Wednesday, January 16, 2013

ATOKEO YA Barclays Premier League na English FA Cup ya tar 16 yako hapa


Arsenal1 - 0Swansea City

Manchester United1 - 0West Ham United                                  

HIZI NI KUTOKA FACEBOOK.....


AJARI ILIYOTOKEA HUU JIJINI MBEYA

Gari la kubeba mchanga lenye nambari za usjiri T 777 AYP limepata ajari mchana huu jijini Mbeya na baadhi ya watu wamejeruhiwa akiwemo dreva wa gari hilo. Hizi ndio picha za ajari hiyo 















HILI NDIO TAMKO LA SERIKALI KUHUSU VURUGU ZINAZOTOKEA NCHINI

SERIKALI imesema haitavumilia kwa namna yeyote ile vurugu za kidini, kikanda na ukabila ambazo baadhi yake zilitaka kulitia doa taifa mwaka jana.
Pia imesisitiza kwamba haitawavumilia wanasiasa wanaotumia rasilimali za taifa kujitafutia umaarufu kwa gharama za kuligawa taifa.

Akizungumza na mabalozi kwa nyakati tofauti Ikulu, Dar es Salaam; kwanza katika sherehe ya kuukaribisha Mwaka Mpya iliyofanyika juzi na alipokuwa akiagana na Balozi wa Uingereza nchini, Dianne Corner jana, Rais Jakaya Kikwete alisema vurugu zilizotaka kujitokeza mwaka jana zinatosha.

“Serikali haitavumilia vurugu wala ukabila kwa namna yoyote ile…. Mwaka 2012 vurugu zenye sura ya kidini zilianza kujitokeza ila sasa nasema kwamba hatutazivumilia kwa namna yeyote ile, inatosha,” alisema Rais Kikwete.

Akizungumza katika hafla hiyo, Kiongozi wa Mabalozi ambaye pia ni Balozi wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (DRC), Juma Mpango alisema jumuiya ya mabalozi imefurahishwa na namna ambavyo Serikali imekuwa ikishughulikia vurugu za kidini ambazo zilitaka kujitokeza bila kusababisha madhara kwa wananchi.

“Tumeridhishwa na namna ambavyo Serikali imekuwa inashughulikia mambo yake vizuri. Tunaomba mwendelee kushughulikia amani ya nchi hii maana ndiyo mhimili wa nchi za Maziwa Makuu,” alisema Balozi Mpango.

Kuhusu gesi
Rais Kikwete alizungumzia suala la rasilimali za taifa na kusisitiza kuwa pia hatavumilia kuona wanasiasa wakitumia suala la gesi kujitafutia umaarufu.

Wakati Rais Kikwete akitoa kauli hiyo jana, habari kutoka Mtwara zilidai kuwa Naibu Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene amewekewa magogo barabarani kumzuia asiende kwenye kijiji kinachozalisha gesi hiyo, huku Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea, Regina Chonjo akizomewa.

Hata hivyo, polisi walikiri wananchi kuweka magogo barabarani kwa lengo la kumzuia waziri huyo, lakini ikaeleza kuwa gari lililozuiwa siyo la Simbachawene.

Akizungumza na Balozi Corner, Rais Kikwete alikemea tabia ya baadhi ya viongozi wa kisiasa kutumia suala la rasilimali za taifa, ikiwamo gesi asilia kujitafutia umaarufu wa kisiasa na kuwapotosha wananchi.

“Ni jambo la hatari na lisilo na tija kwa wanasiasa kujaribu kuigawa nchi vipandevipande kwa sababu ya kujitafutia umaarufu kwa kutumia rasilimali za taifa,” alisema Rais Kikwete na kuongeza:

“Unawezaje kuwa na nchi moja na taifa moja wakati kila mmoja anadai rasilimali kutoka kwenye eneo moja ibakie na kunufaisha watu wa eneo hilo tu. Huwezi kuwa na nchi moja na yenye umoja wakati kuna nchi ya gesi asilia kule Mtwara, kuna nchi ya kahawa kule Kilimanjaro, kuna nchi ya chai na ndizi kule Bukoba,” alisema Rais Kikwete na kuongeza:

