Tuesday, March 19, 2013

KASHFA YAIBUKA TENA IKULU.......

 
Sakata la Mkuu wa Itifaki wa Ikulu, Anthony Itatiro, ambaye anahusishwa na njama za kutaka kuchota kiasi cha Sh3 bilioni kwa ajili ya safari hewa ya Rais, limechukua sura mpya baada ya Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje kutaka kujua hatima ya kigogo huyo jana.

Itatiro na maofisa wanne wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa walituhumiwa mwaka jana kuidhinisha kuchota kiasi hicho cha fedha bila ya kuwapo kwa ziara ya Rais kwenda nchi yoyote ya kigeni.

Mpango huo unadaiwa kusukwa Juni mwaka jana kwa maofisa haokuitaka Wizara ya Fedha kutoa kiasi hicho cha fedha kwa ajili ya safari hewa ya Rais.

Naibu Waziri wa wizara hiyo, Juma Mahadhi alitoa maelezo hayo baada ya kuulizwa swali na Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo ya Nje ya Bunge, Edward Lowassa.

Lowassa, ambaye pia ni Mbunge wa Monduli aliuliza swali hilo ghafla kwa Mahadhi wakati akitoka nje, baada ya kumalizika kwa kikao cha kamati yake kilichofanyika kwenye ofisi za Bunge jijini Dar es Salaam.

Mahadhi, ambaye alilazimika kutoa ufafanuzi wa swali hilo baada ya kubanwa zaidi na waandishi wa habari, alisema Rais Kikwete ndiyo mwenye mamlaka ya kuchukua hatua dhidi ya Itatiro kutokana na ripoti ya uchunguzi ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) na Mkaguzi wa Ndani wa Wizara hiyo.

Alisema pia kuwa walishauriwa kuwa maofisa walioshirikiana na Itatiro nao wachukuliwe hatua za kinidhamu kufuatia njama hizo.

Alipotafutwa kuzungumzia suala hilo, Katibu Mkuu Ombeni Sefue hakupokea simu. Pia hakujibu pindi alipotumiwa ujumbe mfupi kwa njia ya simu. Naye Katibu Mkuu katika Ofisi ya Rais anayeshughulikia Utumishi, George Yambesi alisema hakuwa tayari kuzungumzia suala hilo kwani alikuwa likizo.

Mahadhi alisema wakati tukio hilo linatokea viongozi wakuu wa wizara hiyo walikuwa kwenye majukumu mengine ya Serikali, jambo ambalo lilisababisha nafasi zao kukaimiwa na watendaji hao.

“Wale maofisa walitumia mwanya wao wa kukaimu nafasi ile ndiyo wakasuka mpango huo,” aliongeza Mahadhi.

Alisema kutokana na hali hiyo baadhi ya maofisa hao wamechukuliwa hatua za kinidhamu ikiwamo ya kuwashusha vyeo na kuwabadilisha vitengo.

Mahadhi alisema kwamba huwa ni utaratibu wa kawaida kwa Rais anaposafiri maofisa wa Itifaki na wale wa Wizara ya Mambo ya Nje kupewa fedha na hazina kwa ajili ya kufanikisha ziara zake.

Chanzo: Mwananchi.

ZISOME HAPA STORI ZOTE KUBWA KWENYE MAGAZETI YA LEO TAR 20 MARCH...Uraisi wa damu, Wizi wa bil.4, Lowasa amtikisa Membe,

.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.

HUYU NDIO KIJANA ALIYEMUUA MAMA YAKE KWA SHOKA MKOANI MOROGORO.



Frank Hillary, 27 (t-shirt ya kijani hapo chini), aliyetambuliwa kuwa mlokole, amethubutu na kuweza kukatisha maisha ya mama yake, Ndolukasi Lugamo, 50, akitumia shoka kuondoa uhai wa mzazi wake. 


Tukio hilo, lilitokea Alhamisi iliyopita, Mtaa wa Malipula, Kata ya Chamwino, mkoani Morogoro na inadaiwa kwamba kabla ya mauaji, Hillary alimpiga vibao, mitama na mateke mama yake.


Mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo, Pili Athuman, alidai kwamba siku ya tukio, kulitokea mabishano kati ya Hillary na mama yake.

