Sunday, January 20, 2013

MVUA KALI YASABABISHA MAFURIKO MJINI MTWARA

Mvua kubwa iliyonyesha mapema leo mjini Mtwara imepelekea mafuriko katika maeneo mbali mbali ya mji huu na kufanya wakazi wa maeneo haya kupata kuanza kuhangaika kuhamisha vitu vyao na wengine wakiwa hawajui la kufanya maana maji yamejaa mpakamajumbani mwao.

Ni balaa kubwa hasa eneo la Chuno Eneo hili ni karibu na nyumba ya Mzee Hokororo au Dr Mwakipa. Hali ni mbaya sana na maji yanaendelea kujaa hadi mchana huu.Hakuna taarifa yeyote mtu yeyote aliyepoteza maisha. Msaada wa haraka unahitajika kwa wananchi hawa.
 Picha na Mdau Abdulaziz

HAWA NI VIONGOZI ZANZIBAR WALIOSHIRIKI KUTOA MAONI YA KATIBA MPYA.

  • Januari 20, 2013: Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Dkt. Khalid Mohamed akiongea katika mkutano na Wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba uliofanyika katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam leo. Katibu Mkuu huyo aliwasilisha maoni ya watumishi wa ofisi yake kuhusu Katiba Mpya. 
    Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar
     Dkt. Khalid Mohamed akiongea katika mkutano na Wajumbe wa
     Tume ya Mabadiliko ya Katiba uliofanyika katika ukumbi wa 
    Karimjee jijini Dar es Salaam leo. Katibu Mkuu huyo aliwasilisha
     maoni ya watumishi wa ofisi yake kuhusu Katiba Mpya.
     
    Januari 20, 2013: Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Bw. Awadh Said akiongea katika mkutano kati ya Wajumbe wa Tume na ujumbe wa Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar uliowasilisha maoni ya watumishi wa ofisi hiyo kuhusu Katiba Mpya katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam leo. 
     
    Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Bw. Awadh Said 
    akiongea katika mkutano kati ya Wajumbe wa Tume na ujumbe wa
     Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar uliowasilisha maoni ya 
    watumishi wa ofisi hiyo kuhusu Katiba Mpya katika ukumbi wa
    Karimjee jijini Dar es Salaam leo.
    Januari 20, 2013: Katibu Mkuu Mstaafu Bw. Vincent Mrisho akitoa maoni yake kuhusu Katiba Mpya katika mkutano kati yake na Wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba katika ofisi za Tume leo. Kulia ni Mwenyekiti wa Tume Jaji Jospeh Warioba.
    Katibu Mkuu Mstaafu Bw. Vincent Mrisho akitoa maoni yake 
     kuhusu Katiba Mpya katika mkutano kati yake na Wajumbe wa 
    Tume ya Mabadiliko ya Katiba katika ofisi za Tume leo. Kulia ni 
    Mwenyekiti wa Tume Jaji Jospeh Warioba.

MCHAKATO WA KATIBA NDIO UMEFIKA PATAMU,,,,,SOMA HII

(Jaji Mstaafu, Joseph Warioba ambaye ni Mwenyekiti wa
 Tume ya Mabadiliko ya Katiba akizungumza na Mwenyekiti 
wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji Mstaafu Damiani Lubuva 
(kulia) jijini, Dar es Salaam jana. Picha na Juliana Malondo  mwananchi) 

