Saturday, January 19, 2013

BAADHI YA PICHA NA MATUKIO KATIKA MAHAFALI YA KIDATO CHA SITA AZANIA SEKONDARI LEO


 
Baadhi ya Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya  
Azania wakiwa wamejipanga kumpokea mgeni rasmi  
katika mahafali ya kidato cha Sita ya shule hiyo 
MstahikiMeya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa 
yaliyofanyika leo jijini Dar.
 
Mgeni rasmi Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala 
 Jerry Silaa akibadilishana mawazo na baadhi ya  
Wanafunzi wa shule ya Sekondari Azania  
ambapo na yeye pia alikuwa ni miongoni 
mwaviongozi waliosoma shule hapo baada ya 
kuwasili kwenye hafla mahafali ya wanafunzi wa 
kidato cha sita.
 
Mstahiki Meya Jerry Silaa akipunga mkono kwa wanafunzi wa 
shule ya sekondari Azania waliojipanga mstari kumlaki kwa furaha 
huku akiwa ameambatana na Mkuu wa Shule hiyo Bw. Bernard Ngoze
 na Makamu Mkuu wa Shule hiyo Bi. Elizabeth Ngoda (kulia).
Mgeni rasmi Mstahiki Meya Jerry Silaa akisaini daftari la 
wageni la Shule ya Sekindari Azania katika sherehe za 
mahafali ya Kidato cha sita shuleni hapo.
Mkuu wa shule ya Sekondari Azania Bw. Bernard Ngoze 
akizungumza na mgeni rasmi Mstahiki Meya Jerry Silaa na 
kumwelezea changamoto mbali mbali zinazoikabili shule hiyo. 
Wa kwanza kulia ni Makamu Mkuu wa Shule hiyo Bi. Elizabeth
 Ngoda na Makamu wa pili shuleni hapo Mwl. Joram Nkya.
 Kutoka kushoto ni Mgeni maalum aliyewahi kusoma shuleni hapo
 Bw.Ali Said Mwema, Mjumbe wa Bodi ya Shule hiyo Bi. Hilda Luhanga
 na Msaidizi wa Meya Jerry Silaa Bw. Anthony William wakimsikiliza mkuu
 wa shule ya sekondari Azania (hayupo pichani) wakati akiongea na Mgeni rasmi.
 Mgeni rasmi Mstahiki Meya Jerry Silaa akiongozwa 
na Makamu Mkuu wa Shule ya Azania Bi. Elizabeth Ngoda
 kutazama baadhi ya picha zinazoonyesha hali ya utunzaji wa 
mazingira tangu awali mpaka sasa ambapo kwa kiasi kikubwa 
shule hiyo imeweza kuboresha na kutoa elimu ya mazingira kwa 
wanafunzi wa shule hiyo. Mstahiki Meya amepongeza juhudi zao na
 kuwataka shule nyingi za jijini zilizochini ya manispaa ya Ilala kuiga mfano 
wa shule ya Azania katika kutunza Mazingira.

Vijana wa Skauti wa shule ya Sekondari Azania wakitoa 
heshima kwa mgeni rasmi Mstahiki Meya Jerry Silaa alipowasili
 eneo maalum palipofanyika sherehe za mahafali ya kidato cha Sita.
Mgeni rasmi Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa 
akisalimiana na kuwapongeza baadhi ya wanafunzi wa kidato cha 
Sita wa Shule ya Sekondari Azania.
 
 
Mstahiki Meya Jerry Silaa akipokea heshima kutoka kwa vijana wa 
skauti wa shule hiyo.
                                                                                                                                                       
 Meza kuu ikiimbia wimbo wa taifa.
 Baadhi ya Wazazi na walezi waliohudhuria hafla ya
 watoto wao.
Vijana wa Skauti wakionyesha manjonjo yao 
mbele ya mgeni rasmi kwenye mahafali hayo.
 Binti Pekee wa kikundi cha Skauti cha 
Azania sekondari aliyeshangaza wengi kwa 
kutembea na kamba huku akijiamini vilivyo 
wakati wa sherehe za mahafali hayo.

TUME YA MABADILIKO YA KATIBA LEO.