“Yalikuwa mabishano kidogo lakini ghafla yule kijana alimvamia mama yake na kuanza kumpiga,alisema Pili na kuongeza:


“Yule kijana ni mtoto wa pekee wa yule mama. Tunashindwa kuelewa mpaka sasa chanzo cha tukio hilo. Halafu wale watu ni walokole kabisa na siku zote walikuwa wanaishi kwa upendo.”


Shuhuda mwingine, Julius Josephat alisema: “Mimi nashindwa kuelewa. Huyu marehemu na mwanaye walikuwa wanapendana sana, wakienda kanisani wanaongozana kama kumbikumbi.


“Kinachosikitisha zaidi ni kuwa mama yake aliumia mkono kama siku tatu kabla, akawa amefungwa plasta ngumu (POP), nahisi ndiyo maana alishindwa kujiokoa.”


Naye Maria Maswika ambaye nyumba yake imepakana na ile ya mama Hillary, alieleza: “Leo (Alhamisi),  saa 4 asubuhi nilimsikia huyo mama akipiga kelele za kuomba msada, huku akiingia nyumbani kwangu.

“Nilipotoka chumbani, nilishuhudia kwa macho yangu yule kijana akimpiga shoka mama yake na kumuua palepale. Sababu ya ugomvi wao siielewi. Kwanza nashangaa sana, kwani yule mama wa watu alikuwa anampenda sana mtoto wake.”



Mwandishi wetu alifika eneo la tukio mapema na kushuhudia wananchi wakimkamata Hillary, kumfunga kamba kabla ya polisi nao kuwasili, kuandika maelezo na kumchukua mtuhumiwa huyo wa mauaji ya mama yake mzazi.


Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Morogoro, ACP Faustine Shilogile, alisema: “Uchunguzi zaidi wa tukio unaendelea na utakapokamilika, tutamfikisha mtuhumiwa mahakamani.”


Kitu kilichowashangaza wengi eneo la tukio ni paka anayetajwa kumilikiwa na marehemu ambaye baada ya mama huyo kuuawa, yeye alikwenda kulamba damu kisha akalala kichwani kwenye mwili wa marehemu.

AJARI YAUA 6, NA WENGINE 30 KUJERUHIWA VIBAYA MWANZA.

Basi la Makwizi lililokuwa likitokea Nata wilayani  Serengeti mkoani Mara,  lenye namba za usajili T961 AGP limepata ajali mbaya leo katika eneo la Nyamongolo nje kidogo ya jiji la Mwanza, mara baada ya kugongana na Tipa la mchanga lenye namba za usajili T 971 BYJ na kusababisha ajali hiyo iliyopelekea watu wawili kufariki dunia (wote walikuwa kwenye tipa) na abiria mmoja aliyekuwa amekaa mbele kushoto kwa dereva kwenye  bus hilo, Dereva wa gari hilo amevunjika miguu na amefikishwa katika Hospitali ya Rufaa Bugando. 
Wananchi wakiwa wamelizunguka bas la Makwizi lililokuwa likitokea Nata maeneo ya wilaya ya Serengeti mkoani Mara,  lenye namba za usajili T961 AGP limepata ajali mbaya katika eneo la Nyamongolo nje kidogo kuingia jijini Mwanza, mara baada ya kugongana na Tipa la mchanga lenye namba za usajili T 971 BYJ na kusababisha ajali hiyo iliyopelekea watu wawili kufariki dunia (wote walikuwa kwenye tipa) na abiria mmoja aliyekuwa amekaa mbele kwenye  bus hilo, Dereva wa gari hilo amevunjika miguu yuko hoi Hospitali ya Rufaa Bugando. 

KAMA BADO HUJAIJUA BODI YA WADHAMINI WA CLUB YA YANGA, ICHEKI HAPA.















Wajumbe wa Bodi ya wadhamini kutoka kushoto ni Francis Kifukwe, Captain George Mkuchika na Balozi Ami Mpungwe
















Uongozi wa klabu ya Yanga chini ya mwenyekiti wake Yusuf Manji leo umewatambulisha rasmi wajumbe wa Bodi ya Baraza la Wadhamiini ambao watafanya kazi zote ambazo zitahusiana na klabu ya Yanga (Mali na Ufilisi) kufuatiwa kupitishwa na wanachama katika mkutano mkuu.

