Saturday, January 12, 2013
MATOKEO YA MECHI ZILIZOCHEZWA JANA TAR 12 JAN KATIKA BARCLAYS NA ENGLISH CHAMPIONSHIP YAKO HAPA....
Barclays Premier League
AZAM KULITWAA KOMBE LA MAPINDUZI KWA MARA NYINGINE
Azam FC yatwaa kwa mara ya pili Kombe la Mapinduzi
Azam FC imeweza kutetea kombe hilo na kulibakisha
nchini katika mchezo ulitumia dakika 120 kumalizika kwenye Uwanja wa
Amaan, visiwani Zanzibar.
Goli la mshambuliaji Gaudence Mwaikimba wa Azam FC ndilo limeipatia ubingwa
wa
Kombe la Mapinduzi kwa mara ya pili mfululizo katika mchezo ulimalizika
kwa Azam FC kupata ushindi wa magoli 2-1 dhidi ya Tusker
FC ya Kenya.
Mabingwa hao kwa mara ya pili walipewa medali za dhahabu, kombe na
kitita cha shilingi milioni kumi kama zawadi ya kutwaa ubingwa huo.
Katika mchezo huo kipindi cha kwanza kilimalizika kwa timu zote bila
kufungana, kipindi cha pili Tusker walianza kupata bao kupitia kwa
mchezaji Jese Were aliyetumia uzembe wa beki ya Azam FC katika dakika ya
59.
Azam FC kupitia kwa beki wake mpya Jockins Atudo
alisawazisha goli hilo kwa mkwaju wa penati baada ya mchezaji wa Tusker
Luke Ochieng kunawa mpira wakati akizui mpira wa kichwa uliopigwa na
Mwaikimba, penati ilimriwa na mwamuzi Ramadhan Kibo.
Goli hilo la kusawazisha kwa Atudo, ni goli lake la nne katika mashindano hayo, akifuatiwa na Mwaikimba mwenye magoli mawili.
Matokeo ya sare ya 1-1 yalimaliza dakika 90, katika dakika za nyongeza
Mwaikimba alitumia vema nafasi aliyoipata katika dakika ya 92 na
kupachika goli hilo wavuni na kumaliza mchezo Azam FC ikitwaa ubingwa
kwa ushindi wa 2-1.
Baada ya goli hilo Azam FC walituliza mpira chini na kucheza mtindo wa kulinda lango lao kwa muda wote wa dakika 28 zilizobaki.
Katika mchezo wa leo Azam FC walifanya mabadiliko mawili, walitoka
Uhuru Seleman dk 64 nafasi yake ikachukuliwa na Abdalah Seif na dk 126
aliingia Malika Ndeule kuchukua nafasi ya Brian Umony.
Tusker
walifanya mabadiliko walitoka Fredrick Onyango, Andrew Tololwa, Jese
Were, Khalid Aucho na Ismail Dunga nafasi zao zikachukuliwa na Mark
Odhiambo, Edwin Ombasa, Andrew Sekayambya, Benson Amianda na Michael
Olunga.
Baada ya kutwaa Kombe hilo, kocha mkuu wa Azam FC
amewapongeza wachezaji wake kwa kubakisha kombe hilo na kusema ni
muendelezo wa mipango ya mafanikio katika klabu hiyo.
Amesema
safari inaendelea ya kupeleka makombe katika klabu hiyo, walianza na
Mapinduzi 2012, Ngao ya Hisani walilochukua nchini Congo DRC na hili la
Mapinduzi 2013.
Kikosi cha Azam FC kilichotwaa ubingwa, Mwadini
Ally, Himid Mao, Samih Haji Nuhu, David Mwantika, Jockins Atudo,
Michael Bolou, Humprey Mieno, Khamis Mcha, Gaudence Mwaikimba, Uhuru
Seleman/Seif Abdalah 64’ na Brian Umony/Malika Ndeule 126’.
Wengine waliokuwa na kikosi hicho, Aishi Salum, Wandwi Wiliam, Luckson
Kakolaki, Omary Mtaki, Abdi Kassim ‘Babi’, Jabir Aziz, Ibrahim
Mwaipopo,Salum Abubakar, Tchetche Kipre kabla ya kuumia, waliokosa
mashidano hayo ni Abdulhalim Humud, John Bocco, Waziri Salum ambao ni
majeruhi.
Azam FC yatwaa kwa mara ya pili Kombe la Mapinduzi Azam FC imeweza kutetea kombe hilo na kulibakisha nchini katika mchezo ulitumia dakika 120 kumalizika kwenye Uwanja wa Amaan, visiwani Zanzibar.
Goli la mshambuliaji Gaudence Mwaikimba wa Azam FC ndilo limeipatia ubingwa wa Kombe la Mapinduzi kwa mara ya pili mfululizo katika mchezo ulimalizika kwa Azam FC kupata ushindi wa magoli 2-1 dhidi ya Tusker FC ya Kenya.
Mabingwa hao kwa mara ya pili walipewa medali za dhahabu, kombe na kitita cha shilingi milioni kumi kama zawadi ya kutwaa ubingwa huo.
Katika mchezo huo kipindi cha kwanza kilimalizika kwa timu zote bila kufungana, kipindi cha pili Tusker walianza kupata bao kupitia kwa mchezaji Jese Were aliyetumia uzembe wa beki ya Azam FC katika dakika ya 59.
Azam FC kupitia kwa beki wake mpya Jockins Atudo alisawazisha goli hilo kwa mkwaju wa penati baada ya mchezaji wa Tusker Luke Ochieng kunawa mpira wakati akizui mpira wa kichwa uliopigwa na Mwaikimba, penati ilimriwa na mwamuzi Ramadhan Kibo.
Goli hilo la kusawazisha kwa Atudo, ni goli lake la nne katika mashindano hayo, akifuatiwa na Mwaikimba mwenye magoli mawili.
Matokeo ya sare ya 1-1 yalimaliza dakika 90, katika dakika za nyongeza Mwaikimba alitumia vema nafasi aliyoipata katika dakika ya 92 na kupachika goli hilo wavuni na kumaliza mchezo Azam FC ikitwaa ubingwa kwa ushindi wa 2-1.
Baada ya goli hilo Azam FC walituliza mpira chini na kucheza mtindo wa kulinda lango lao kwa muda wote wa dakika 28 zilizobaki.
Katika mchezo wa leo Azam FC walifanya mabadiliko mawili, walitoka Uhuru Seleman dk 64 nafasi yake ikachukuliwa na Abdalah Seif na dk 126 aliingia Malika Ndeule kuchukua nafasi ya Brian Umony.
Tusker walifanya mabadiliko walitoka Fredrick Onyango, Andrew Tololwa, Jese Were, Khalid Aucho na Ismail Dunga nafasi zao zikachukuliwa na Mark Odhiambo, Edwin Ombasa, Andrew Sekayambya, Benson Amianda na Michael Olunga.
Baada ya kutwaa Kombe hilo, kocha mkuu wa Azam FC amewapongeza wachezaji wake kwa kubakisha kombe hilo na kusema ni muendelezo wa mipango ya mafanikio katika klabu hiyo.
Amesema safari inaendelea ya kupeleka makombe katika klabu hiyo, walianza na Mapinduzi 2012, Ngao ya Hisani walilochukua nchini Congo DRC na hili la Mapinduzi 2013.
Kikosi cha Azam FC kilichotwaa ubingwa, Mwadini Ally, Himid Mao, Samih Haji Nuhu, David Mwantika, Jockins Atudo, Michael Bolou, Humprey Mieno, Khamis Mcha, Gaudence Mwaikimba, Uhuru Seleman/Seif Abdalah 64’ na Brian Umony/Malika Ndeule 126’.
Wengine waliokuwa na kikosi hicho, Aishi Salum, Wandwi Wiliam, Luckson Kakolaki, Omary Mtaki, Abdi Kassim ‘Babi’, Jabir Aziz, Ibrahim Mwaipopo,Salum Abubakar, Tchetche Kipre kabla ya kuumia, waliokosa mashidano hayo ni Abdulhalim Humud, John Bocco, Waziri Salum ambao ni majeruhi.
WATU 25 WANUSURIKA KIFO KATIKA AJARI YA NDEGE YA ATCL
STORY YA POLISI KUTIWA MBALONI KWA WIZI WA MILLIONI 150 IKO HAPA
Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es
Salaam linashikilia askari Polisi watano kwa tuhuma za kuhusika na
upotevu wa Sh milioni 150 zilizoporwa na watu wanaosadikiwa kuwa
majambazi eneo la Kariakoo.Sambamba na askari hao pia wamekamatwa watu wawili wanaodaiwa kuhusika na tukio hilo ambao ni Deogratias Kimaro (30), mkazi wa Kalakata na Kulwa Mwakabala (30) mkazi wa Kijiwesamli Ilala.
Akizungumza na waandishi wa habari jana Dar
es Salaam, Kamanda wa Kanda hiyo, Suleiman Kova alisema askari hao
wanashikiliwa kutokana na uchunguzi wa kina uliofanywa na jopo la
upelelezi likiongozwa na Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai wa Kanda
hiyo, Ahmed Msangi.
Alisema baada ya tukio hilo zilipatikana
taarifa kwamba fedha hizo zilipotea baada ya mtuhumiwa Augustino Kayula
au Frank Mwangiba, kukamatwa akiwa na bastola aina ya Browning bila
fedha zilizoporwa wakati inasemekana ndiye aliyepora fedha hizo akiwa na
wenzake.
“Askari hawa tunawashikilia na tayari mashitaka ya kijeshi yameanza huku uchunguzi ukiendelea na utakapokamilika, tutapeleka jalada kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa hatua za kisheria ili kuleta uwazi na uwajibikaji ndani ya jamii yetu”.
Alisema Jeshi hilo limekuwa likionesha uwajibikaji ambapo mwaka jana pekee askari 20 walichukuliwa hatua mbalimbali za kinidhamu.
Aidha, alisema majina ya askari hao yanahifadhiwa kwa sasa, kwa ajili ya usalama na wakati ukifika yatawekwa wazi huku polisi wakiendelea na upelelezi na gwaride la utambulisho.
Alisema baada ya tukio hilo kulikuwa na taarifa zenye kutuhumu askari hao juu ya upotevu wa fedha hizo na ndipo uchunguzi ulipoendelea ili kubaini ukweli.
“Baada ya uchunguzi wa kina na ushahidi uliokusanywa, umefanya askari hao washikiliwe na kuhojiwa … pamoja na uchunguzi askari kwanza watajibu mashitaka ya kijeshi,” alisema.
Katika tukio hilo la uporaji Desemba mwaka jana, inadaiwa Kayula na wenzake wakiwa wamepanda pikipiki mtindo wa ‘mshikaki’, walivamia duka la Kampuni ya Artan Limited na kupora Sh milioni 150, zilizokuwa zikitolewa dukani Kariakoo kwenda benki, ambapo watu watatu walipoteza maisha.
Waliopoteza maisha ni pamoja na mtuhumiwa Kayula, Sadiki Juma (38) na Ahmed Issa (55) waliopigwa risasi na majambazi katika eneo la tukio.
Katika hatua nyingine, Kova alikanusha taarifa kwamba alisema ameunda tume ya kuchunguza tukio la kiongozi wa Jumuiya ya Madaktari, Dk Stephen Ulimboka badala yake akasema ameunda Jopo la Upelelezi.
ALIYEPIGA PICHA NA LEMA AKIWA NA SARE ZA JWTZ, ATUPWA JELA MIAKA MINNE.
