Friday, March 29, 2013

MTUHUMIWA WA MAUAJI YA PADRI EVALIST MUSHI AKAMATWA ZANZIBAR

MTU ANAESADIKIWA KUWA NDIE MUUAJI WA PADRI EVALIST MUSHI WA KANISA KATOLIKI,VISIWANI ZANZIBAR,AMEKAMATWA ALASILI HII MAENEO YA KARIAKOO,ZANZIBAR.

JESHI LA POLISI LIMETHIBITISHA KUKAMATWA KWA MTUHUMIWA HUYO,NA KWENDA NAE KITUONI KWA AJILI YA MAHOJIANO ZAIDI.

PADRI MUSHI ALIUWAWA KWA KUPIGWA RISASI MWEZI ULIOPITWA WAKATI AKIWA KWENYE GARI LAKE KUELEKEA KANISANI KWENYE IBADA YA JUMAPILI.

UTAPATA TAARIFA HII KWA KINA ZAIDI.
CHANZO: Michuzi blog

RAIS ATEMBELEA ENEO LA INDIRA, IDADI YA WATU WALIOFARIKI HUKO DAR BAADA YA GOROFA KUPOROMOKA IMEONGEZEKA....!

Mpaka sasa watu watatu wamepatikana 

wakiwa wamefariki

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwasili mtaa wa Indira Ghandi jijini Dar es salaam leo akiwa ameongozana na mkewe Mama Salma Kikwete kujionea mwenyewe jengo lililoporomoka asubuhi saa mbili na nusu leo Machi 29, 2013 ambapo hadi Rais anafika mahali hapo saa saba kamili watu wawili wamethibitishwa kuwa wamekufa na wengine 19 kujeruhiwa, wawili wakiwa mahututi. Juhudi zinaendelea kuokoa watu wanaosadikiwa kunaswa kwenye kifusi cha jengo hilo lililokuwa limefikia ghorofa ya 15, likijengwa ubavuni mwa Msikiti wa Shia Ithnaasheri.



Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipata maelezo toka kwa Mkuu wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam Bw. Suleiman Kova na Mkuu wa Mkoa huo Mhe saidi Meck Sadiki katika eneo la jengo lililoporomoka mtaa wa Indira Ghandi jijini Dar es salaam asubuhi saa mbili na nusu leo Machi 29, 2013 ambapo hadi Rais anafika mahali hapo saa saba kamili watu wawili wamethibitishwa kuwa wamekufa na wengine 19 kujeruhiwa, wawili wakiwa mahututi. Juhudi zinaendelea kuokoa watu wanaosadikiwa kunaswa kwenye kifusi cha jengo hilo lililokuwa limefikia ghorofa ya 15, likijengwa ubavuni mwa Msikiti wa Shia Ithnaasheri.

UNAJUA ATHARI ZA MARASHI NA SABUNI KWA MWANAMKE?...SOMA HAPA UJUE YALIYOMO.

Wanawake ni miongoni mwa wanajamii wengi wanaopenda kutumia marashi na vitu vingine kama sabuni zenye kemikali kwa ajili ya kujirembesha.
Pia, wanawake wamekuwa wakipenda usafi wao binafsi, wakitumia vitu  ambavyo baadhi yake ni hatari.
Wapo baadhi ya wanawake wanaopenda kusafisha sehemu zao za siri kwa kutumia sabuni zenye kemikali, marashi (pafyumu) au kupaka mafuta.
Kwa maelezo ya wataalam, hao wapo hatarini kupata magonjwa ya zinaa au ya kuambukiza.
Watafiti katika Chuo Kikuu cha California, Marekani wanasema sabuni ngumu au hata za maji, pafyumu (deodorant) zinaharibu tishu muhimu zilizomo ndani kabisa ya uke na kumweka mhusika katika hatari ya kupata malengelenge, fangasi  na hata Ukimwi.
Aidha, sabuni au dawa zinazouzwa na wafanyabiashara zikitangaza kuboresha uke au kuondoa harufu kwenye sehemu hizo nyeti nazo zimeelezwa kuwa na madhara.

 Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Wanawake katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Cyriel Massawe anasema sabuni au mafuta yenye kemikali  huchubua  ngozi laini ya uke na ni rahisi vimelea vya magonjwa kuenea kwa urahisi.
Dk Massawe anasema michubuko hiyo ambayo si rahisi kuonekana kwa macho ndicho chanzo cha kuingia kwa maradhi ya kuambukiza.
“Hamna haja ya kuweka kemikali, au pafyumu ukeni. Hizo sehemu zinahitaji kuoshwa vizuri kwa maji,” anasema Dk Massawe.
Anasema kemikali inapoingia ukeni inavuruga hali ya kawaida na asidi inayolinda sehemu hizo.
Anaongeza  kuwa ni vyema wanawake wakaelimishwa kuhusu matumizi ya  bidhaa zinazodaiwa kuweka harufu nzuri  katika sehemu zao za siri, kurudisha bikira au mafuta ya kulainisha uke.
Naye Daktari Bingwa wa Kitengo cha Patholojia MNH, Henry Mwakyoma anasema wanawake wanaofanya usafi sehemu zao za siri kwa kutumia bidhaa au baadhi ya vifaa visivyofaa kutumiwa ukeni huweza kupata saratani ya shingo ya uzazi.
Dk Mwakyoma aliyewahi kufanya utafiti kuhusu saratani ya shingo ya kizazi nchini anasema, bidhaa zenye kemikali ya ‘coal tar,’ ambazo mara nyingine huwekwa kwenye sabuni ama manukato na kutumiwa ukeni na wanawake huweza kuchochea saratani hiyo.
Kiongozi wa utafiti huo, Dk Joelle Brown, alisema upo ushahidi wa kutosha kuwa kutumia sabuni za kuogea za maji au ngumu katika sehemu za siri za ndani za mwanamke kunaharibu uwiano wa bakteria na kusababisha bakteria kuzalishwa kwa wingi na kumweka mwanamke katika hatari ya maradhi ya  zinaa ya kuambukiza.
Chanzo:Mwananchi

HIKI NDIO KIKOSI CHA MASS COMMUNICATION UMITED KUTOKA SAUT, MWANZA

   
Kikosi cha Mass communication United wakiwa tayari kucheza na watoto wa Cheti

 


Hapa ni katika mashindano ya FAWASCOyaliyoanza wiki mbili zilizopita katika Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino (SAUT) jijini Mwanza.

Mass Communication United wameingia katika michuano hii kwa mwaka huu wakiwa na kumbukumbu ya kujinyakulia nafasi ya pili kwa msimu wa mwaka jana.

Akiongea Maneger wa timu hiyo Mr. Charz, amesema kwa mwaka huu wamejipanga vizuri kabisa kwa kulitwaa kombe.''Tangu tulivyoanza mashiundano tumepoteza mechi moja''

 



Goli kipa wa timu ya Mass communication(Abuu Juma) wakati wa mazoezi


Baadhi ya mashsbiki kutoka Mass Communication 2

Meneja wa timu ya Mass Communication akiwangalia vijana wake  


Baadhi ya wachezaji wakisubili kuingia(Sub)


Hawa ni mashabiki wakiamsha amsha wakati mchezo unaendelea



Zilizosomwa zaidi