Tuesday, April 2, 2013

JAY DEE APANIA KUANZISHA KITUO CHAKE CHA REDIO.

Hatimaye tumepata jibu la kwanini Judith Mbibo aka Lady Jaydee amekuwa akitweet vitu vizito weekend iliyopita. Kama hukufaniwa kuziona tweets hizo ni kwamba mwanadada huyo alishusha mfululizo wa mabomu kuelekea kwa kituo kimoja cha radio na kujikuta akiongeza aka mpya, Anaconda.

Na sasa imebainikiwa kuwa mwanamuziki huyo mkongwe na mjasiriamali anakuja na kituo chake cha radio kiitwacho Kwanza FM. Habari hiyo aliibreak mwenyewe jana na bila shaka haihusiani na April’s Fools Day.

    Kwanza FM coming soon. Yangu mwenyewee

    — Lady JayDee (@JideJaydee) April 1, 2013

Inaonesha kuwa mchakato wa kuanzisha radio hiyo unaenda vizuri kiasi cha kuweka wazi na kuwa hiyo ndio sababu alichukua uamuzi huo wa kuandika mambo ambayo yangeweza kuiharibu career yake ya muziki.

    Huwezi kuanza mapambano km hujajizatiti, si utapigwa ufe.? Vita ni pale tu unapokuwa tayari. Sikuwa tayari huko nyuma ndio maana sikuongea

    — Lady JayDee (@JideJaydee) April 1, 2013

Kila lakheri Lady Jaydee. Kwa usimamizi wa mumewe Gadner G Habash ambaye ana uzoefu mkubwa kwenye masuala ya radio, kituo hicho huenda kikafanya vizuri.
Source:Bongo5

HILI NDIO TAMKO LA SHIRIKA LA NYUMBA KUHUSU KIWANJA CHA GHOROFA LILILOANGUKA JUZI JIJINI DAR.

.
.Shirika la nyumba la Taifa NHC limekiri kwamba ndio mmiliki wa kiwanja kilichokua kimejengwa jengo la gorofa 16 ambalo liliporomoka siku kadhaa zilizopita Dar es salaam na kusababisha vifo vya watu 36 na kujeruhi 18.

Mkurugenzi Mkuu Nehemia Mchechu amesema kwa kawaida shirika la nyumba limekua likiingia ubia na watu binafsi wenye uwezo wa kujenga nyumba kama hizo ambapo liliingia ubia na kampuni ya ujenzi ya RAZA na kusaini mkataba wa kujenga jengo lenye gorofa 10 tu kwenye eneo hilo ingawa baadae kampuni hiyo iliomba kubadili mkataba ili wajenge gorofa 16.

Kuhusu umiliki kwa asilimia 25 kwenye jengo lililoporomoka, Mchechu amesema kwa ubia uliokuwepo walipaswa kupewa asilimia hizo baada ya ujenzi kukamilika na asilimia nyingine 25 wangepewa miaka kumi baadae kulingana na mkataba na hawakupaswa kuhusika kwenye gharama zozote wala taratibu za ujenzi.

Asema “february 15 2011 ndio walituandikia kwamba wanakusudia kuongeza gorofa zifike 16 na kwamba wanawasiliana na Mamlaka husika kwa ajili ya kupata vibali hivyo na wakifanikiwa wangeomba kuongezewa muda wa kumaliza mradi na pia baada ya kupata kibali wangetutaarifu kwa ajili ya kufanya marekebisho ya mkataba”
Kwenye line nyingine, NHC imeunda timu kwa ajili ya kufanya ukaguzi katika miradi yake yote ya ujenzi wa ubia ili kujihakikishia usalama wa majengo husika.

ICC KUSIKILIZA MASHITAKA YA UHURU, RUTO KUPITIA VIDEO

From left: ICC Chief Prosecutor Fatou Bensouda, William Ruto and President-elect Uhuru Kenyatta. Photos | AFP and FILE |
Badala ya Raisi wa Kenya Bw. Uhuru Kenyatta na mwenzake Ruto kwenda kusomewa Mashtaka yake katika moja kwa moja kaatika Mahakama ya Makosa ya Jinai (ICC), Kesi yao itasikilizwa kupiti picha za video wakiwa nchini Kenya.

