Thursday, May 23, 2013

HUYU NDIO SHEH WA TOMONDO- ZANZIBAR ALIYEMWAGIWA TINDIKALI JANA USIKU

Sheha Mohammed Omary Said aliyemwagiwa tindikali na mtu asiyejulikana akiwa katika hospitali ya Mnazi Mmoja Unguja akipatiwa matibabu, Sheikh Mohammed amepata maumivu makali sehemu za kifuwa na jicho kuumia

Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Mjini Magharibi,Mukhadam Khamis,amesema chombo kilichotumika kumwagia tindikali Sheha huyo kilipatikana eneo la tukio na kwamba polisi imekichukua kwa kukichunguza kitaalam ili kugundua aliyekuwa akikitumia kwa kuangalia alama za vidole.

Sheha huyo alimwagiwa tindikali jana usiku wakati alipotoka nje ya nyumba yake kuchota maji na ndipo mhalifu huyo alipomwagia tindikali na kwamba hakuweza kumtambua.

Sheha Mohammed Kidevu akiwa katika wodi ya Hospitali kuu ya Rufaa Mnazi Mmoja akipata matibabu ya majaraha ya kitu kinachosadikiwa kwa Tindi Kali,akipata matibabu hayo katika hospitali hiyo.

MAJAMBAZI YAVAMIA GARI ASUBUHI YA LEO NA KUPORA MAMILIONI JIJINI DAR

(Pichani ndio matundu ya risasi tatu zilivyorindima kwenye kioo cha dereva na   kumjeruhi dereva sehemu ya bega na kufanikiwa kunyakua begi linalosadikiwa kuwa,lilikuwa na kiasi cha fedha shilingi milioni 40 na kutokomea nazo.)
(Pichani kulia ni Askari Usalama barabarani akichukuliwa maelezo yake kutokana kushuhudia tukio la ujambazi lililofanyika maeneo ya Sayansi mataa-Kijitonyama jijini Dar mapema leo mnamo majira ya saa tano kasoro)
 
Ambapo kwa mujibu wa mashuhuda waliokuwepo eneo la tukio wanaeleza kuwa majambazi hao walikuwa wapatao wanne wakiwa wamepanda piki piki,ghafla wakasimama na kulizunguka gari aina Vitz yenye usajili wa namba T929 CCX (pichani chini) kwa haraka,mmoja wao akiwa na mashine gun na wengine walikuwa na bastola.
 
Mmoja wao alifyatua risasi hewani kumtaka dereva asimame na ashushe vioo vya gari yake,kufuatia hali ya utata wa majibishano ya muda mfupi majambazi hao waliifyatulia risasi kadhaa gari hiyo upande wa dereva, bahati mbaya wakamjeruhi sehemu ya bega,ndipo wakafanikiwa kuondoka na begi kubwa linalosadikiwa kuwa lilikuwa na kiasi cha fedha shilingi milioni 40 (kwa mujibu wa dereva aliempeleka majeruhi hospitali).

Mara baada ya majambazi hayo kutimka wasamalia wema wakamchukua dereva huyo aliyekuwa akigugumia kwa maumivu ya jeraha lake na kumtafutia tax na hatimae kumkimbiza hospitali ya Kairuki kwa huduma ya haraka.
 Baadhi ya watu wakijaribu kubadilshana mawazo kwa kulitafakari tukio hilo la ujambazi.
 Gari iliyokuwa imevamiwa na majambazi ikikokotwa na gari la polisi mara baada ya kushindwa kuwaka.

MAAJABU HAYA, ASKARI ALIYENASWA NA MAGUNIA 18 YA BANGI HUKO HIMO AWATOROKA POLISI

ASKARI Polisi Koplo Edward, anayedaiwa kusafirisha dawa za kulevya (bangi) gunia 18 huko Himo, Kilimanjaro tarehe 18, Mei 2013, ametoroka chini ya ulinzi wa askari polisi saba na kutokomea kusikojulikana.