Photo: Januari 19, 2013: Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Bw. Ludovick Utouh (kushoto) akiongea na Wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba katika ukumbi wa mikutano wa Tume hiyo jijini Dar es Salaam leo. Bw. Utouh alikutana na Wajumbe wa Tume hiyo kutoa maoni ya taasisi yake kuhusu Katiba Mpya. Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Bw. Ludovick Utouh (kushoto) akiongea na Wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba katika ukumbi wa mikutano wa Tume hiyo jijini Dar es Salaam leo. Bw. Utouh alikutana na Wajumbe wa Tume hiyo kutoa maoni ya taasisi yake kuhusu Katiba Mpya.
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
Photo: Januari 19, 2013: Waziri Mstaafu na Mwanasiaisa Mkongwe nchini, Mzee George Kahama (kushoto) akizungumza katika mkutano na wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba leo katika ofisi za Tume Jijini Dar es Salaam leo na kutoa maoni yake kuhusu Katiba Mpya. Kulia ni Mwenyekiti wa Tume, Jaji Joseph Warioba. 

 Waziri Mstaafu na Mwanasiaisa Mkongwe nchini, 
Mzee George Kahama (kushoto) akizungumza katika mkutano na 
wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba leo katika ofisi za Tume 
Jijini Dar es Salaam leo na kutoa maoni yake kuhusu Katiba Mpya. Kulia ni
 Mwenyekiti wa Tume, Jaji Joseph Warioba.
 
 

MSHITAKIWA WA EPA AJIUA KWA RISASI


MSHITAKIWA Katika kesi ya wizi wa zaidi ya Sh bilioni tano za Benki Kuu ya Tanzania kutoka katika Akaunti ya Madeni ya Nje ya Benki Kuu ya Tanzania (EPA), Jai Somani amejiua kwa kujipiga risasi.
Mshitakiwa huyo anadaiwa kujiua jana asubuhi nyumbani kwake katika mtaa wa Mindu, Upanga katika Manispaa ya Ilala.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa Parang Somani ambaye ni kaka yake, hajui kwanini mdogo wake amejiua lakini hapo awali Jai alikuwa akisumbuliwa na tatizo la msongo wa mawazo.
Jai alikuwa anakabiliwa na kesi hiyo pamoja na kaka yake Ajay Somani ambaye amehukumiwa kifungo cha miaka miwili jela pamoja na kulipa faini ya Sh milioni 400 baada ya kukutwa na hatia katika kesi ya wizi wa Sh bilioni 2.2 kutoka Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kupitia akaunti ya EPA.
Jai, Ajay na washitakiwa wengine wanne wanakabiliwa na kesi hiyo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kesi hiyo bado inaendelea. Parang alisema maandalizi ya maziko yanaendelea nyumbani kwa marehemu katika mtaa wa Mindu.
Akizungumza na Habari leo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Marietha Minangi alithibitisha Jai kujiua na kuwa polisi wanaendelea na upelelezi wa chanzo cha kifo chake kwa kuwa hajacha ujumbe wowote.
Washitakiwa wanakabiliwa na mashitaka matano ya kula njama, kughushi, kuwasilisha hati ya kuhamisha deni iliyoghushiwa, kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na kujipatia ingizo la kiasi hicho cha fedha kutoka BoT.

HUYU NDIO MWANDISHI WA HABARI ANAYETAKA KUGOMBEA UBUNGE

Mwandishi wa habari wa gazeti la Mwanahalisi Saed Kubenea, inasemekana amejapanga kugombea Ubunge Jimbo la Kibaha Mjini kupitia CHADEMA mwaka 2015. kwa hivi sasa Jimbo hilo linaongozwa na Silvestry Koka [CCM].

Hii itakuwa habari njema kwa tasnia ya habari kujiingiza katika masuala ya uongozi wa kisiasa, Kubenea kapata msukumo wa kugombea Ubunge baada ya kushauriana na Dr Slaa na kumuakikishia kuwa anaweza kushinda Ubunge Jimbo la Kibaha Mjini kama akijipanga vizuri na kupata msaada wa CHADEMA.

Kila la Heri Saed Kubenea.

Zilizosomwa zaidi