Thursday, March 28, 2013

UNAFAHAMU KISA CHA MENEJA WA KAMPUNI YA NDEGE YA FASTJET KUTIWA MBARONI?..KISOME HAPA KISA HICHO.



Meneja wa wafanyakazi wa Ndani ya Ndege wa Kampuni ya ndege ya  Fastjet Emma Donovan, amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala Dar es Salaam kujibu shtaka linalomkabili la kutoa lugha ya matusi.
 
Emma (40) alipandishwa kizimbani jana na kusomewa shtaka hilo na Wakili wa Serikali Nassoro Katuga, mbele ya Hakimu Joyce Minde.
 
Katuga alidai kuwa Machi 19 mwaka huu Emma alimtolea lugha ya matusi Samson Itinde jambo ambalo ni kinyume cha sheria. 
Emma alikana shtaka hilo ambapo Katuga alidai upelelezi umekamilika na kuomba kupangiwa tarehe kwa usikilizwaji wa awali.
 
Hakimu Joyce alisema kuwa dhamana ya mshtakiwa iko wazi lakini kwa kuzingatia vigezo vya dhamana vitakavyotolewa kwa kuwa mshtakiwa ni raia wa kigeni.

Alitaja masharti ya dhamana kuwa mshtakiwa anatakiwa kuwasilisha hati yake ya
kusafiria au kutoa fedha taslim sh milioni tano na pia awe na wadhamini
wawili ambao ni Watanzania.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Aprili 9 ili kupangwa tarehe ya kuanza kwa usikilizwaji wa awali.

No comments: