Monday, January 14, 2013

MAUAJI YA ALBINO YAIBUKA TENA TANZANIA...

    (Mary Owido mlemavu wa ngozi akiwa na watoto wake)
 
Walemavu wa ngozi nchini Tanzania yaani albino wamesema kuwa kumeibuka mbinu mpya zinazotumiwa na makundi ya watu wanaotumia kigezo cha kufunga ndoa na watu wa jamii hiyo na baadaye hutekeleza azma yao ya kuwaua na  kukata viungo vyao.

Kauli hiyo imetolewa na chama cha maalibino nchini Tanzania wakati walipokutana na waandishi wa habari kuelezea hali mpya ya wasiwasi inayowaandama watu wenye ulemavu wa ngozi nchini humo.

Huku wakielezea kuzorota kwa ulinzi na usalama, jamii hii ya walemavu wa ngozi  imesema kuwa serikali haijachukua hatua madhubuti kakabiliana na wimbi la matukio hayo ya kikatili ambayo pia yanahusishwa na imani za kishirikina.

Wale wanaoamini nguvu za kishirikina wamekuwa wakiviwinda viungo vya walemavu wa ngozi katika kile kinachoaminika kuwa  viungo hivyo vina nyota muhimu inayoweza kuwasaidia watu hao kupata utajiri wa mali.

Tangu kuzukwa kwa imani hiyo, mamia ya watu wenye ulemavu wa ngozi wamepoteza maisha wengine wakisababishwa ulemavu wa viungo na wengine kupoteza ndugu na familia zao.

Wakati matukio ya uvamizi na mashambulizi yakipungua kiasi  lakini kumeibuka mbinu mpya ambayo hutumiwa na wajanja wachache kuwarubuni wale wenye  ulemavu wa ngozi kwa minajili ya kufunga nao ndoa lakini baadaye ndoa hiyo hugeuka shubiri.

Wachambuzi wa mambo ya kijamii wanasema kuwa  serikali bado haijapiga hatua kubwa kuwahakikishia amani watu wenye ulemavu wa ngozi na pia huduma zinazotolewa kwao bado ni za kiwango cha chini.

MAMIA WAZUNGUMZIA SUALA LA GESI KUTOKA MTWARA...


Wananchi wa mikoa ya Mtwara na Lindi nchini Tanzania waendelea na malalamiko yao dhidi ya mpango wa serikali kujenga bomba la kusafirisha gesi iliyogunduliwa katika mikoa hiyo ya kusini na kusafirishwa hadi Dar es Salaam.

Wakuu wa usalama walivunja mpango wa maandamano na mkutano ulopangwa wa wanafunzi wa vyuo vya Iringa siku ya Jumapili Januari 13, 2012. Wanafunzi wanaopinga mpango huo wa serikali unaozusha utata, wanadai kwamba sehemu kubwa ya rasilmali hiyo inabidi kuwanufaisha wakazi wa mikoa hiyo badala ya kusafirishwa nje.

Mapema mwezi wa Januari wabunge kutoka Mkoa wa Mtwara waliwalaumu wakuu wa mikoa hiyo ya Mtwara na Lindi kwa kutowaelimisha wananchi juu ya mpango huo baada ya kupelekwa nchi za nje kupata maarifa juu ya namna ya kuwahamasisha wananchi kuhusiana na masuala hayo ya uzalishaji gesi na mafuta.

Mhadhiri wa masuala ya kiuchumi katika chuo kikuu cha Mzumbe, Bakari Mohamed, anasema inabidi kuhakikisha kwamba mapato ya gesi yanabidi kuwanufaisha kwanza wakazi wa mikoa hiyo katika Nyanja zote kabla ya maslahi mengine yoyote ile.

Onesmo Olenguruma, mwanasheria na mtetezi wa haki za binadam anasema kutokana na hictoria ya Tanzania wananchi wa Mtwara na Lindi wanahaki ya kutetea maslahi yao kufuatana na katiba na hasa kutokana na historia ya nchi juu ya namna inavyo tumia rasilmali zake.