Wakati wa kampeni za uchaguzi nchini Kenya, Uhuru aliiomba ICC kutumia picha za video katika kusikiliza kesi inayomkabili kama atashinda katika uchaguzi mkuu ili aendelee kuwaongoza wanainchi wa Kenya.

RUFAA YA ZOMBE KUSIKILIZWA APRIL 22.

Rufaa ya Jamhuri dhidi ya aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi wa Mkoa wa Dar es Salaam, Abdallah Zombe na askari wenzake wanane, sasa imepangwa kusikilizwa mwezi huu.

Awali rufaa hiyo ilipangwa kusikilizwa na Mahakama ya Rufani Desemba 11, 2012, lakini ilikwama kutokana na kuugua kwa Jaji Semistocles Kaijage ambaye alikuwa ni mmoja katika jopo la majaji waliopangwa kuisikiliza. Majaji wengine katika jopo hilo walikuwa ni, Jaji Nathalia Kimaro na Jaji Catherine Oriyo.
 
Hata hivyo kwa mujibu wa ratiba ya vikao vya mahakama hiyo vya mwezi April, sasa rufaa hiyo imepangwa kusikilizwa Aprili 22 na 23, 2013, kuanzia saa 3:00 asubuhi. Ratiba hiyo pia inaonyesha kuwa rufaa hiyo itasikilizwa na jopo la majaji watatu tofauti na wale wa kwanza. Majaji hao ni Edward Rutajangwa,  Salum Mbarouk na Bernard Luanda.
Zombe na wenzake walikuwa wakikabiliwa na mashtaka ya mauaji ya kukusudia ya wafanyabiashara watatu wa madini kutoka Mahenge mkoani Morogoro na dereva wa teksi wa Manzese jijini Dar es Salaam.
 Agosti 17, 2009, Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam  iliwaachia huru washtakiwa wote ikisema kuwa baada ya kusikiliza ushahidi na hoja za mawakili wa pande zote imeridhika kuwa washtakiwa hawakuwa na hatia.

NAULI YAPANDA KWA ASILIMIA 24..

 
(Abiria wakigombania kuingia katika daladala.)
Mamlaka ya Udhibiti wa Majini na Nchi Kavu (Sumatra), imepandisha nauli za daladala, mabasi ya kwenda mikoani, usafiri wa reli na tozo za majini kuanzia Aprili 12, mwaka huu.Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Sumatra, Ahmad Kilima alisema jana kuwa nauli za daladala zimeongezeka kwa asilimia 24.46 kwa kuzingatia maoni ya wadau na gharama za uendeshaji.

Kwa upande wa usafiri wa daladala nauli zimepanda kwa umbali tofauti kutoka Sh300 hadi 400, Sh350 hadi 450, Sh500 hadi 600, Sh650 – 750 na kwa wanafunzi kutoka Sh150 hadi 200 katika sehemu yoyote watakayokwenda.

Nauli za usafiri wa mabasi makubwa ya masafa marefu nauli hizo zimeongezeka kwa viwango tofauti. Mathalan kwa basi la kawaida kutoka Dar es Salaam kwenda Mbeya ni Sh30,700, njia ya vumbi kutoka Kigoma hadi Sumbawanga Sh25,400 na basi la hadhi ya kati (Semi Luxury) kati ya Dar na Mwanza ni Sh61,400, wakati basi la hadhi ya juu (Luxury) kati ya Dar na Arusha ni Sh 36,000.

Kilima alisema: “Kuanzia Aprili 12 mwaka huu, kati ya kilometa 0 hadi 10, nauli ya daladala itakuwa Sh400 badala ya Sh300 zinazolipwa hivi sasa.
“Pia nauli za mabasi ya kwenda mikoani zimeongezeka kwa asilimia 20.3 kwa mabasi ya kawaida, mabasi ya kati kwa asilimia 16.9 na mabasi ya daraja la juu kwa asilimia 13.2,” alisema.

