Monday, March 25, 2013

MESSAGE ZA UCHOCHEZI KUENEA MTANDAONI, TCRA KUCHUKUA HATUA MADHUBUTI.

 

Ujumbe mfupi wa maneno (SMS) wenye mlengo wa ubaguzi wa kidini dhidi ya serikali, umekuwa ukitawanywa kwa fujo, ule wenye sura ya Kiislam ukisindikizwa na maneno “watumie Waislam wenzako” na wa Kikristo ukielekeza “watumie Wakristo wenzako.”

Uchunguzi wetu umebaini kuwa baadhi ya watu ambao tunaamini wakisakwa watapatikana, wamekuwa wakitunga na kusambaza ujumbe mfupi kwa watu mbalimbali, wakiwahamasisha kuhusu jambo fulani kwa masilahi ya dini zao.


SMS hizo , zimekuwa zikikosoa serikali kwamba muundo wake upo kiupendeleo, zile zenye sura ya Kikristo zikidai Waislam wanapendelewa, vilevile za Kiislam zikidai Wakristo wanapendelewa. 


Baadhi ya waandishi wetu ni miongoni mwa waliotumiwa ujumbe na watu hao ambao wanaweza kulitia doa taifa letu ikiwa hatua za dharura hazitachukuliwa.

Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni, ACP Charles Kenyela.

Ujumbe unaosambazwa na watu hao una lengo la kuigawa nchi katika misingi ya kidini, hali ambayo kwa mpenda amani yeyote hawezi kukubali au kufurahia kwani wanaofanya hivyo wanahatarisha usalama na umoja wetu wa kitaifa.

Uchunguzi wetu umebaini kuwa baadhi ya wananchi waliotumiwa ujumbe wa aina hiyo wameonesha wasiwasi wao kwa vyombo vya usalama hasa polisi, Idara ya Usalama wa Taifa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kama wana habari kuchukua hatua.

“Siku za hivi karibuni kila mara ujumbe mfupi wa uchochezi husambazwa kwenye simu na watu wasiofahamika, mbaya zaidi vyombo vya dola havijasema chochote, ina maana hawana habari?” alihoji kijana mmoja aliyeomba jina lake kuhifadhiwa.

Mwananchi mwingine mkazi wa Mwenge Mlalakua jijini Dar es Salaam alikiri kupokea ujumbe wenye maneno ya uchochezi lakini akasema hajafanya kama alivyoelekezwa na mtumaji.
“Mtumaji ameandika aliyotaka kuandika kisha akanitaka nitume kwa watu wa dini yangu kumi, sikufanya hivyo maana niliona kuwa huu ni uchochezi,” alisema.

SMS hizo, zinataja asilimia ya viongozi waliopo madarakani kwamba ni wa dini fulani kisha ujumbe wenyewe unaonya kwamba muundo wa serikali ni hatari kwa usalama wa taifa bila kutaja sababu za hatari hiyo.

Hata hivyo, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni, ACP Charles Kenyela ametoa wito kwa yeyote ambaye atatumiwa ujumbe wa uchochezi kutoa taarifa kwake ili watu hao washughulikiwe.

“Kusambaza ujumbe wa uchochezi kwa kutumia simu au kitu chochote ni uhalifu na mhusika akikamatwa anashitakiwa, hivyo yeyote atakayetumiwa ujumbe wa uchochezi namkaribisha ofisini kwangu ili wahalifu hao washughulikiwe,” alisema Kenyela.

6 WAFARIKI KATIKA MAPOROMOKO HUKO INDONESIA...!

Waokoaji nchini Indonesia
Mvua kubwa iliyonyesha nchini Indonedia imesababisha vifo vya watu sita  na wengine 18 hawajulikani walipo baada ya ardhi kuporomoka katika kisiwa cha Java nchini humo.
Mamia ya polisi, wanajeshi na umma wamekuwa wakichimba magofu wakiwatafuta walionusurika..

CHEKI HAPA NA KATUNI ZA MPANGALA....!

MADARAJA MAPYA YA KUFAULU KIDATO CHA NNE HAYA HAPA.


Serikali kwa kupitia Wizara ya Elimu
 imefanya mabadiliko kwenye Madaraja ya 
alama za mitihani ya kidato cha nne.