Mtuhumiwa huyo alikuwa dereva wa gari aina ya Toyota Landcruiser namba PT. 2025 la Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) Mkoa wa Arusha. 
 
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas alisema askari huyo akiwa chini ya ulinzi wa askari polisi saba, walikwenda nyumbani kwake kwa ajili ya ukaguzi, na walipofika nyumbani kwa  mtuhumiwa, walimwamini na kumwacha kuingia ndani peke yake nao waliingia ndani ili kuendelea na upekuzi, na ndipo mtuhumiwa alipofungua mlango wa nyuma ya nyumba yake na kukimbia bila ya wao kufanikiwa kumkamata
 

Alisema polisi imemkamata Inspekta wa Polisi Izaack Manoni aliyekuwa anasimamia upekuzi huo: “Inspekta Manoni yupo chini ya ulinzi na hatua za kinidhamu dhidi yake zitachukuliwa,” alisema ACP Sabas na kuongeza:  
“Mtuhumiwa Edward, anayetafutwa kwa sasa alishafukuzwa kazi, akipatikana atafikishwa mahakama ya kiraia kusomewa mashitaka ya kufanya biashara ya dawa za kulevya,” alisema.

Alisema tayari mtuhumiwa mwenzake ambaye ni askari polisi mwenye namba G. 2434 PC George, amesomewa mashitaka yake jana.

Mbali na mtuhumiwa huyo, watuhumiwa wengine waliokamatwa na magunia 30 ya bangi wilayani Arumeru nao wamepandishwa kizimbani kusomewa mashitaka yao.
 
CHANZO.MTANZANIA GAZETI

WANANCHI WATAKIWA KUPEWA ELIMU JUU YA UGONJWA WA FISTULA

 
(Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Hussein Mwinyi)
Wakati leo ni Siku ya Fistula duniani huku hafla ya kitaifa ikifanyika jijini Dar es Salaam Makao Makuu ya CCBRT, wakazi wa Morogoro wametaka kampeni ya fistula kusambazwa vijijini ili kutoa somo kwa wanawake wengi wenye matatizo hayo.
Fistula ni ugonjwa unawapata wanawake wengi kwa kutokwa na haja zote kwa wakati mmoja bila kujitambua. Kampeni ya kuelimisha umma kuhusu fistula ilyoanzia mkoani Kagera imeingia mkoani Morogoro ikiwa ni kampeni ya kuelimisha umma kuhusu fistula.
Wamesema ingawa walikuwa wakifahamu kuhusu tatizo la fistula, lakini elimu hiyo iliyohusisha ushuhuda kutoka kwa baadhi ya wanawake waliowahi kukumbwa na fistula na baadaye kupata matibabu imewapa uelewa na ufahamu mpana zaidi ambao ipo haja ya kuhakikisha ujumbe huo unafika kila kona ya nchi hususan vijini.
“Nimefurahi sana nimeelimika vya kutosha kuhusu fistula. Mwanzoni nilifika hapa kumshuhudia Msanii Mwana FA lakini mawazo yangu yalibadilika ghafla na kujikuta naguswa na elimu ya fistula.”alisema Emmanuel Nyangaka.
Kwa upande wake pamoja na kupongeza juhudi za Vodacom pamoja na kuuliza maswali kadhaa, mkazi mwingine Hassan Ndungate alisema elimu hiyo ni fusra ya kipekee kwa jamii kujua mambo mbalimbali yanayohusu fistula ili waweze kutoa msaada au na kuhamamisha jamii kujitokeza kupata matibabu.
Alishauri elimu hiyo iendelee hadi vijiji mbalimbali.     


ZISOME HAPA STORI KWENYE MAGAZETI YA LEO TAR 23 MAY.

DSC 0095 2a886DSC 0089 657b7DSC 0087 9656eDSC 0088 b82f0DSC 0090 80a25DSC 0091 7c7c9DSC 0086 40c77

Zilizosomwa zaidi