Monday, March 18, 2013

WASIOKUWA NA TAALUMA WABAINIKA KUUZA DAWA MUHIMU.

Watu 462 kati ya 1,205 mkoani Mwanza waliokuwa wakisailiwa na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kupitia Baraza la Famasi, wamebainika kuwa na vyeti bandia.
Kubainika huko kulijitokeza wakati wakifanyiwa mafunzo kuhusu uuzaji wa dawa katika maduka muhimu.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Mwanza, Mratibu wa Mpango wa Maduka Muhimu katika Baraza la Wafamasi, Richard Silumbe, alisema Mkoa wa Mwanza, umeongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya watu waliobainika kuwa na vyeti bandia.
Kwa mujibu wa mratibu huyo, tatizo lilibainika wakati wa kutoa mafunzo elekezi kwa wanafanya kazi wa maduka ya dawa baridi, katika mikoa mbalimbali nchini.

“Asilimia 46 ya waliofika katika usaili huo, walikuwa na vyeti bandia kutoka katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando na vingine vikitoka katika Chuo cha Kanisa la AIC Korandoto. Hali hii imetutisha kwa sababu watu hawa wapo madukani na wanawahudumia wananchi,” alisema Kilumbe.

Alisema pamoja na kuwachuja wauguzi hao waliokuwa wameomba kupata mafunzo ya uuzaji wa maduka ya dawa muhimu, bado kuna wengine waliobainika kuwa hawana ujuzi wowote katika fani hiyo.

SIKU YA KUCHAGUA MABARAZA HADI APRIL 5

Tume ya Mabadiliko ya Katiba imeongeza siku mbili za kupiga kura ya kuchagua wajumbe wa Mabaraza ya Katiba ya Wilaya, zoezi ambalo awali lilipangwa mara ya kwanza kufanyika kati ya Machi 30 mpaka Aprili 3, mwaka huu.
Mabadiliko hayo ya ratiba yamekuja baada ya baadhi ya makanisa kutumia ibada ya juzi Jumapili pamoja na mambo mengine kuonya juu ya ratiba hiyo ya Tume kuwanyima haki wafuasi wa dini ya Kikristo kutokana na siku zilizokuwa zimepangwa kuangukia kwenye Sikukuu ya Pasaka.

Katibu wa Tume hiyo, Assaa Ahmad Rashid aliieleza Mwananchi jana kuwa muda umesogezwa mpaka Aprili 5 mwaka huu badala ya Aprili 3 kama ilivyokuwa imetangazwa awali.

“Kwa mujibu wa mabadiliko mapya, vikao hivyo sasa vitafanyika kati ya Machi 30 hadi Aprili 5, kwa msingi huu kila kijiji au mtaa kitachagua tarehe ambayo wananchi watapiga kura kuwachagua wajumbe wa Mabaraza ya Katiba ya Wilaya,” alisema.

ISOME HABARI YA UHURU KUTAKA MASHTAKA YAKE ICC YAFUTWE.

Uhuru Kenyatta mahakamani ICC
Wanasheria wa rais mteule wa Kenya, Uhuru Kenyatta, wameiomba Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai, ICC, kumfutia mashitaka yanayomkabili mbele ya mahakama hiyo.
Bwana Kenyatta amekanusha kuchochea ghasia baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2007.
Kikao maalum cha mahakama hiyo kimefanyika wiki moja baada ya mashitaka dhidi ya mshtakiwa-mwenza, Francis Muthaura, kutupiliwa mbali na mahakama ya ICC.
Mawakili wa Kenyatta wanasema kuachiwa kwa Muthaura, pia kunafuta mashitaka dhidi ya Kenyatta, lakini mwendesha mashitaka wa ICC amesema ana ushahidi zaidi dhidi ya Uhuru Kenyatta.
Kesi dhidi ya Bwana Kenyatta, ambaye alishinda uchaguzi mkuu uliofanyika mapema mwezi huu, na kutangazwa rais mteule baada ya kupata asilimia kidogo juu ya 50%, imepangwa kuanza kusikilizwa mwezi Julai.
Baada ya matokeo ya uchaguzi wa Desemba mwaka 2007 - wakati Bwana Raila Odinga aliposhindwa dhidi ya Rais wa sasa Mwai Kibaki, zaidi ya watu 1,000 waliuawa na wengine 600,000 kuachwa bila makaazi.
Bwana Kenyatta, mtoto wa mwasisi wa taifa la Kenya, Jomo Kenyatta anatuhumiwa kupanga mashambulio dhidi ya makundi ya kikabila yaliyokuwa yakimuunga mkono Bwana Odinga kufuatia uchaguzi wa mwaka 2007.
 
Zaidi ya Wakenya 1,000 waliuawa baada ya uchaguzi wa mwaka 2007. Wiki iliyopita, mwendesha mashitaka wa ICC, Fatou Bensouda alisema kesi dhidi ya Bwana Muthaura imetupiliwa mbali kufuatia baadhi ya mashahidi kuogopa kutoa ushahidi wao, huku mwingien akikana sehemu ya ushahidi wake na kukiri kupokea rushwa.

Shahidi muhimu - akijulikana kama shahidi namba nne - alikuwepo katika mkutano ambako BwanaMuthaura na Bwana Kenyatta walituhumiwa kupanga kuwatumia kikundi cha Mungiki kinachoogopewa nchini humo kuwashambulia Wakalenjin, ambao walionekana kuwa wafuasi wa Bwana Odinga katika uchaguzi wa mwaka 2007.

Kiongozi wa mawakili wa Bwana Kenyatta, Stephen Kay anesema kwa kuwa shahidi namba nne ndiye aliyemhusisha Kenyatta na kikundi cha Mungiki, kwa hiyo kujitoa kwake katika ushahidi kuna maana kwamba Kenyatta hana kesi ya kujibu.
Uhuru Kenyatta ashinda Urais Kenya

"kwa kiasi fulani tumepoteza imani katika utoaji maamuzi kama tulivyotahadharisha kikao cha kwanza cha mahakama cha kuthibitisha mashitaka, kutokana na aina ya ushahidi uliokuwa ukitolewa , na tukapuuzwa," Bwana Kay tameiambia mahakama ya ICC, ripoti kutoka shirika la AFP
.
"Ushahidi dhidi ya Bwana Muthaura ambao umelazimisha kuondolewa kwa mashitaka dhidi ya Kenyatta ni sawa sawa na Bwana Kenyatta," amesema. Amewaomba majaji kurejesha kesi ya Bwana Kenyatta kwenye mahakama ya kuthibitisha kesi ili majaji waweze kupitia ushahidi uliobakia kabla ya kuanza kesi kusikilizwa na kuamua kama kuna ushahidi kamili unaothibitisha kesi hiyo kusikilizwa.

Mwandishi wa BBC Anna Holligan kutoka The Hague anasema baada ya kufutwa kwa kesi dhidi ya mtuhumiwa mwenzake, Francis Muthaura, kumekuwa na uvumi kwamba mashitaka dhidi ya Bwana Kenyatta huenda pia ikatupiliwa mbali.
Chanzo BBC.

HIZI NDIO STORI KUBWA KWENYE MAGAZETI YA LEO JUMANNE 19.


..
..
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
 
 
 
.
.
.
.
.
.
. 


Zilizosomwa zaidi