Viwango hivi Vipya vya nauli ya Mabasi ya mikoani vitaanza kutumika kuanzia tarehe 12 Aprili, 2013.
Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA) imekamilisha mchakato na kuridhia viwango vipya vya nauli kwa ajili ya usafiri wa mijini na usafiri wa kwenda mikoani.
Viwango hivi vipya
vimefikiwa baada ya kufuata taratibu za kisheria na za kiutendaji ambazo
SUMATRA kama msimamizi na mdhibiti wa sekta ya usafiri wa barabara inapaswa
kuzifuata kabla ya kuridhia viwango hivyo.
Viwango vipya vya
nauli vitaanza kutumika kuanzia tarehe 12 Aprili, 2013.
SUMATRA ina wajibu kisheria kuhakikisha pamoja na mambo
mengine kuwa maslahi ya watumiaji na watoa huduma za usafiri yanalindwa ili
kuwepo na huduma endelevu ya usafiri ulio bora, salama na wenye kukidhi
mahitaji. Aidha SUMATRA ina jukumu la kujenga na kulinda mazingira mazuri na ya
kuvutia kwa watoa huduma ili huduma ya usafiri inayotolewa inakuwa katika
kiwango na gharama zinazoendana na huduma zenyewe.
Katika kipindi cha mwaka wa fedha wa 2011/2012, SUMATRA
ilipokea maombi rasmi kutoka kwa wamiliki wa vyombo vya usafiri wa barabara
yakiwemo makampuni ya usafirishaji abiria ya Cordial Transport Services P.L.C,
Happy Nation Co. Ltd, ABC Trans na Mwesigwa Mtazaha Kazaula yakipendekeza
mapitio ya viwango vya nauli za mabasi yanayotoa huduma za usafiri mijini
(Daladala) na mabasi yanayotoa huduma katika Mikoa kufuatia ongezeko la gharama
za uendeshaji kwa mujibu wa mawasilisho yao.
Wakati maombi ya wamiliki wa Daladala yalilenga katika
kuongeza viwango vya nauli kwa 149% ya viwango vya sasa, wamiliki wa mabasi ya
masafa marefu waliomba nyongeza kati ya 35% na 48.5%.
Kwa mujibu wa Kifungu Na 18 cha Sheria ya SUMATRA, 2001,
SUMATRA iliwashirikisha wadau mbalimbali katika kujadili na kupata maoni yao
kuhusu maombi ya wamiliki ya kuongeza viwango vya nauli kabla ya kufanya
maamuzi ya mwisho.
Aidha Mamlaka iliridhia viwango vipya kwa mujibu wa kifungu
cha 16 Cha Sheria ya SUMATRA ambacho kinaipa Mamlaka kufanya mapitio ya nauli
mara kwa mara kwa kuzingatia gharama za kutoa huduma, maslahi ya watoa huduma,
faida, maslahi ya watumia huduma ya kulipa nauli yenye uwiano na gharama za
huduma inayotolewa.
Kwa kuzingatia hoja za waombaji, maoni ya wadau, uchambuzi
wa menejimenti, haja ya kupunguza gharama zisizo za lazima za uendeshaji na
udhibiti wa vitendo vya uvunjaji wa Sheria na taratibu za uendeshaji shughuli
za usafirishaji, Mamlaka ya SUMATRA iliamua kuongeza viwango vya juu vya nauli
za Daladala kwa wastani wa 24.46%.
Aidha kwa mabasi ya masafa marefu, viwango vimeongezwa kwa
20.3% kwa mabasi ya kawaida, 16.9% kwa mabasi ya daraja la kati na 13.2% kwa
mabasi ya daraja la juu.
Mchanganuo wa viwango vipya vya nauli ni kama ifuatavyo:
1.
