Monday, September 10, 2012

Baada ya vuta nikuvute kati ya jeshi la polisi na waandishi wahabari jijini Dar, sasa waandishi wa habari waruhusiwa kufanya maandamano hapo kesho. Kamanda wa polisi Suleiman Kova amethibitisha kuwepo kwa maandamano. Maandamano hayo ni ya kupinga mauaji ya mwandishi Daud Mwangosi yaliyotokea wiki iliyopita huko iringa. Kilele cha maandamano hayo itakuwa katika viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar.

No comments:

Zilizosomwa zaidi