Kilima alisema nauli za mabasi ya mikoani zimepanda kutoka Sh30.67 hadi Sh36.89 kwa kilometa kwa mabasi ya daraja la kawaida katika njia za lami.
Kwa upande wa mabasi ya kawaida kwa njia ya vumbi imepanda kutoka Sh37.72 hadi Sh 46.11 kwa kilometa na kwamba mabasi ya hadhi ya kati, nauli zimepanda kutoka Sh45.53 hadi Sh 53.22 kwa kilometa.

Alisema mabasi ya hadhi ya juu nauli zimepanda kutoka Sh51.64 hadi Sh58.47 kwa kilometa.
“Kupanda kwa nauli kunatakiwa kwenda sambamba na huduma bora na kwamba Sumatra imepiga marufuku kutumia wapigadebe kuuza tiketi za safari”alisema.

Usafiri wa Reli
Katika uamuzi huo, usafiri wa reli pia umepanda ambapo daraja la kwanza Dar es Salaam hadi Morogoro, nauli mpya na ya zamani katika mabano ni Sh21,100, (Sh16,852), Dar hadi Dodoma Sh34,700, (Sh27,788), Dar es Salaam-Tabora Sh54,800, (Sh43,859).
Dar es Salaam-Isaka Sh62,100, (Sh49,662), Dar- Shinyanga Sh65,300 (Sh52,229) Dar –Mwanza Sh74,800 (Sh 59,818), Dar- Kigoma Sh75,700, (Sh60,599)

Daraja la pili, Dar es Salaam-Morogoro Sh16,600, (Sh13,280), Dar es Salaam-Dodoma Sh26,400 (Sh 21,092), Dar es Salaam-Tabora Sh40,500 (Sh 32,364), Dar es Salaam-Isaka Sh45,800, (Sh36,605), Dar es Salaam-Shinyanga Sh48,000 (Sh38,390), Dar es Salaam- Mwanza Sh54,700 (Sh43,747), Dar es Salaam-Kigoma Sh55,400 (Sh44,305).

Daraja la tatu, dar es Salaam-Morogoro Sh8,800 (Sh6,138), Dar es Salaam-Dodoma Sh13,500 (Sh9,374), Dar es Salaam-Tabora 20,400 (Sh14,173), Dar es Salaam-Isaka Sh22,800 (Sh15,847), Dar es Salaam –Shinyanga Sh24,000 (Sh16,628), Dar es Salaam-Mwanza Sh27,200 (Sh18,860), Dar es Salaam- Kigoma Sh27,500 (Sh19,084).

Akizungumzia tozo za majini, Kaimu Mkurugenzi huyo alisema mamlaka hiyo imeridhia ongezeko la tozo la asilimia 34.3 kwa vyombo vinavyotumia bandari za Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA).

Awali TPA walipendekeza tozo hizo kuongezeka kati ya asilimia saba hadi 400 kulingana na aina ya huduma zinazotolewa kwa meli zinazotumia bandari za mamlaka hiyo.

VIWANGO VIPYA VYA NAULI KAMA VILIVYOTANGAZWA NA SUMATRA HIVI HAPA.


Kaimu Mkurugenzi wa

SUMATRA

Athman Kilima akizungumza

na waandishi wa habari leo

April 02,2013

katika makao makuu ya

taasisi hiyo wakati akitangaza

kupanda kwa viwango vya

nauli ya mabasi ya mikoani

na Daladala.

Viwango hivi Vipya vya nauli ya Mabasi ya mikoani vitaanza kutumika kuanzia tarehe 12 Aprili, 2013. 

Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA) imekamilisha mchakato na kuridhia viwango vipya vya nauli kwa ajili ya usafiri wa mijini na usafiri wa kwenda mikoani.