Nauli
za Daladala – Jiji la Dar es Salaam
Umbali
wa Njia
|
Kiwango
Kipya cha Nauli
|
Mfano
wa Njia
|
Kilomita
kati ya 0 – 10 (Na mipaka ya Jiji Kati)
|
Sh
400/=
|
Ubungo
– Kivukoni
|
Kilomita
kati ya 11 – 15
|
Sh
450/=
|
Mwenge
– Temeke
|
Kilomita
kati ya 16 – 20
|
Sh
500/=
|
Tabata
Chang’ombe – Kivukoni
|
Kilomita
kati ya 21 – 25
|
Sh
600/=
|
Pugu
Kajiungeni – Kariakoo
|
Kilomita
kati ya 26 – 30
|
Sh
750/=
|
Kibamba
– Kariakoo
|
Mamlaka imeandaa majedwali kwa njia zote za Dar es Salaam.
Majedwali hayo yanaweza kupatika katika tovuti yetu www.sumatra.or.tz.
Nauli ya Mwanafunzi itakuwa Sh 200/= ambayo ni nusu ya nauli
ya mtu mzima ya kiwango cha chini cha nauli ya Sh 400/=. Nauli hii itatumika
kwa njia zote za Jiji la Dar es Salaam.
2.
Nauli
za Mabasi ya Masafa Marefu
Daraja
la Basi
|
Nauli
ya zamani kwa km-abiria
|
Nauli
mpya kwa km-abiria
|
Mfano
wa kiwango kipya cha nauli kwa baadhi ya njia
|
|
Basi
la Kawaida kwa njia ya lami
|
Sh
30.67
|
Sh
36.89
|
DSM–Mbeya
Km 833
|
Sh
30,700
|
Basi
la Kawaida kwa njia ya vumbi
|
Sh
37.72
|
Sh
46.11
|
S/wanga-KigomaKm
551
|
Sh
25,400
|
Basi
la hadhi ya kati (Semi Luxury
|
Sh
45.53
|
Sh
53.22
|
DSM–Mwanza
Km 1,154
|
Sh
61,400
|
Basi
la hadhi ya juu (Luxury)
|
Sh
51.64
|
Sh
58.47
|
DSM–Arusha
Km 616
|
Sh
36,000
|
Ili kuhakikisha kuwa kuna uwiano kati ya viwango vipya vya
nauli na ubora wa huduma ya usafiri, Mamlaka imetoa maagizo kwa wamiliki wa
mabasi ya masafa marefu kuboresha maeneo yanayohusiana na huduma ya usafiri
kama ifuatavyo:
1.
Wamiliki
wa mabasi kutokutumia wapiga debe katika kuuza tiketi za safari
2.
Wamiliki
wa mabasi kuhakikisha wanafuata Kanuni za SUMATRA za Udhibiti wa Tozo na Nauli
(SUMATRA Tarrif Regulations) ambazo zinahimiiza kuwepo kwa kumbukumbu sahihi za
mahesabu ili kurahisisha mapitio ya viwango vya nauli
3.
Kufuata
Sheria, Kanuni na Masharti ya Leseni ya usafirishaji abiria
4.
Kutoza
nauli kwa mujibu wa daraja la basi lenye sifa kamili la daraja husika kama
ilivyoainishwa katika Kanuni za Usalama na Ubora
Aidha kwa mabasi ya mjini, Mamlaka imetoa maelekezo
yafuatayo:
5.
Kuhakiksha
kuwa abiria wote wanapatiwa tiketi
6.
Kudhibiti
vitendo vya ukiukwaji wa Sheria ikiwemo kutokamilisha safari maarufa kama
kukata ruti, kubadili njia na unyanyasaji wa aina yoteyote kwa abiria
7.
Kutokutumia
wapiga debe
8.
Wafanyakazi
wa mabasi kuvaa sare nadhifu wakati wote.
Mamlaka ya SUMATRA inaendelea kuimarisha ushirikiano kwa
kufanya kazi kwa karibu na Mamlaka zingine kama Wakuu wa Mikoa, Serikali za
Mitaa, Mamlaka za Miji, Polisi, TBS, TANROADS, Kamisheni ya Bima na wananchi
kwa ujumla, katika kuleta mageuzi kamili ya utoaji wa huduma za usafiri wa
barabara kwa kiwango cha juu.
A.S.K. Kilima
KAIMU MKURUGENZI MKUU
2 Aprili, 2013
No comments:
Post a Comment