Wednesday, August 28, 2013

AJARI IMETOKEA MKOANI SHINYANGA, 13 WAFARIKI NA 11 WAJERUHIKA...

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiG5W_clJDTAmXZq75fxPx1FsEJn9IRzZtXKnOY3D4FbNkdiRZRC6aCnR-EaysTkJpFqHT3y0cpKtWuAA3EW5hPWOPfOOMCKtgOaCMy3EY_D6WTBwXlmbG-Fgl_jQXYOfYdZe3PEUiEJNS_/s1600/2013-06-02+14.35.15.jpg Watu 13 wamefariki na wengine 11 kujeruhiwa vibaya katika ajari iliyotokea mkoani Shinyanga usiku wa kuamkia leo.
Ajari hiyo imehusisha magari mawili ambapo gari aina ya Hiace yenye nambari  za usajiri
T756 CHX, Ilienda kuliparamia lori lililokuwa limeharibika lenye nambari za usajiri T696 AMS

Gari hilo aina ya Hiace lilikuwa limebeba wasafiri likitokea wilayani Kahama kuelekea wilaya ya Ushirombo ambapo kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanga Bw. Kihema Kihema  amethibitisha kutokea kwa ajari hiyo na kusema kuwa miongoni mwa watu waliopoteza maisha ni Dereva wa Hiace ambaye alifariki palepale baada ya ajari kutokea na majeruhi wamepelekwa katika Hospitali ya Wilaya ya Kahama kwa ajiri ya Huduma ya kwanza na matibabu.

No comments:

Zilizosomwa zaidi