Anasema kawaida wananchi wa maeneo ambako rasilmali asili inapatikana hawafaidiki na utajiri huo, kutokana na hiyo inabidi kuwepo na sera na mipango kabambe ya serikali za kuwashirikisha na hapo huwenda wakaridhika
.
Wakati huo huo wakazi wa mikoa mingine ya Tanzania wameanza kuunga mkono madai ya wakazi wa Mtwara na Lindi kudhibiti sehemu kubwa ya mapato ya gesi inayopatikana huko kusini mwa Tanzania

KIONGOZI WA BOKO HARAM AKAMATWA

Maiduguri ni mojawapo ya miji ambayo imeathirika pakubwa kutokana na harakati za Boko Haram

Wanajeshi wa Nigeria wamesema wamemtia nguvuni kiongozi mmoja wa kundi la wapiganaji wa Boko   Haram Mohammed Zangina kaskazini mwa nchi ya Nigeria
Wanajeshi hao wanadai Zangina alihusika kupanga mashambulizi ya kujitolea muhanga katika Miji kadhaa.
Jeshi la Nigeria lilikuwa limetangaza zawadi ya dola laki moja na sitini kwa yeyote atakayemkamata kiongozi huyo.
Kikosi maalum cha jeshi kilisema kilimkamata Zangina mapema Jumapili katika mtaa mmoja wa kifahari mjini Maiduguri ambako ndio ngome ya harakati za Boko Harama.
Hata hivyo duru zinasema kuwa jeshi la Nigeria wakati mwingine huongeza chumvi madai yake kuhusiana na kundi hilo ambalo limehusika na mashambulizi kadhaa Kaskazini mwa nchi.
Taarifa ya jeshi ilisema kuwa alikuwa mjini Maiduguri kupanga mashambulizi dhidi ya raia na maafisa wa usalama
Likitaja miji kadhaa nchini humo, jeshi lilisema kuwa Zangina ndiye amekuwa akiongoza mashambulizi katika miji hiyo ikiwemo Abuja, Kaduna, Kano, Jos na Potiskum."
Jeshi limekuwa likidai kuwakamata vigogo wa kundi hilo katika miezi ya hivi karibuni ingawa hakuna uhakika ikiwa Boko Haram imeathirika kwa vyovyote.

JESHI LA UFARANSA LATUA MALI DHIDI YA WAPIGANAJI WA KIISLAM .....

WAKIMBIZI WAISHI KWA MASHAKA AFRIKA MASHARIKI

Hali mbaya kwa wakimbizi katika kambi ya IFO 1 huko Dadaab, karibu na mpaka wa Kenya na Somalia.
wakimbizi wanaeleza kwamba wanalazimika kuhama kambi kutokana na ukosefu wa huduma za msingi, unyanyasaji, uhalifu, ubakaji na hakuna mfumo wa elimu kwa watoto wanaoishi kwa muda mwingi ndani ya kambi.
Kenya hivi karibuni iliwaamrisha wakimbizi wote walohama katika miji mbali mbali kurudi katika kambi ya Dadaab, kambi kuu ya wakimbizi barani Afrika, hiyo ikiwa njia moja ya kujibu wimbi la masham bulizi ya kigaidi katika miji ya nchi hiyo.

LEODEGER TENGA KUTOGOMBEA TFF 2013

Print E-mail
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Leodegar Tenga amesema hatagombea tena wadhifa huo katika uchaguzi uliopangwa kufanyika Februari 24 mwaka huu.