   
 Viwango hivi vipya vimefikiwa baada ya kufuata taratibu za kisheria na za kiutendaji ambazo SUMATRA kama msimamizi na mdhibiti wa sekta ya usafiri wa barabara inapaswa kuzifuata kabla ya kuridhia viwango hivyo.


 Viwango vipya vya nauli vitaanza kutumika kuanzia tarehe 12 Aprili, 2013.


SUMATRA ina wajibu kisheria kuhakikisha pamoja na mambo mengine kuwa maslahi ya watumiaji na watoa huduma za usafiri yanalindwa ili kuwepo na huduma endelevu ya usafiri ulio bora, salama na wenye kukidhi mahitaji. Aidha SUMATRA ina jukumu la kujenga na kulinda mazingira mazuri na ya kuvutia kwa watoa huduma ili huduma ya usafiri inayotolewa inakuwa katika kiwango na gharama zinazoendana na huduma zenyewe.


Katika kipindi cha mwaka wa fedha wa 2011/2012, SUMATRA ilipokea maombi rasmi kutoka kwa wamiliki wa vyombo vya usafiri wa barabara yakiwemo makampuni ya usafirishaji abiria ya Cordial Transport Services P.L.C, Happy Nation Co. Ltd, ABC Trans na Mwesigwa Mtazaha Kazaula yakipendekeza mapitio ya viwango vya nauli za mabasi yanayotoa huduma za usafiri mijini (Daladala) na mabasi yanayotoa huduma katika Mikoa kufuatia ongezeko la gharama za uendeshaji kwa mujibu wa mawasilisho yao.


Wakati maombi ya wamiliki wa Daladala yalilenga katika kuongeza viwango vya nauli kwa 149% ya viwango vya sasa, wamiliki wa mabasi ya masafa marefu waliomba nyongeza kati ya 35% na 48.5%.


Kwa mujibu wa Kifungu Na 18 cha Sheria ya SUMATRA, 2001, SUMATRA iliwashirikisha wadau mbalimbali katika kujadili na kupata maoni yao kuhusu maombi ya wamiliki ya kuongeza viwango vya nauli kabla ya kufanya maamuzi ya mwisho.

Aidha Mamlaka iliridhia viwango vipya kwa mujibu wa kifungu cha 16 Cha Sheria ya SUMATRA ambacho kinaipa Mamlaka kufanya mapitio ya nauli mara kwa mara kwa kuzingatia gharama za kutoa huduma, maslahi ya watoa huduma, faida, maslahi ya watumia huduma ya kulipa nauli yenye uwiano na gharama za huduma inayotolewa.


Kwa kuzingatia hoja za waombaji, maoni ya wadau, uchambuzi wa menejimenti, haja ya kupunguza gharama zisizo za lazima za uendeshaji na udhibiti wa vitendo vya uvunjaji wa Sheria na taratibu za uendeshaji shughuli za usafirishaji, Mamlaka ya SUMATRA iliamua kuongeza viwango vya juu vya nauli za Daladala kwa wastani wa 24.46%.


Aidha kwa mabasi ya masafa marefu, viwango vimeongezwa kwa 20.3% kwa mabasi ya kawaida, 16.9% kwa mabasi ya daraja la kati na 13.2% kwa mabasi ya daraja la juu.


Mchanganuo wa viwango vipya vya nauli ni kama ifuatavyo:

1.     Nauli za Daladala – Jiji la Dar es Salaam

Umbali wa Njia
Kiwango Kipya cha Nauli
Mfano wa Njia
Kilomita kati ya 0 – 10 (Na mipaka ya Jiji Kati)
Sh 400/=
Ubungo – Kivukoni
Kilomita kati ya 11 – 15
Sh 450/=
Mwenge – Temeke
Kilomita kati ya 16 – 20
Sh 500/=
Tabata Chang’ombe – Kivukoni
Kilomita kati ya 21 – 25
Sh 600/=
Pugu Kajiungeni – Kariakoo
Kilomita kati ya 26 – 30
Sh 750/=
Kibamba – Kariakoo

Mamlaka imeandaa majedwali kwa njia zote za Dar es Salaam. Majedwali hayo yanaweza kupatika katika tovuti yetu www.sumatra.or.tz.


