

Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa mchezo huo, Milovan alisema kuwa Kagera kipindi cha pili ilionyesha kandanda safi na la kuvutia hadi kuwafunika wachezaji wake, ambao walionekana kuzidiwa kasi.
“Kagera wamecheza soka safi na hasa katika kipindi cha pili na kuwazidi wachezaji wangu, ambao kutokana na makosa kadhaa waliyoyafanya, walitoka sare ya mabao 2-2,” alisema Milovan huku akimpa mkono wa hongera, kocha mkuu wa Kagera Sugar, Abdallah ‘King’ Kibadeni.
No comments:
Post a Comment