Monday, January 21, 2013

MATOKEO YA AFCON, ZAMBIA V/S ETHIOPIA, NIGERIA V/S BURKINA FASO NDIO HAYA



Zambia1 - 1Ethiopia

Nigeria1 - 1Burkina Faso

MPAKA SASA DIWANI ALIYEFUMANIWA HUKO IRINGA, AGOMA KWENDA HOSPITALI KUTIBIWA

Kama ni kituko cha mwaka basi hiki  pia ni kituko cha aina yake pamoja na diwani wa kata ya Ifunda  jimbo la Kalenga  wilaya ya Iringa mkoani Iringa  Mheshimiwa Elia Mgwila  kufumaniwa na kukatwa  sikio moja na kung'olewa meno ila bado  diwani huyo ambae ni majeruhi ameendelea  kugoma katukatu kwenda  Hospital kutibiwa majeraha hayo.

Mbali ya  kuwagomea  ndugu na marafiki hao bado diwani huyo amegoma kwenda  kituo cha  polisi kufungua shitaka hilo na kudai kuwa  yote anamwachia mwenyezi Mungu  muumba wa mbingu na nchi na vyote vilivyopo duniani .

Wakati  diwani  huyo akigoma  kufika Hospital kutibiwa taarifa  zinadai  kuwa jeshi la  polisi  ambalo lilikuwa  likimshikilia bwana mwenye mke  aliyefumaniwa na diwani huyo mkazi  wa kijiji cha Ifunda kibaoni pamoja na mdogo  wake na mkewe  wameachiwa  huru na jeshi la polisi ambalo lilikuwa  likiwashikilia kwa  tukio hilo la kumjeruhi  diwani .

Huku  habari  za kipolisi  zikidai kuwa  watuhumiwa hao  wameachiwa  huru  kutokana na diwani huyo kugoma  kufungua kesi juu ya shambulio  hilo  la mwili.
Diwani  Elia Mgwila aliyesimama
Mpiga  kura  akigonga mlango  wa diwani  bila mafanikio

Nyumba  ya aliyofumaniwa  diwani  huyo na mke wa mtu  hii hapa
Hapa ni nyumbani kwa  mheshimiwa mlango ukiwa umefungwa  huku ufunguo ukiwa nje
Mwananchi akitoka kumwona diwani huyo  bila mafanikio  leo


GARI LA SERIKALI LANASWA LIKIWA NA PEMBE ZA NDOVU ARUSHA

 
GARI aina ya Toyota VX linaloelezwa kuwa mali ya Serikali limekamatwa na polisi likiwa limebeba pembe za ndovu.
Gari hilo lilikamatwa juzi saa 3:00 usiku katika Kijiji cha Kigongoni katika Mji wa Mto wa Mbu, wilayani Manyara baada ya gari hilo kupinduka.
Vyanzo vya uhakika kutoka ndani ya Jeshi na Polisi zimeeleza kuwa askari wa jeshi hilo aliyekuwa akiendesha gari hilo anashikiliwa na polisi.
Uchunguzi umebainisha kuwa ndani ya gari hilo kulikuwa na meno ya tembo na watu wengine watatu ambao walikimbilia porini na baadhi ya nyara hizo.
Habari hizo zimedai bado kuna utata kuhusu gari lililokuwa likitumiwa na maofisa hao kwa kuwa kibao cha namba za gari hilo kinasomeka kwa namba za kiraia lakini vioo vimechorwa namba za Serikali, huku Mkurugenzi Mkuu wa Tanapa akisema pia kulikuwa na namba za JWTZ.
Kulingana na taarifa kutoka ndani ya Jeshi la Polisi, kukamatwa kwa gari hilo kulitokana na Askari wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (Tanapa), Hifadhi ya Ziwa Manyara kudokezwa na raia wema.
Inaelezwa kuwa baada ya askari hao kudokezwa, walianza kufuatilia nyendo za maofisa hao ndani ya hifadhi na walipogundua wanafuatiliwa, gari hilo liliongeza mwendo kuelekea Mji wa Mto wa Mbu.
Hata hivyo, kutokana na mwendokasi wa gari hilo na kutokuwa wazoefu kulinganisha na Askari wa Tanapa, gari la maofisa hao lilipinduka lilipofika Kijiji cha Kigongoni nje kidogo ya Mto wa Mbu.
“Baada ya kupekuliwa lilikutwa na pembe mbili za ndovu na uchunguzi wa awali umethibitisha maofisa waliokimbia walifanikiwa kutoroka na pembe nyingine tatu,” kilidokeza chanzo hicho.
Kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo kulitokana na wananchi kumtilia shaka yeye na wenzake gari lao lilipopata ajali kwa kitendo cha watu wawili waliokuwepo kwenye gari hilo kuonekana wakihamisha mizigo  na kukimbilia porini.
“Matairi mawili ya gari yalipasuka lakini ajabu ni kwamba wananchi walipojitokeza kusaidia majeruhi, wawili kati yao walinyanyua mizigo isiyojulikana na kukimbilia porini huku wakimwacha mwenzao aliyevaa sare za jeshi akisubiri garini,” alisema mtoa taarifa wetu.
Kwa mujibu wa mashuhuda, wakati wa ajali hiyo, mtuhumiwa alikuwa amevaa jaketi la JWTZ pamoja na suruali ya jinsi akiwa na bunduki aina ya Rifle.
Katika msako uliofanywa na polisi kwa kushirikiana na wananchi, pembe mbili zaidi  za ndovu zilikutwa zikiwa zimefichwa karibu na eneo la ajali.
Mkurugenzi mkuu wa Tanapa, Allan Kijazi alithibitisha kutokea kwa tukio hilo lakini akasema hana taarifa kamili kwani yuko Tanga na wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira.
“Ni kweli nimearifiwa juujuu tu, nasubiri taarifa kamili lakini nimeambiwa tu hilo gari lilipinduka wakati wakifukuzana na askari wetu, lakini mnaweza mkapata taarifa zaidi polisi,” alisema Kijazi.
Msemaji wa JWTZ, Kanali Kapambala Mgawe alisema hajapata taarifa hiyo, hivyo asingeweza kutolea maoni kwa namna yeyote.

Chanzo: Mwananchi

AIBU KUBWA STENDI KUU YA MABASI UBUNGO BAADA YA UKUTA KUBOMOKA

 Magari mbalimbali yakiwa chini ya kifusi.
 Gari aina ya Noah likiwa limegandamizwa na zege.
 Hii ndiyo hali halisi ya tukio lilivyokuwa.
 Gari aina ya Toyota likiwa limebonyezwa na zege.
 Watu wakiangalia magari yao.
 Kenyela akiongea jambo juu ya ajali hiyo.
 likuwa ni hasara tupu.
 Hali ilikuwa ni mbaya katika zahama hiyo ya alfajiri ya leo.
 

Zilizosomwa zaidi