Thursday, April 18, 2013

BAADHI YA PICHA KWENYE MAZISHI YA BI KIDUDE....




                     Tulikupenda lakini Mungu amekupenda zaidi

                 Jeneza la bibi likielekea msikiti kwa ajili ya kusaliwa

Mtangazaji Hassan Bond, Fid Q, Diamond Platnumz na Ruge Mutahaba wakiwa msibani nyumbani kwamarehemu bi Kidude,  Zanzibar


Msanii Fid Q, Baraka cousin ya Marehemu Bi Kidude na Hassan Bond Mussa (FID Q ndo alikuwa msanii wa kwanza mkubwa kufika msibani kwa bibi)

              Ruge mutahaba, Babu Tale and Guru. .......msibani kwa Bi Kidude

                             Guru G na Mh Bhaa mazikoni

Hassan na Fid Q wakiwa katika picha ya pamoja na familia ya Marehemu Bi Kidude

Sehemu ya umati wa Watu waliofika msibani

HUKUMU YA SHEIKH PONDA BADO IKO NJIA PANDA..


HUKUMU ya Kesi inayomkabili Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu, Sheikh Ponda Issa Ponda, aliyekuwa akikabiliwa na kesi ya maandamano haramu bado iko njia panda baada ya kuaahirishwa mpaka tarehe 9 mei mwaka huu.
Kesi hiyo imeharishwa baada ya Hakimu  Mkazi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Victoria Nongwa ,kutokuwepo Mahakamani hapo.
Awali hakimu huyo alitarajiwa kuketi katika kiti cha enzi na kutoa hukumu ya kesi hiyo Na.245/2012 inayomkabili Ponda na wenzake. 
Aprili 3 mwaka huu, Mawakili wa upande wa Jamhuri ,Tumaini Kweka na Jessy Peter na mawakili wa utetezi Juma Nassor na Njama waliwasilisha majumuisho yao mahakamani hapo kwa njia ya maandishi ambapo mawakili wa upande wa jamhuri waliiomba mahakama iwaone washitakiwa wote wana hatia na wapewe adhabu kwa mujibu wa sheria.
Wakati mawakili wa utetezi waliiomba mahakama iwaone washitakiwa hawana hatia na iwaachilie huru kwa sababu hawakutenda makosa yanayowakabili na kwamba upande wa jamhuri umeshindwa kuthibitisha kesi yao.

HAPA NI BAADA YA LISU KUTIMULIWA KATIKA UKUMBI WA BUNGE HAPO JANA.

 
Tundu Lissu
Naibu Spika Ndugai jana  aliamuru Mbunge wa Jimbo la Singida Vijijini na Mwanasheria wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo,Tundu Lissu atolewe nje ya Bunge huku wabunge wa upinzani wakizomea na kusema hatoki mtu. 

Amri hiyo ilitokaea baada ya Lisu  kuingilia kati mchango wa Mwigulu Nchemba aliyesema kwamba udini ni jambo geni hapa nchini....
 Tanzania imeongozwa na CCM tangu uhuru, na marais wote wamekuwa wakitoka CCM, rais wa kwanza alikuwa mkristo, wa pili muislam, wa tatu mkristo na wa nne ni muislam..akasema kama udini ni jambo geni watanzania tujiulize limekujaje? Kwanini sasa na sio wakati huo?

Akasema katika kampeni za urais 2010 Dr Slaa akiwa katika kampeni mkoani singida alitumia viongozi wa dini kufanya vikao vya kampeni badala ya kutumia wanachama wa chama chake...na viongozi hao wapo tayari kutoa ushahidi...
Ndipo Tundu Lissu aliposimama na kuomba mwongozo, spika akamwambia atulie kwa sababu Susan Kiwanga tayari amepewa nafasi akalisemea hilo na muda ni mdogo Lissu akang'ang'ania ndipo Naibu Spika akaamuru askari amtoe nje Lissu.

Pamoja na hayo Naibu spika amewafungia vikao vitano kinyume na kanuni za Bunge Mh. Lema, Mh. Mbilinyi. Mh. Kiwia, Mh. Msigwa, Mh. Wenje

HIZI NDIO STORI KWENYE KURASA ZA MWANZO NA MWISHO WA MAGAZETI YA LEO ALHAMISI 18 APRIL

.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.

Zilizosomwa zaidi