Friday, March 15, 2013

IKO HAPA RATIBA YA LEO TAR 16 MARCH KATIKA BARCLAYS PRIMIER LEAGUE.


Everton
v/s.
Manchester City
-3:45 PM



Stoke City
v./s
West Bromwich Albion
-6:00 PM



Swansea City
v./s
Arsenal
-6:00 PM



Southampton
v./s
Liverpool
-6:00 PM



Aston Villa
v./s
Queens Park Rangers
-6:00 PM

MTOTO MIAKA 7 ANUSURIKA KUUZWA....!

7 Year Old Escapes Deathly RitualMtoto mwenye umri wa miaka saba mwenye ulemavu wa ngozi (albinism)
nchini Kenya amefanikiwa kumtoroka mjomba wake pamoja na ndugu zake waliokuwa wamemteka
ili wamuuze kwa ajili ya kujipatia fedha.

Mtoto huyo aliwatoroka kwakuruka kupitia kwa dirisha la gari alipokuwa anapelekwa  kuuzwa na hivyo kuponea chupuchupu.

LOWASA ATWAA UENYEKITI WA KAMATI ZA BUNGE

Ofisi ya Bunge imetangaza majina ya wenyeviti na makamu wapya wa Kamati za Kudumu za Bunge huku Mbunge wa Jimbo la Monduli, Edward Lowassa akichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
 
Kuchaguliwa kwa Lowassa kuongoza kamati hiyo kunaibua upya vita kati yake na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, kutokana na wote kutajwa kutaka kugombea urais katika uchaguzi mkuu ujao mwaka 2015.
Awali, Lowassa alikuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, ambayo iligawanywa hivi karibuni na kuzaliwa kamati mbili; ya Ulinzi na Usalama na Kamati ya Mambo ya Nje.
Katika uchaguzi huo, Musa Azzan Zungu ambaye alikuwa makamu wa Lowassa kabla ya kugawanya kwa kamati hiyo, amechaguliwa tena kushika nafasi hiyo.
Uchaguzi wa wenyeviti na makamu wao ulifanyika jana katika Ofisi Ndogo za Bunge jijini Dar es Salaam, ikiwa ni siku moja baada ya ofisi ya Bunge kutaja majina ya kamati mpya 16 pamoja na wajumbe wake.
Kamati nyingine iliyofutwa ni ile ya Sheria Ndogo wakati zimeundwa kamati mpya za Bajeti, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na ya Ulinzi na Usalama.
Taarifa za ndani kutoka katika chaguzi hizo zinaeleza kuwa Zitto ambaye alikuwa akichuana na John Cheyo, alipata kura 13 kati ya 17 zilizopigwa na wajumbe wa kamati yake, hivyo Zitto sasa ndiye Mwenyekiti wa Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC)
.
Uchaguzi huo umefanyika ukiwa umepita mwezi mmoja tangu kumalizika kwa mkutano wa 10 wa Bunge ambapo, Spika wa Bunge, Anne Makinda alitangaza mabadiliko ya kamati hizo, huku akiifuta Kamati ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC) iliyokuwa ikiongozwa na Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe.
Kutokana na mabadiliko hayo, shughuli za POAC sasa zitafanywa na Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC).

SURUHISHO IMEPATIKANA MGOGORO GEITA

Baadhi ya viongozi wa Dini ya Kiislam na Kikristo kutoka Geita wamekaa pamoja na kuondoa tofauti zao hususan katika suala la uchinjaji wa nyama kwa ajili ya kitoweo, miongoni mwa makubaliano waliyofikia ni nyama yoyote inayochinjwa kwa ajili ya biashara wachinje waislamu lakini kwenye sherehe zinazowahusu waislam wachinje waislamu na sherehe zinazowahusu wakristo wachinje wakristo wenyewe. Hivyo sherehe zozote za kidini wasiingiliane kwenye taratibu za kidini kwa kila mmoja. 

Mhamasishaji katika mapatano hayo alikuwa ni Mkurugenzi mtendaji wa magazeti ya Global publisher bwana Erick Shigongo pamoja na Mhariri wa gazeti la Championi, katika mapatano hayo wakristo na waislamu walikumbatiana kuonesha wamemaliza tofauti zao na kisha kwa pamoja wakaungana na kwenda kwenye mechi ya fainali kati ya Buseresere na Katoro, ambapo Katoro walitwaa kombe.

Kabla ya kukabidhi kombe, masheikh na wachungaji walizungumza na kusisitiza sana suala la amani pia wakazungumzia mapatano yao baada ya kikao na mashabiki waliokuwa uwanjani hapo wakashangilia.