Nauli ya Mwanafunzi itakuwa Sh 200/= ambayo ni nusu ya nauli ya mtu mzima ya kiwango cha chini cha nauli ya Sh 400/=. Nauli hii itatumika kwa njia zote za Jiji la Dar es Salaam.

2.     Nauli za Mabasi ya Masafa Marefu

Daraja la Basi
Nauli ya zamani kwa km-abiria
Nauli mpya kwa km-abiria
Mfano wa kiwango kipya cha nauli kwa baadhi ya njia
Basi la Kawaida kwa njia ya lami
Sh 30.67
Sh 36.89
DSM–Mbeya Km 833
Sh 30,700
Basi la Kawaida kwa njia ya vumbi
Sh 37.72
Sh 46.11
S/wanga-KigomaKm 551
Sh 25,400
Basi la hadhi ya kati (Semi Luxury
Sh 45.53
Sh 53.22
DSM–Mwanza Km 1,154
Sh 61,400
Basi la hadhi ya juu (Luxury)
Sh 51.64
Sh 58.47
DSM–Arusha Km 616
Sh 36,000

Ili kuhakikisha kuwa kuna uwiano kati ya viwango vipya vya nauli na ubora wa huduma ya usafiri, Mamlaka imetoa maagizo kwa wamiliki wa mabasi ya masafa marefu kuboresha maeneo yanayohusiana na huduma ya usafiri kama ifuatavyo:

1.     Wamiliki wa mabasi kutokutumia wapiga debe katika kuuza tiketi za safari
2.     Wamiliki wa mabasi kuhakikisha wanafuata Kanuni za SUMATRA za Udhibiti wa Tozo na Nauli (SUMATRA Tarrif Regulations) ambazo zinahimiiza kuwepo kwa kumbukumbu sahihi za mahesabu ili kurahisisha mapitio ya viwango vya nauli
3.     Kufuata Sheria, Kanuni na Masharti ya Leseni ya usafirishaji abiria
4.     Kutoza nauli kwa mujibu wa daraja la basi lenye sifa kamili la daraja husika kama ilivyoainishwa katika Kanuni za Usalama na Ubora

Aidha kwa mabasi ya mjini, Mamlaka imetoa maelekezo yafuatayo:

5.     Kuhakiksha kuwa abiria wote wanapatiwa tiketi
6.     Kudhibiti vitendo vya ukiukwaji wa Sheria ikiwemo kutokamilisha safari maarufa kama kukata ruti, kubadili njia na unyanyasaji wa aina yoteyote kwa abiria
7.     Kutokutumia wapiga debe
8.     Wafanyakazi wa mabasi kuvaa sare nadhifu wakati wote.

Mamlaka ya SUMATRA inaendelea kuimarisha ushirikiano kwa kufanya kazi kwa karibu na Mamlaka zingine kama Wakuu wa Mikoa, Serikali za Mitaa, Mamlaka za Miji, Polisi, TBS, TANROADS, Kamisheni ya Bima na wananchi kwa ujumla, katika kuleta mageuzi kamili ya utoaji wa huduma za usafiri wa barabara kwa kiwango cha juu.


A.S.K. Kilima
KAIMU MKURUGENZI MKUU
2 Aprili, 2013

KAMA UNADHANI MAREKANI HAKUNA OMBAOMBA ANGALIA HAPA..



(Mmoja wa ombaomba huko U.S.A)
Sasa hali ya umaskini unaongezeka nchini marekani. Idadi ya watunanaopata chakula cha msaada imeongezeka ka asilimia 70 tangu mwaka 2008 kwa takribani watu millioni 50.
Uchunguzi unaonesha kuwa tangu kuporomoka kwa uchumi Marekani, hali ya watu inazidi kuwa ngumu.


STORI KWENYE MAGAZETI YA LEO NDIO HIZI HAPA....

.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
DSC03773
.
.
.
.
.

Zilizosomwa zaidi