Una hakika mwanao anapokuaga
nyumbani kweli anakwenda shule? Ni swali ambalo wazazi na walezi
wanapaswa kufuatilia ili kupata uhakika.
Imebainika kuwa wazazi na walezi wengi
wanadanganywa, wapo watoto ambao wanawahi kuamka nyumbani wakisema
wanakwenda shule, kumbe wanakwenda kufanya ngono au mambo mengine yasiyo
ya maana, kabla ya kwenda shule.
Aidha kwa wale ambao wanaishi bwenini, baadhi yao
matendo wanayofanya yanatia ‘kichefuchefu’ hata kusikia. Swali la msingi
kwa wazazi kulipatia jibu ni je, mwanao yuko salama?
Haijalishi kama shule ya msingi au sekondari au
hata chuo, ni suala la msingi kwa mzazi kufuatilia na kupata jibu, hasa
kutokana na baadhi ya tafiti kubainisha kuwa baadhi yao wamekuwa
wakifanya mambo ya yenye kutia aibu wanapokuwa mbali na walezi au wazazi
wao.
Baadhi ya watoto ni waongo kupindukia kwa wazazi
wao, huku wengine wakijifanya kuwasikiliza wazazi na walezi, tofauti na
ukweli wa matendo yao wanayoyafanya baada ya kuachana nao.
Mfano halisi wa matendo ya wanafunzi
Kumekuwa na ongezeko kubwa la utoro kwa wanafunzi
Shule ya Sekondari ya Kata Majani ya Chai iliyopo eneo la Kipawa, Jijini
Dar es Salaam.
Wanafunzi mbalimbali wakiwemo wa kidato cha nne na
baadhi ya wale wanaosomea sanaa wanadaiwa kuongoza kwa matendo ya
kuvuta bangi na kufanya ngono wakitumia baadhi ya nyumba zilizopo jirani
na eneo hilo la shule.
Akiongea katika hali ya kuonyesha kukata tamaa na kukerwa, Mkuu wa Shule hiyo, Jansinta Assey anasema “Hili tatizo limekithiri sana kwa wanafunzi wa kike na wa kiume, tulijaribu kuwabana kuwauliza wanaenda kufanya nini walitujibu wanaenda kuvuta bangi na baadhi ya wasichana walidai wanawafuata wavulana kwa ajili ya kufanya nao ngono”.
Akiongea katika hali ya kuonyesha kukata tamaa na kukerwa, Mkuu wa Shule hiyo, Jansinta Assey anasema “Hili tatizo limekithiri sana kwa wanafunzi wa kike na wa kiume, tulijaribu kuwabana kuwauliza wanaenda kufanya nini walitujibu wanaenda kuvuta bangi na baadhi ya wasichana walidai wanawafuata wavulana kwa ajili ya kufanya nao ngono”.
Muhimu kwa wazazi
Hapo ndipo linapokuja swali kwa wazazi wenye
watoto…je unayajua anayofanya mwanao baada ya kuachana nae? Je, unafanya
nini kuhakikisha kizazi chako kinakuwa salama katika hali kama hii
ambayo watoto wengine wanaibika kwenda kuvuta bangi na kufanya ngono
badala ya kwenda kusoma kama wanavyoaga wanavyotoka nyumbani?
Hali katika shule
Mwalimu Jansinta anasema vitendo vya uvutaji bangi
na biashara ya ukahaba kwa wanafunzi wake vinachangiwa na ushirikiano
haba anaoupata kutoka kwa baadhi ya vyombo vya ulinzi na usalama katika
eneo hilo.
CHANZO: MWANANCHI
CHANZO: MWANANCHI
No comments:
Post a Comment