Monday, September 10, 2012

Chama cha wananchi CUF kimeanzisha mikutano ya hadhara ya mfulurizo. Katika mkutano uliofanywa na cha hicho jana katika viwanja vya jangwani jijini Dar, Dk Ibrahim Lipumba ameishauri serikali kuweka sera itakayowasaidia wakulima wadogowadogo ili kuimarisha uchumi wa nchi na sio vinginevyo. Aliongeza kuwa nchi nyingi duniani kama vile Denmark zimeweza kujiimalisha kiuchumi kwa kuanza kuimarisha uzalishaji wa wakulima wadogowadogo. Kama serikali na wanaharakati wote watashindwa kufanyia kazi mawazo haya, bado nchi itaendelea kuwa na hali ngumu kiuchumi.

No comments:

Zilizosomwa zaidi