Akizungumza na Waandishi wa Habari kwenye ofisi za TFF leo, Rais Tenga amesema wakati anaingia kwenye uongozi mwaka 2004 ajenda ilikuwa na kuijenga TFF kama taasisi kwa kuweka mifumo ya uendeshaji ikiwemo kutengeneza katiba na kanuni, jambo ambalo limefanyika
'Wajumbe wamekuwa wakiniuliza Rais vipi? Mimi hapana. Nilishafika pale pa kufika. Tulipoanza wakati ule ilikuwa ni kujenga taasisi. Na kazi hiyo tumeifanya. Tulipoingia mwaka 2004 hiyo ndiyo ilikuwa ajenda,” amesema Rais Tenga.
Amesema walitengeneza Katiba, vyombo huru vya kufanya uamuzi, kuongeza wigo wa wapiga kura ambapo hivi sasa kwenye mpira wa miguu hakuwezi kutokea migogoro, hata ikitokea kuna mfumo wa kuidhibiti.
Rais Tenga ameishukuru Sekretarieti ya TFF, Kamati ya Uchaguzi ya TFF, kamati za uchaguzi za wanachama wa TFF na vyama wanachama wa TFF kwa hatua iliyofikiwa katika uchaguzi ambapo mikoa yote imekamilisha uchaguzi na kubaki vyama shiriki pekee.
Ametoa mwito kwa wadau kujitokeza kugombea uongozi TFF, kwani baada ya kujenga taasisi ajenda iliyobaki ni mpira wa miguu wenyewe ikiwemo nini kifanyika ili mpira uchezwe katika maeneo mbalimbali.
“Tumeshatengeza mfumo, sasa ni kuangalia jinsi ya kuendeleza mpira. Changamoto ni tufanye nini ili mpira uendelee. Tunataka watu wengine wabebe hiyo ajenda ili tuangalie tunakwendaje mbele,” amesema.
Pia amesema ushirikiano ambao amepata kwa wapenzi na wadau wa mpira wa miguu ni wa ajabu. Vilevile ameishukuru vyombo vya habari, Serikali, klabu, wadhamini na wafadhili kwa mchango wao katika uendeshaji wa mpira wa miguu nchini.

ITAZAME HAPA VIDEO YA BE-BLACK FT EDDO "ACHA DHARAU"

HIZI NDIO VURUGU ZILIZOTOKEA LEO JIJINI DA ES SALAAM




WANAFUNZI WA IFM WAVAMIA WIZARA YA MAMBO YANDANI, WALALAMIKIA KUKOSA ULINZI KWENYE HOSTELI ZAO HALI AMBAYO IMESABABISHA WANAFUNZI WAWILI WAKIUME KULAWITIWA 

 Wanafunzi wa Chuo Cha Uongozi wa Fedha cha jijini Dar es Salaam (IFM) wakiwa mbele ya geti la Wizara ya Mambo ya ndani walipovamia leo majira ya saa nne nanusu asubuhi wakiwa na madai ya kutopewa ulinzi na jeshi la polisi kwenye makazi yao ya Hosteli za Kigamboni kutokana na kuvamiwa na majambazi mara kwa mara. Wanafunzi hao walidai siku ya Ijumaa walifanya kikao na jeshi hilo ili wawape ulinzi lakini suala la ajabu siku waliyofanya kikao na Jeshi hilo ndio siku waliovamiwa wenzao wawili wakiume na kubakwa  hali iliyosababishwa wanafunzi hao kubakwa. Majambazi hao wamekua wakidai kupewa Laptop simu na fedha kama mwanafunzi akikataa humfanyia vitendo vya kulawitiwa

 Kamanda wa Polisi wa Kanda maalum ya Kipolisi ya jiji la Dar es Salaam Suleiman Kova akimsikiliza Rais wa Serikali ya wanafunzi ya Chuo cha IFM mara baada ya kuwasili eneo la ofisi za Wizara ya Mambo ya ndani ambapo aliwaamuru wanafunzi hao wafuatane waende hadi Kigamboni kwenye Kituo walichoripoti taarifa zao pamoja na kwenda kwenye Hosteli zao. Kova aliahidi kushughulikia jambo hilo kwa haraka bila kusita.
Wakianza maandamano kuelekea Feli kwaajili ya kuvuka kwenda Kigamboni.
Kova akitoa maelezo kwa waandishi wa habari juu ya hatua zitakazochukuuliwa baada ya kupata taarifa hizo ambapo aliwaamuru wanafunzi hao wote kwapamoja kwenda Kigamboni kufuatilia tukio hilo kwa pamoja.
Mitaani Posta.

Tunaimba! Tunavuka bure Tunavuka bure kwenye Pantoni.
Kova akishangiliwa wakati wa safari kuelekea Feli.

Kwenye Kona ya feli kuwania geti ili waingie bure!

Wakajazana kupita kiasdi Kova akazuia kivuko kisiondoke hadi wapungue!
Hapa wakigoma kupungua kazi iliyochukua zaidi ya Saa moja hadi kivuko kuendelea na kazi ya kuvusha abiria.

Zilizosomwa zaidi