Mmoja wa viongozi wa serikali aliyehudhuria ni mbunge, Gaudencia Bukwimba CCM

Ikumbukwe hivi karibuni kulikuwa na machafuko huko Geita na kusababisha kifo cha mchungaji wa PAGT Mathayo Kachira. ambapo Waziri Stephen Wasira na Waziri mkuu Mizengo Pinda walijaribu kusuluhisha mgogoro huo bila ya mafanikio





KITALE AENDELEA KUSHIKILIWA NA POLISI

Hali ya afya ya Mkuu wa Usalama na Ulinzi wa Chadema, Wilfred Lwakatare anayeshikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kuwahamasisha watu kufanya vitendo vya uvunjifu wa amani kupitia mitandao ya jamii, imezorota.
Wakili wake Nyaronyo Kicheere, amelalamikia hali yake kuwa si njema kutokana na ugonjwa wa kisukari alionao.
Alikuwa akitembea kwa kujivuta, na alidai kuwa ameshindwa kula chakula inavyotakiwa.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi, wakili Kicheere alisema amehangaika sana katika kuhakikisha kuwa mteja wake anapata dhamana lakini imeshindikana, hali ambayo inamtia hofu kutokana na hali aliyomwona nayo.
“Mteja wangu ni mgonjwa wa kisukari, kwa kawaida hutakiwa kula chakula na kunywa maji mengi, lakini nimehangaika sana, leo (jana) nilikuwa na matumaini kwamba atapelekwa mahakamani ambapo nilijipanga kwa kuandaa watu makini wenye hati za nyumba nikiwa na imani kwamba angepata dhamana, lakini wamemrudisha mahabusu,” alisema Kicheere.
Kicheere muda mwingi alionekana kuhaha kuwasiliana na viongozi wa Chadema kwa simu yake ya mkononi, pamoja na kuwasiliana na baadhi ya wanasheria akiwamo Tundu Lissu na Peter Kibatala ambao walijipanga katika kuhakikisha kuwa wanapata wadhamini watakaoweza kumdhamini Lwakatare.
Wakili huyo alisema kuwa kinachotendeka kwa mteja wake ni kinyume cha sheria kwa kuwa ni tuhuma ndizo zimemfanya akamatwe.
Alisema mteja wake ana haki ya kupewa dhamana hasa kwa kuzingatia kuwa saa zaidi ya 24 zimepita na hali yake si njema, na kwamba kuendelea kuwa mahabusu ni kuhatarisha usalama wa afya yake.
Maofisa wa juu kutoka ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelelezi wa Makosa ya Jinai, waliwasili Kituo Kikuu cha Polisi jijini Dar es Salaam ambapo walikutana na wakili Kicheere na mtuhumiwa huyo na kufanya mazungumzo.
Taarifa za kuaminika zilizopatikana awali zilieleza kuwa juzi saa 11 jioni maofisa kadhaa wa polisi, walimchukua mtuhumiwa huyo na kwenda naye nyumbani kwake wakiwa na lengo la kufanya upekuzi kwa mara ya pili lakini juhudi zao ziligonga mwamba baada ya kutokuwa na kibali cha upekuzi.
“Wakili wake anawabana maofisa wa polisi akitaka wafanye kazi zao kwa mujibu wa sheria hivyo juzi hawakuweza kuingia ndani, pia walizuiwa na wakili huyo huyo kumhoji kwa kumrekodi kwa video, ambapo kulitokea hali ya majibishano ya kisheria, lakini hatimaye akahojiwa bila kurekodiwa,” kilieleza chanzo cha habari.
Lwakatare alikamatwa Jumatano ya wiki hii katika makao makuu ya chama hicho na tangu siku hiyo anaendelea kushikiliwa na polisi kwa mahojiano.
Chanzo Mwananchi gazeti.

KIBONZO CHA LEO.

 
(Kutoka kwa Nathani)

ISOME HAPA RATIBA YA KESHO TAR 15 MARCH KATIKA BARCLAYS PRIMIER LEAGUE.


