God Tanzania (EAGT), Moses Kulola amefariki dunia.

Kwa mujibu wa taarifa za kuaminika ambazo tumezipata kutoka kwa watu wa ndani wa familia hiyo, zinaeleza kuwa Askofu Kulola amefariki katika hospitali ya AMI (African Medical Investments) iliyopo Slipway jijini Dar es Salaam.

Askofu Kulola, ambaye amezaliwa mwaka 1928, amekuwa akisumbuliwa na maradhi kwa muda mrefu na hata kufikia hatua ya kupelekwa nchini India kwa matibabu.


No comments:

Zilizosomwa zaidi