Yanga ilifanya mkutano mkuu mwezi Januari 20, 2013 mkutano uliofanyika katika ukumbi wa bwalo la Polisi Oysterbay ambao wanachama wa klabu walilridhia kuwaongezea tena mda Mama Karume na Francis Kifukwe amabao awali walikua wamemaliza mda wao wa miaka miwili.

Katika mkutano huo wanachama waliridhia kwa mwenyekiti kuongeza idadi ya wajumbe wa bodi ya wadhamini kutoka wawili waliokuwepo na kufikia wajumbe saba, ambapo kwa sasa klabu itakua na wajumbe wanne na kamati ya utendaji itapata fursa ya kuongeza wengine watau ili kufikia idadi ya wajumbe saba.

Akiongea na waandishi wa habari leo makao makuu ya klabu ya Yanga, Manji amesema uteuzi huo wa bodi ya wadhamini umezingatia wasifu wa wajumbe hao ambao wamewahi kufanya kazi katika sekta mbali mbali ndani na nje ya nchi.

Klabu ya Yanga awali ilikua na wajumbe wawili wa Bodi ya wadhamini ambao ni Mama Fatma Karume na Injinia Francis Kifukwe.
Kwa sasa bodi ya wadhamini itakua na wajumbe wa wanne (4) ambao ni Mama Fatma Karume, Francis Kifukwe, na wajumbe wapya waliotambulishwa leo ni Balozi Ami Mpungwe na Kaptain George Mkuchika.
Akitoa wasifu wa wajumbe hao, Manji alisemaBalozi Amir Mpungwe amekua ni kiongozi wa serikali kwa nyadhifa mbali mbali kwa miaka kadhaa, amekua Balozi wa kwanza Tanzania nchini Afrika Kusini mara baada ya nchi hiyo kupata uhuru na kwa sasa anafanya shughuli zake binafsi.

Kaptain George Mkuchika ni waziri wa nchi ofisi ya waziri utawala bora pia amekua kiongozi wa serikali kwa nyadhifa mbalimbali na hata katika chama chake amekua kiongozi makini kwa muda mrefu.
Aidha kuhusu Mama Fatma Karume na Mzee Kifukwe mwenyekiti amesema wanafahamika kwa kazi zao walizozifnya kwa maendeleo ya klabu ya Yanga hali iliyopelekea mkutano mkuu wa wanachama kuwaongezea muda tena wa miaka miwili.

Mara baada ya kutambulishwa rasmi na kupewa katiba za Yanga mwenyekiti alitumia fursa hiyo kuwazungusha wajumbe kuona majengo na mali za klabu kabla ya kupiga picha ya pamoja. 
Wajumbe wa Bodi ya wadhamini wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa klabu ya Yanga

PAPA FRANCIS ATAWAZWA RASMI LEO MJINI ROMA.

Papa Francis, kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani

Sherehe za kumtawaza kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Francis, zimefanyika katika viunga vya Kanisa la Mtakatifu Petro mjini Roma, ikiwa ni ishara ya kuanza rasmi kwa shughuli zake za Papa.
Mapema, Papa Francis alizunguka katika viunga hivyo akiwa katika gari la wazi, akiteremka kuwabariki
mahujaji waliofika hapo.

Kiongozi huyo wa Kanisa Katoliki, amewataka viongozi na watu wote duniani kuwalinda wanyonge na watu maskini. Watu wapatao laki mbili (200,000) wamehudhuria sherehe hizo.

Papa Francis alichaguliwa na mkutano wa Makadinali wiki iliyopita kuchukua nafasi ya Papa Benedict XVI aliyetangaza kujiuzulu wadhifa huo tarehe 28 Februari 2013
.
Papa Benedict amekuwa papa wa kwanza kujiuzulu katika miaka 600 ya historia ya Kanisa Katoliki. Alitangaza kujiuzulu mwezi uliopita akitaja sababu za umri wake wa miaka 85 na kwamba asingeweza kutekeleza kikamilifu majukumu yake.

Papa huyo wa kwanza kutoka bara la Amerika, anaonekana kuwa na mtazamo tofauti na watangulizi wake.

Zilizosomwa zaidi