“Kwa sababu kama gesi asilia inatakiwa kubakia na kunufaisha watu wa Mtwara tu, basi wenye haki zaidi ya kudai jambo hili siyo watu wa Mtwara, bali ni watu wa Msimbati ambako ndiko ilipogunduliwa gesi ambako ni maili 60 kutoka Mtwara, kilomita 200 kutoka Newala.”
 Chanzo: Mwananchi

HAYA NDIO YALIYOFICHIKA NDANI YA CHADEMA

Hali si shwari ndani ya Chademabaada ya Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Vijana (Bavicha) wa chama hicho, Juliana Shonza amesema ameamua kumshtaki Mwenyekiti wake, John Heche kwa kumuita kuwa ni msaliti wa chama na kwamba anatumiwa na CCM na kuamua kumfukuza nafasi yake bila kutoa nafasi ya kusikilizwa.

Pia, amemlipua Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk Willibrod Slaa akidai kuwa amefanya ufisadi ndani ya chama kwa kujikopesha Sh140 milioni ambazo hajazilipa hadi sasa.
Mbali na hilo, amemshukia Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe kwa kudai kuwa anatoa kauli za kukurupuka ambazo zinakiyumbisha chama hicho kikuu cha upinzani nchini.

Shonza alitoa kauli hizo jana wakati akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam juu ya tuhuma zilizotolewa na mwenyekiti wa Bavicha na kuhusu kufukuzwa kwake ndani ya chama akiwa na wenzake Mtela Mwampamba na Habibu Mchange.

“Heche na Mbowe wamenifedhehesha kwa kauli zao na wamenichafua na kunidhalilisha mbele ya umma wa Watanzania, hivyo nitapambana nao kuhakikisha haki yangu inapatikana,” alisema Shonza.

Shonza alisema kwamba yeye bado ni makamu mwenyekiti wa Bavicha na mwanachama halali wa Chadema kwa kuwa hadi anazungumza hakuwa amepewa barua ya kufukuzwa kwa kuwa kikao kilichotoa uamuzi huo ni batili.

Alisema kikao kilichoitwa ni cha kamati tendaji na kufikia maamuzi ya kumfukuza kilikuwa batili kwa kuwa katiba pamoja na mwongozo wa Bavicha ulikiukwa, kitu kinachosababisha aeleze kuwa uamuzi uliotolewa na kikao hicho yalikwishapangwa na viongozi wa kitaifa.

“Nasisitiza kwamba ni ukweli uliowazi kwamba ajenda na maazimio ya kikao hicho yalikwishaamuliwa hata kabla ya kikao hicho, kwa sababu taarifa za kufukuzwa kwetu zilikwishaanza kusikika kwenye mitandao ya kijamii kabla hata ya kamati tendaji batili,”alisema Shonza.

Alisema mkakati wa Heche na vibaraka wake umejikita kutukuza ukanda ndani ya chama waziwazi, akieleza kuwa watu waliofukuzwa ndani ya chama hicho wanatokea Ukanda wa Nyanda za Juu Kusini haswa Mbeya wakati vijana wa Kaskazini wameachwa kwa madai kuwa wametoa ushirikiano.

“Natarajia kuomba ufafanuzi wa kikatiba juu ya shutuma zilizotolewa dhidi yangu na Heche kwa kuwaaminisha Watanzania uongo wake,”alisema Shonza.

Kuhusu Mbowe
Alisema kuwa amesikitishwa na kauli ya kiongozi wake huyo katika baadhi ya vyombo vya habari kwamba, madai aliyoyatoa ni ya kitoto kwani ni kitu cha kushangaza kwa kuwa yeye Juliana hayajui ni madai gani hayo.

Alisema kama madai ambayo Mbowe anadai ni ya kitoto ni ya yeye kuhoji kwa nini chama hakiweki akiba kwenye akaunti kwa ajili ya uchaguzi wa 2015 kama ilivyokubaliwa kwenye baraza kuu basi itakuwa ni ajabu.

Alisema inashangaza kwa mwenyekiti wa chama anafumbia macho hatua ya Dk Slaa kujikopesha pesa ya ruzuku ya Watanzania zaidi ya Sh140 milioni, kwani ni kinyume na utaratibu uliopo.

