Papa Benedict wa 16 ametuma ujumbe wake wa kwanza kwenye
akaunti yake yaTwitter. Ujumbe huu ulikuwa umesubiriwa kwa hamu sana.
Alionekana akibonyeza kwenye tabiti yake ya iPad na kutuma ujumbe huo
UJumbe wake ulikuwa unasoma hivi ''Marafiki wapendwa, nimefurahi sana
kuwasiliana nanyi kupitia Twitter. Asanteni sana kwa ujumbe wenu na ninawabariki
nyote.''
Msemaji wake alisema kuwa ujumbe wa Papa utafikia kila mtu amjuaye kwa
kutumia akaunti zake zilizo kwenye lugha saba.Akaunti ya papa iliyo kwenye lugha ya kiingereza tayari ina wafuasi zaidi ya laki sita.
Akaunti zake zote ambazo ni @pontifex zinafuatana moja baada ya nyingine.
Mwaka jana Papa alituma ujumbe wake wa kwanza kutoka Vatican kuweza kuzindua mtandao wake wa maelezo mbali mbali.
Papa ni kiongozi wa waumuni bilioni 1.2 wa kikatoliki na atakuwa akitia saini ujumbe wake wala hatoundika mwenyewe.
No comments:
Post a Comment