Hapo awali  Madaraja yalikuwa hivi;
A = 81% - 100% 

B = 61% - 80% 

C = 41% - 60% 

D = 21% - 40% 

F = 0% - 20% 
Mabadiliko mapya yamefanywa na sasa 
Madaraja MAPYA ni kama ifuatavyo:
A = 80% - 100% 

B = 65% - 79% 

C = 50% - 64% 

D = 35% - 49% 

F = 0% - 34% 
Taarifa imetolewa mapema ili wanafunzi kwa
 kidato cha nne waanze kujiandaa vyema na 
mitihani ijayo.

BAADA YA KAJALA KUACHIWA HURU, HALI ILIKUWA HIVI NJE YA MAHAKAMA YA KISUTU.


Wema Sepetu leo amejizolea umaarufu wa kutosha baada ya kutoa mfukoni mwake shilingi milioni 13 kulipa faini aliyopigwa muigizaji mwenzie Kajala Masanja ambaye hukumu yake ilikuwa imetolewa  kwenda jela miaka mitano ama kulipa kiasi hicho cha fedha.
Kajala na Wema wakikumbatianaKajala na Wema wakikumbatiana
Akiongea  kwa  kujiamini, Wema amesema hakufikiria mara mbili kutoa kiasi hicho cha fedha.

“Kusema kweli wanasemaga kwamba kutoa ni moyo so naamini what I did is best, nimetoa kwasababu I had to do it and sikuthink twice kuhusu kufanya hivyo,”
 amesema Wema.
Wema akwa na KajalaWema akiwa na Kajala
 
“Nimefanya kama namsaidia rafiki yangu, ndugu yangu na sidhani kama ingekuwa ni kitu kizuri kumuona mwenzako anaingia kwenye dhahama, kwenye tabu, kwenye mateso na wakati nina uwezo wa kumsaidia kwahiyo I just did what I had to do.”

Kuachiwa kwa Kajala kumepokelewa kwa furaha kubwa na mastaa mbalimbali nchini.


Kajala akikumbatiana na ZamaradiKajala akikumbatiana na Zamaradi

WANAWAKE NA CHANGAMOTO YA KUMILIKI ARDHI....!

Naibu waziri wa katiba na sheria Bi. Angela Kairuki amesema richa
ya kuwa wanawake wamepewa fursa za wazi kabisa kisheria katika
kumiliki ardhi, bado umiliki wa ardhi ni mdogo sana nchini.

Kauli hiyo imetolewa leo wakati wa semina  ya Chama Cha Wanawake
 nchini (TAWLA) juu ya umiliki wa ardhi kwa wanawake na uwekezaji
 iliyofanyika jijini Dar es salaam.

Naibu waziri huyo amesema kutokana na muamko mdogo wa wanawake
kumiliki ardhi kwa kiasi cha juu, ndio kunawafanya washindwe kutumia
fursa za kisheria za kumiliki ardhi.

HAYA NDIO YALIYOJILI KESI YA KAJALA..

Muigizaji Kajala Masanja ambaye leo hukumu yake imesomwa katika mahakama ya hakimu mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam.amehukumiwa kwenda jela miaka mitano au kulipa faini ya shilingi milioni 13 na mumewe kwenda jela miaka saba au kulipa faini ya shilingi milioni 200.

 Taarifa kutoka mahakamani zinadai kuwa wasanii wa bongomovie wanachanga fedha hizo ili wazilipe na tayari inasemekana Wema Sepetu amezitoa fedha hizo zote kutoka mfukoni mwake.

Kajala na mumewe Faraja Chambo walikuwa wakikabiliwa na makosa matatu ambayo ni pamoja na kula njama ambapo washtakiwa wote kwa pamoja walitenda kosa kwa kuhamisha umiliki wa nyumba iliyopo Kunduchi Salasala jijini Dar es Salaam. 


MATOKEO YA TIMU ZOTE KATIKA KUFUZU KUSHIRIKI KOMBE LA DUNIA 2014 NDIO HAYA.

Group A FT Ethiopia 1 - 0 Botswana Group B FT Equatorial Guinea 4 - 3 Cape Verde Islands Group C FT Tanzania 3 - 1 Morocco Group D FT Lesotho 1 - 1 Zambia FT Ghana 4 - 0 Sudan Group G FT Mozambique 0 - 0 Guinea Group H FT Rwanda 1 - 2 Mali Group I FT Congo DR 0 - 0 Libya

Zilizosomwa zaidi