ANGALIA PICHA ZA KUPOKEA SAFARI ZA PRECISION AIR MKOANI MBEYA


 KIKUNDI CHA NGOMA KIKITUMBUIZA MUDA MCHACHE BAADA YA NDEGE KUWASILI 

 VIONGOZI WA SERIKALI PAMOJA NA WADAU MBALIMBALI WAKISHUHUDIA UJIO WA SAFARI ZA KWANZA ZA PRECISION AIR MKOANI MBEYA KATIKA UWANJA WA KIMATAIFA WA SONGWE.
 KILA MWANDISHI ANAJITAJIDI KUPATA PICHA NZURI YA NDEGE 
WAFANYAKAZI WA PRECISION AIR WAKIWA WAMEPENDEZA MUDA HUU KATIKA UWANJA WA KIMATAIFA WA SONGWE MBEYA
 BURUDANI BADO INAENDELEA HAPA
 VIONGOZI WA SERIKALI PAMOJA NA WADAU MBALIMBALI WAKIWA WANATAZAMA KWA UMAKINI NGOMA YA ASILI IKITUMBUIZA
 HII NI MEZA KUU
 NAO WAKAZI WA SONGWE MKOANI MBEYA WAMEFIKA UWANJA WA NDEGE KUSHUHUDIA JINSI NDEGE YA SHIRIKA LA PRECISION AIR ILIPO TUA ENEO HILO.
 MKUU WA WILAYA WA MBEYA MHESHIMIWA NORMAN SIGALA, AKIONGEA MUDA BAADA YA NDEGE KUWASILI
MKURUGENZI MTENDAJI WA PRECISION AIR NDUGU SHIRIMA AKIONGEA NA WAGENI WAALIKWA PAMOJA NA WANANCHI WALIO JITOKEZA KATIKA KUPOKEA NDEGE HIYO AMBAYO INAANZA SAFARI ZAKE ZA KWANZA MKOANI MBEYA NA KUWASHUKURU  KWA MAPOKEZI HAYO.
 MKURUGENZI WA UCHUKUZI MHESHIMIWA PETER LUPATU , AKIMWAKILISHA WAZIRI WA UCHUKUZI KATIKA UZINDUZI WA SAFARI HIZO MKOANI MBEYA
MSHEHERESHAJI MC CHARLES MWAKIPESILE AKIZUNGUMZA JAMBO WAKATI WA SHEREHE HIZO

MKOANI MBEYA MUDA HUU,

 KIKUNDI CHA NGOMA KIKITUMBUIZA MUDA MCHACHE BAADA YA NDEGE KUWASILI 

 VIONGOZI WA SERIKALI PAMOJA NA WADAU MBALIMBALI WAKISHUHUDIA UJIO WA SAFARI ZA KWANZA ZA PRECISION AIR MKOANI MBEYA KATIKA UWANJA WA KIMATAIFA WA SONGWE.
 KILA MWANDISHI AMEJITAJIDI KUPATA PICHA NZURI YA NDEGE 
WAFANYAKAZI WA PRECISION AIR WAKIWA WAMEPENDEZA MUDA HUU KATIKA UWANJA WA KIMATAIFA WA SONGWE MBEYA
 BURUDANI BADO INAENDELEA HAPA
 VIONGOZI WA SERIKALI PAMOJA NA WADAU MBALIMBALI WAKIWA WANATAZAMA KWA UMAKINI NGOMA YA ASILI IKITUMBUIZA
 HII NI MEZA KUU
 NAO WAKAZI WA SONGWE MKOANI MBEYA WAMEFIKA UWANJA WA NDEGE KUSHUHUDIA JINSI NDEGE YA SHIRIKA LA PRECISION AIR ILIPO TUA ENEO HILO.
 MKUU WA WILAYA WA MBEYA MHESHIMIWA NORMAN SIGALA, AKIONGEA MUDA BAADA YA NDEGE KUWASILI
MKURUGENZI MTENDAJI WA PRECISION AIR NDUGU SHIRIMA AKIONGEA NA WAGENI WAALIKWA PAMOJA NA WANANCHI WALIO JITOKEZA KATIKA KUPOKEA NDEGE HIYO AMBAYO INAANZA SAFARI ZAKE ZA KWANZA MKOANI MBEYA NA KUWASHUKURU  KWA MAPOKEZI HAYO.
 MKURUGENZI WA UCHUKUZI MHESHIMIWA PETER LUPATU , AKIMWAKILISHA WAZIRI WA UCHUKUZI KATIKA UZINDUZI WA SAFARI HIZO MKOANI MBEYA
MSHEHERESHAJI MC CHARLES MWAKIPESILE AKIZUNGUMZA JAMBO WAKATI WA SHEREHE HIZO

