Tuesday, January 15, 2013

ALIYEOA MWANAAFUNZI KUKAMATWA

Mwanaume aliyeoa mwanafunzi kukamatwa: WAZAZI wa mtoto aliyeozwa na mwanaume aliyemuoa mtoto katika Kata ya Mvuha wilaya ya Morogoro na kusababisha ashindwe kuanza masomo ya sekondari, watakamatwa na kufikishwa mahakamani

AJARI MWANZA YAUA SABA NA KUJURUHI 47

WATU saba wamekufa na wengine zaidi ya 47 kujeruhiwa vibaya kwenye ajali iliyohusisha mabasi mawili yaliyogongana uso kwa uso katika barabara kuu ya Mwanza-Musoma, wilayani Bunda mkoani Mara. 
  Akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mara, Absalom Mwakyoma, alisema kuwa tukio hilo lilitokea juzi saa 11:00 jioni, katika Kijiji cha Nyatwali, mpakani mwa Wilaya ya Bunda na mji mdogo wa Lamadi, Wilaya ya Busega mkoani Simiyu.

Mwakyoma alisema ajali hiyo ilihusisha basi la Mwanza Coach lenye namba T 736 AWJ na Best Line lenye namba 535 AJR, na kwamba chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi wa madereva wa mabasi hayo.

Alisema kuwa watu sita walikufa papo hapo na mmoja alifia katika Hospitali ya Wilaya ya Bunda na kwamba madereva wa mabasi yote mawili walitoroka baada ya ajali hiyo kutokea.

Aliwataja marehemu waliotambuliwa hadi sasa kuwa ni Amina Juma (35) mkazi wa jijini Mwanza, Grace Mlimwa (50), mkazi wa Bunda na Magori Ibrahimu (23) mkazi Bunda.

Alisema kuwa basi la Mwanza Coach lilikuwa linatokea mkoani Mara, likielekea jijini Mwanza wakati Best Line lilikuwa linatokea jijini Mwanza kuelekea Sirari, wilayani Tarime.

Aidha, Mganga Mkuu wa Wilaya ya Bunda, Dk. Rainer Kapinga alisema kuwa wamepokea miili ya watu sita wakiwa ni wanawake watatu na wanaume watatu na kwamba majeruhi mwingine alikufa baada ya kufikishwa hospitalini hapo.

Alisema kuwa majeruhi waliofikishwa hospitalini hapo ni 47, ambapo wanane kati yao wamehamishiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando jijini Mwanza kutokana na hali zao kuwa mbaya.


AJARI YA TREN MISRI YAUA 19

Treni hii ilikuwa imewabeba makurutu wa jeshi
Treni ya kijeshi iliyokuwa imebeba makurutu wa jeshi imeanguka Kusini mwa Misri na kuwaua watu 19 na wengine zaidi ya miamoja kujeruhiwa.
Treni hiyo ilikuwa inaelekea katika kambi ya kijeshi mjini Cairo wakati behewa moja liling'oka na kuangukia treni moja ya mizigo katika eneo la Badrashin mjini Giza.
Waziri mkuu alitembelea eneo la ajali lakini aliokolewa na maafisa wake wa usalama baada ya watu walioshuhudia tukio hilo kumzomea.
Barabara za Misri pamoja na njia zake za reli zina rekodi mbaya sana ya usalama.
Mwezi Novemba mwaka jana watoto walifariki wakati treni walimokuwa wanasafiria ilipogongana na basi lao.
Waziri wa usafiri pamoja na mkuu wa mamlaka ya reli, walilazimika kujiuzulu kufuatia ajali hiyo.
Ghadhabu zimekithiri dhidi ya serikali kwa kukosa kuimarisha usalama wa usafiri wa reli pamoja na miundo msingi mjini Misri.
Watu walioshuhudia ajali ya leo walimzomea waziri mkuu Hisham Qandil wakisema ana damu mikononi mwake kwa kutokea ajali hiyo.
Ripoti zinasema kuwa zaidi ya abiria 1,300, walikuwa kwenye treni hiyo wakati ilipoanguka subuhi ya kuamkia leo.
Mmoja wa walioshuhudia ejali yenyewe alisema kuwa majeruhi walikuwa wamenaswa kwenye vifusi na kwamba magari ya Ambulance hayakuwasili hadi baada ya nusu saa. Miili ilikuwa imetapakaa kila mahali. Usaidizi uliweza kuwafikia tu baada ya saa moja.
Duru zinasema kuwa ajali hii inaweza kuongeza shinikizo dhidi ya serikali kuimarisha usalama wa usafiri wa treni
Miaka minne iliyopita watu kumi na nane waliuawa na wengine wengi kujeruhiwa katika ajali ya treni mbili zilizogongana katika eneo la Giza.
Na mnamo mwaka 2002, treni nyingine iliteketea mjini Cairo, na kuwaua watu 373.

Zilizosomwa zaidi