Everton
v/s.
Manchester City
-3:45 PM



Stoke City
v./s
West Bromwich Albion
-6:00 PM



Swansea City
v./s
Arsenal
-6:00 PM



Southampton
v./s
Liverpool
-6:00 PM



Aston Villa
v./s
Queens Park Rangers
-6:00 PM

ZIMBABWE KUPIGA KURA YA KATIBA MPYA LEO.


wapiga kura katika foleni

Zimbabwe inapigia kura ya maoni kielelezo cha katiba 
hii leo, ikiwa ni mara ya kwanza tangu uchaguzi ufanyike 
nchini humo uliokumbwa na utata mwaka wa 2008.
Hata hivyo malalamiko yametolewa kuwa huenda nchi hio 
haijajiandaa vilivyo kutokana na ukosefu wa fedha za 
kutosha na wachunguzi wanadai kuwa wamefungiwa nje
ya shughuli hiyo.
Mugabe na Tsvangirai

Lakini kwa mara ya kwanza inaonekana kuwa hakuna
 Utata uliojitokeza katika kura hii. Chama chake rais 
Robert Mugabe ZANU - PF na kile cha upinzani 
ambacho sasa kiko katika serikali ya muungano MDC, 
vyote vinaunga mkono kielelezo hicho cha katiba.
Katiba hiyo inapendekeza kuhifadhiwa nafasi ya rais 
mwenye nguvu nyingi serikalini na hii inampa rais Mugabe 
uwezo wa kusalia madarakani kwa miaka kumi zaidi.

Hata hivyo kura hii ya maoni haijawachangamsha sana 
wananchi wa Zimbabwe huku raia wengi wakionekana 
kulenga zaidi uchagzui mkuu unaopangwa kufayika miezi chache zijazo.
Katiba mpya inatazamiwa kunyoosha njia ya 
kufanyika uchaguzi huo mkuu japo kuna wasiwasi 
kwa machafuko zaidi kutokea nchini humo.

STORI ZOTE KUBWA KWENYE MAGAZETI YA LEO IJUMAA 15 MARCH ZIKO HAPA..

.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.

KAULI YA MEMBE BAADA YA KUHUSISHWA NA TUHUMA YA UKATILI ALIOFANYIWA KIBANDA.


.
.Hii ndio kauli iliyotolewa na Waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa Bernard Membe kuhusu kilichoandikwa na gazeti la Mtanzania march 13 2013 toleo namba 7255.
“SAKATA LA KUTESWA KWA KIBANDA: Membe atajwa” na kwamba eti mimi ninahusika na vitendo vya kikatili na unyama alivyofanyiwa Mhariri Mtendaji Mkuu wa kampuni ya New Habari, Bw. Absalom Kibanda”

“Nimeshangazwa na kusikitishwa sana na habari hizo na ningependa kuwahakikishia Watanzania wenzangu kwamba sijahusika, sihusiki na sina sababu ya kuhusika kwa namna yoyote ile. Sina nia, genge wala fedha za kufanya shughuli kama hiyo. Katika maisha yangu yote, sijawahi kugombana naye na hajawahi kunifanyia ubaya wowote. Kwa kifupi, sina uhasama na Bw. Absalom KIbanda”

“Taarifa iliyotolewa na Mtanzania ni taarifa ya uongo, ni habari za kuunga-unga maneno na habari za kughshi. kwa vyovyote vile, mwandishi wa habari hii na wenzake wana malengo ya kisiasa anayoyajua yeye na wenzake wanaomtumia. Huu ni mwendelezo wa mkakati wa kisiasa wa kunichafua ambao umekuwa ukiendelezwa na wale wasionitakia mwema. Wanajaribu kuwaondoa Watanzania katika kiu yao ya kutaka kufahamu ukweli wa jambo hili”

“Nawashukuru sana wananchi wenzangu, jamaa na marafiki walioniletea salamu za kunitia moyo. Naungana nao katika kujiuliza, hivi kiburi hiki, dhihaha hii na ujsriri huu wa kusema uongo hadharani wanautoa wapi!? Jeuri na kiburi cha nmana hii hakiwezi kutokana na sheria za nchi, haki ya kikatiba wala hofu ya Mwenyezi Mungu. Naomba Watanzania wenzangu mnisaidie kutegua kitendawili hiki. Naamini kwa dhati kwamba ukweli kuhusu suala hili utajulikana na yeyote mwenye ushahidi wa kweli aonyeshe uzalendo wake kwa kutoa taarifa kwenye vyombo vya ulinzi na usalama”

“Mwisho, wakati nashauriana na wanasheria wangu kuona hatua ya kuchukua dhidi ya kuchafuliwa huku, nawaomba Watanzania wenzangu tuvute subira na tuache vyombo vya ulinzi na usalama vifanye kazi zake ili Watanzania hatimaye wajue ukweli wa kilichotokea”

Zilizosomwa zaidi