HII NDIO STORI KAMILI KUHUSU OKWI KUCHEZEA SOKA TUNISIA

BAADA ya kuhangaika muda mrefu hatimaye mshambuliaji wa mabingwa wa Tanzania Bara, Simba na timu ya taifa ya Uganda, Emmanuel Okwi amejiunga naklabu ya Etoile du Sahel ya Tunisia kwa gharama ya Ddola 300,000 (sawa na Sshs 477 milioni).
Okwi alisaini mkataba huo wa kuichezea timu hiyo kwamuda miaka mitatu na nusu mbele ya Mmwenyekiti wa Simba,Ismail Aden Rage na Rrais wa Etoile, Ridha Charfeddinejana Jumanne mchana Okwi ambaye mwishoni mwa mwaka jana aliongeza mkataba wa kuichezea Simba mpaka mwaka 2014, ameuzwa kwa dola za kimarekani 300,000, na kuweka rekodi ya mauzo yajuu kwa klabu hiyo.Katika mkataba huo Okwi aneweka kibindoni dola100,000 kwa kukubali kusaini mkataba huo pamoja nakulipwa mshahara wa Ddola 15,000 kwa mwezi.
Habari hiyo iliyothibitishwa na OAfisa Habari wa klabu hiyo,Ezekiel Kamwaga zilisema kuwa Simbailiwakilishwa namwenyekiti wa klabu hiyo, Ismail Aden Rage kukamilishazoezi hilo.

Okwi aliyekuwa katika majaribio na timu hiyo uhamishowake ulifanyika harakaa haraka ili kuwahi mwisho wa usajiliwa nchi hiyo.Mchezaji huyo wa Uganda, mara kadhaa amekuwa gumzokatika usajili na katika dirisha dogo, liliwalazimu viongozi waSimba kumfuata Uganda na kumsainisha kwa miaka miwili.

Hatua hiyo ilitokana na uvumi kuwa mchezaji huyo alikuwana mpango wa kujiunga na watani wa jadi wa Simba, Yangana klabu ya Azam FC ambazo zilidaiwa kutoa ofa kubwakwa mchezaji huyo.Katika usajili wa mwanzoni mwa mwaka jana, Okwi alikimbiliakusaka timu nje ya nchi, hata hivyo pamoja na kufanya vizuri,hakuweza kucheza huko na kurejea katika timu yake yaSimba.

Afisa Habari wa klabu ya Simba, Ezekiel Kamwagaalisema kuwa ni kweli kuwa Okwi ameuzwa kwa timu hiyo,hata hivyo hakuwa tayari kuweka bayana masuala mbalimbali ya mkataba wa mchezaji huyo.“Nipo likizo, taarifa hizo ni za kweli, lakini kutokana na haliilivyo, mwenyekiti wa timu, Rage atakuja kuelezea kwa kinasuala la mchezaji huyo na kuhusiana na marlupurlupu menginepamoja na makubaliano hasa mshahara, kwa sasa sinataarifa zaidi ya kuuzwa kwa mchezaji huyo,” alisemaKamwaga. Alisema kuwa anajua kuwa Okwi hakwenda na timu Omankwa ajili ya mazoezi ya maandalizi kwa ajili ya Ligi Kuu yaTanzania Bara na michuano ya kimataifa na vile vile anajuataarifa za kuondoka kwa Rage kwenda huko kukamilishazoezi la mauzo ya mchezaji huyo.

Miaka miwili iliyopita, Simba iliuzwa wachezaji wake wawili,Mbwana Samatta and Mganda Patrick Ochan kwa klabuya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) kwa Ddola 100,000 (Sshs150 milioni ) kila mmoja.Kutokana na kuuzwa kwa Okwi, Simba sasa inabakiwa na
wachezaji wanne wa kigeni, Mzambia Felix Sunzu, KomabilKeita (Mali), Mussa Mudde na kipa Abel Dhaira kutoka Uganda.

Zilizosomwa zaidi