MWENYEKITI wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec), Jaji Mstaafu Damian Lubuva ametoa maoni mbele ya Tume ya Katiba akipendekeza kuwa Katiba Mpya iunde Tume Huru ya Uchaguzi na kwamba itambulike kwa jina la Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi.
Jaji Lubuva aliyekuwa akitoa maoni hayo kwa niaba ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi, alisema kuwa tume huru ni inayokubalika na wadau wote wa uchaguzi na wananchi kwa jumla, ambayo katika utekelezaji wa majukumu yake, itafanya kazi zake bila kuingiliwa.
“Uhuru wa tume utaanzia tangu kwenye jina la tume yenyewe…; Kubadilishwa kwa jina na kuweka neno ‘Huru’ kunaweza kubadili fikra za wadau juu ya Tume ya Uchaguzi,”alisema Lubuva.
Lubuva alifafanua kuwa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, inapaswa kuanzishwa chini ya sheria mama ya nchi ambayo ni Katiba, kama ilivyo kwa nchi nyingine za Afrika.
Alizitaja baadhi ya nchi hizo zilizo na tume huru za uchaguzi kuwa ni pamoja na Afrika Kusini, Kenya, Ghana, Zimbabwe na Botswana.
Alipendekeza pia uteuzi wa wajumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi ufanywe na wadau mbalimbali na kuteuliwa na rais kabla ya kuthibitishwa na Bunge. “Na kwa kuboresha mazingira ya upatikanaji wa wajumbe wa tume hiyo na viongzi wengine tumependekeza pia Katiba Mpya itamke kwamba wadau mbalimbali watashiriki kupendekeza majina, ambayo mwisho wake Rais atashiriki kuteua majina, lakini siyo rais ateue moja kwa moja,” alisema Jaji Lubuva.
Mbali na hayo, Jaji Lubuva pia alipendekeza Katiba Mpya itambue Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, lakini akataka isiunganishwe na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi katika utendaji wake wa kazi.
“Pia tunapendekeza Katiba iipe Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi mamlaka ya kugawa kata katika maeneo ya uchaguzi wa madiwani,” alisema.
Alisema kuwa mamlaka hiyo hivi sasa iko chini ya Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, (Tamisemi), jambo alilosema lina athari kipindi cha uchaguzi, kwa kuwa huathiri uchaguzi wa madiwani, ambao hufanywa na Tume.
Ofisi ya Msajili wa Vyama
Akizungumzia utendaji kazi wa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa pamoja na NEC, Mwenyekiti huyo wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi alisema: “Tumependekeza kwamba Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa itambulike kikatiba. Tumetaka pia kazi za ofisi hiyo zifanyike kwa kujitegemea na zisichanganywe na NEC.”
Tangu mwaka 1995 ulipofanyika Uchaguzi Mkuu wa kwanza chini ya mfumo wa vyama vingi uliorejeshwa mwaka 1992, NEC imekuwa ikilaumiwa kuwa siyo huru na kwamba inaegemea chama tawala.

SAKATA LA KUPINGA GESI KUTOKA MTWARA NDIO HII

SAKATA la kupinga ujenzi wa bomba la gesi inayovunwa katika Kijiji cha Msimbati mkoani Mtwara kwenda Dar es Salaam, limechukua sura mpya baada ya maelfu ya wakazi wa Mkoa wa Mtwara kujiandikisha katika fomu maalumu kupinga mradi huo.
Tayari majina hayo yamekabidhiwa kwa Katibu wa Wabunge wa Chama cha Wananchi (CUF), Magdalena Sakaya kwa ajili ya kuyawasilisha bungeni kama kielelezo halali cha wananchi hao kupinga mradi huo, ambapo utaratibu wa wananchi hao kujiorodhesha uliandaliwa na chama hicho.
Taarifa zinaeleza kuwa zaidi ya wakazi 30,000 wa Mtwara wamejiorodhesha kupinga mradi huo wa gesi.
Makabidhiano hayo yamefanyika kwenye mkutano mkubwa wa hadhara uliofanyika katika Viwanja vya Mashujaa mjini Mtwara na kuhudhuriwa na maelfu ya wananchi kutoka wilaya zote tano ya mkoa huo, ambao hawakujali mvua kubwa iliyokuwa ikinyesha.
Watu wa kada mbalimbali waliliambia Mwananchi Jumapili kwamba haijawahi kutokea umati mkubwa wa watu kuhudhuria mkutano wa hadhara mkoani humo kama ilivyokuwa kwa mkutano wa jana.
Walisema kuwa idadi hiyo ya watu ni zaidi ya waliojitokeza katika maandamano ya kupinga mradi huo, yaliyofanyika Desemba 27 mwaka jana.
Majina hayo yalikabidhiwa na makatibu wa CUF wa wilaya za mkoani huo  huku mwakilishi wao Saidi Kulaga, akisema kuwa zaidi ya watu 30,000 wamejiandikisha kupinga mradi huo.
Alisema wananchi hao wanataka Serikali kujenga mitambo ya kufua umeme  mkoani humo, ili kuinua uchumi wa mikoa ya kusini.
“Kwa niaba ya wananchi hawa na mbele yao,  nakukabidhi majina na  sahihi zao, wakipinga mradi wa kusafirisha gesi kwenda Dar es Salaam. Wazee wetu waliwaondoa wanyonyaji weupe, sasa ni zamu ya vijana kuwaondoa wanyonyaji weusi,”  alisema Kulaga huku akishangiliwa na umati wa watu.
Akipokea fomu hizo, Sakaya alisema kuwa wabunge wa CUF, wamesikia kilio cha wananchi wa Mtwara na kwamba watahakikisha wanawasilisha katika Bunge lijalo.
Katika mkutano huo mabango kadhaa yalibebwa na baadhi yakisomeka: “Shemejiii gesi haitoki…: Kikwete tuachie gesi yetu.”
Kabla ya mkutano kuanza umeme ulikatika eneo hilo hali  iliyosababisha kundi la vijana kuivamia Ofisi ya Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), mkoani humo wakiishinikiza urudishwe, kitendo kilichowalazimu polisi kuingilia kati na kufyatua mabomu ya machozi ili kuwatawanya wananchi hao.
Wananchi waliondoka eneo la ofisi hizo na kurudi uwanja wa mkutano, ambapo baadaye na mkutano huo uliendelea kwa  amani na utulivu, huku polisi wakiwa katika tahadhari kubwa.

HII NDIO RATIBA YA CAF 2013

Ratiba ya CAF 2013 ndio hii hapa na baadhi ya timu zimekipiga jana ambapo Afrika Kusini v/s Cape Verde na Angola v/sMorocco zote zilitoka sare ya bila kufungana

Group A:

1.Angola | P: 1 | Pointi: 1

2. Cape Verde | P: 1 | Pointi:1

3. Morocco | P: 1 | Pointi: 1

4. South Africa| P: 1 | Pointi: 1

23/01/13:
  • Afrika Kusini dhidi ya Angola (Saa Kumi na mbili Jioni)
  • Morocco dhidi ya Cape Verde (Saa Tatu za Usiku)
27/01/13:
Afrika Kusini dhidi ya Morocco (Saa Mbili za Usiku)
Cape Verde dhidi ya Angola (Saa Mbili za Usiku)

Group B

1. Ghana | P: 0 | Pointi: 0
2. Mali | P: 0 | Pointi: 0
3. Niger | P: 0 | Pointi: 0
4. DR Congo | P: 0 | Ponti: 0
_________________________________________________________
20/01/13:
  • Ghana dhidi ya DR Congo (Saa Kumi na Mbili za Jioni)
  • Mali dhidi ya Niger (Saa Tatu za Usiku)
24/01/13:
  • Ghana dhidi ya Mali (Saa Kumi na Mbili za Jioni)
  • Niger dhidi ya DR Congo (Saa Tatu za Usiku)
28/01/13:
Ghana dhidi ya Niger (Saa Mbili za Usiku)
DR Congo dhidi ya Mali (Saa Mbili za Usiku)

Group C

1. Zambia | P: 0 | Pointi: 0
2. Nigeria | P: 0 | Pointi: 0
3. Ethiopia | P: 0 | Pointi: 0
4. Burkina Faso | P: 0 | Pointi: 0
_________________________________________________________
21/01/13:
Zambia v Ethiopia (Saa Kumi na Mbili Jioni)
Nigeria v Burkina Faso (1 (Saa Tatu za Usiku)
25/01/13:
  • Zambia dhidi ya Nigeria (Saa Kumi na Mbili za Usiku)
  • Burkina Faso dhidi ya Ethiopia (Saa tatu za Usiku)
29/01/13:
  • Zambia dhidi ya Burkina Faso (Saa Mbili za Usiku)
  • Ethiopia dhidi ya Nigeria (Saa Mbili za Usiku)

Group D

1. Ivory Coast | P: 0 | Pointi: 0
2. Algeria | P: 0 | Pointi: 0
3. Tunisia | P: 0 | Pointi: 0
4. Togo | P: 0 | Pointi: 0
_________________________________________________________
22/01/13:
  • Ivory Coast dhidi ya Togo (1500) ()
  • Tunisia dhidi ya Algeria (1800) ()
26/01/13:
  • Ivory Coast dhidi ya Tunisia (1500) ()
  • Algeria dhidi ya Togo (1800) ()
30/01/13:
  • Ivory Coast dhidi ya Algeria (Saa Mbili za Usiku)
  • Togo dhidi ya Tunisia (Saa Mbili za Usiku)

Robo fainali

02/02/13:
  • Mshindi wa kundi B kupambana na timu ya pili kundi A (Saa Kumi na Mbili za Usiku)
  • Mshindi wa kundi A kumbana na timu ya pili kundi B (Saa tatu na nusu za Usiku)
03/02/13:
Mshindi wa kundi D dhidi ya timu ya pili kundi C (Saa Kumi na mbili jioni)
Mshindi wa kundi C dhidi ya timu ya pili kundi D ( (Saa tatu na nusu za Usiku)

Nusu fainali

06/02/13:
Mshindi wa robo fainali ya pili dhidi ya mshindi wa robo fainali ya tatu saa (Saa Mbili za Usiku)
Mshindi wa robo fainali ya nne dhidi ya mshindi wa robo fainali ya kwanza (Saa tatu na nusu za Usiku)

Mshindi wa tatu

09/02/13:
Timu itakayoshindwa katika mechi ya nusu fainali (Saa tatu Usiku)

Fainali

10/02/13:
Washindi wa mechi ya nusu fainali (Saa Tatu za Usiku)

Zilizosomwa zaidi