MTU aliyepiga picha na Mbunge wa Arusha mjini,
Godbless Lema akiwa amevalia sare za Jeshi la Wananchi wa Tanzania
(JWTZ), amehukumiwa kifungo cha miaka minne jela.Abubakari Kikulu (29), alipiga picha na mbunge huyo Desemba 23 mwaka jana, baada ya Lema kumaliza kuhutubia mkutano wa hadhara eneo la Mererani, ikiwa ni sehemu ya mikutano aliyoifanya kutokana na Mahakama ya Rufani Tanzania kumrejeshea ubunge wake.
Mbali na kupiga picha hiyo na Lema pamoja na Mbunge wa Arumeru Mashariki Joshua Nassari, kijana huyo alionekana katika picha hiyo akionyesha vidole viwili, ambayo ni alama ya Chadema.
Baada ya picha hiyo, JWTZ lilimtilia shaka kijana huyo na kutangaza rasmi kumsaka, ili lijiridhishe kama ni mmoja wa wanajeshi wake.
Baada ya kumsaka kwa takriban siku 12, kijana huyo alikamatwa Januari 13, katika Mji wa Bomang’ombe wilayani Hai na baada ya kupekuliwa alikutwa na sare hizo.
Jana, Kikulu alifikishwa mahakamani mjini Moshi, akiwa chini ya ulinzi wa polisi na kusomewa mashtaka mawili, ambayo yote alikiri kuyafanya kama ilivyodaiwa mahakamani.
Baada ya kukiri kosa hilo Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Mkoa wa Kilimanjaro, alimhukumu kifungo cha miaka minne jela, ili iwe fundisho wa wakosaji wengine wa aina hiyo.
Kabla ya hukumu hiyo, Wakili wa Serikali, Ignas Mwinuka alimsomea mshtakiwa huyo mashitaka yake mawili, likiwamo la kujifanya Ofisa wa Jeshi, wakati akijua ni uongo.
Wakili huyo alidai mahakamani kuwa Januari 3, mwaka huu katika eneo la Bomang’ombe wilayani Hai, mtuhumiwa huyo alijitambulisha kama mtumishi wa umma.
Katika shtaka la pili, wakili huyo alidai siku hiyo hiyo katika Mtaa wa Msikitini, eneo hilo la Bomang’ombe, mtuhumiwa alipatikana na sare za JWTZ kinyume cha sheria.
Sare hizo ni pamoja na suruali moja, mashati mawili na kofia mbili, vyote vikiwa na alama za Jeshi la Wananchi wa Tanzania la Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Baada ya Hakimu Kobelo kumuuliza mshtakiwa kama ni kweli alitenda makosa anayoshitakiwa, mshtakiwa huyo alikiri makosa yake katika hali ambayo haikutarajiwa.
Kutokana na kukiri kwake makosa hayo, Hakimu Kobelo alimhukumu kifungo cha miaka miwili kwa kosa la kwanza la kujifanya Ofisa wa JWTZ na miaka mingine miwili kwa kosa la pili.
Hata hivyo, Hakimu Kobelo alisema kuwa kwa kuwa adhabu hizo zinakwenda kwa pamoja, mshtakiwa huyo atatumikia kifungo cha miaka miwili jela.
Kwa mujibu wa hakimu huyo, kosa alilolifanya mtuhumiwa huyo ni baya na linastahili adhabu kali, ili iwe fundisho kwa watu wengine wanaotumia vibaya sare za majeshi nchini.
Subscribe to:
Posts (Atom)
Zilizosomwa zaidi
-
Israel Magesa Wakili Magesa aliyeko (pichani) amefariki dunia ghafla leo asubuhi. Wakili Magesa, ambaye ni mmiliki wa kampuni y...
-
GARI aina ya Toyota VX linaloelezwa kuwa mali ya Serikali limekamatwa na polisi likiwa limebeba pembe za ndovu. ...
-
-
Jeshi la Polisi mkoani Mtwara limemkamata mbunge wa Mtwara Mjini (CCM), Hasnain Murji likimtuhumu kuchochea vurugu za kupinga mradi wa bo...
-
Nimepokea mwaliko wa kikao maalumu cha kikao cha fedha na uongozi wa tarehe 3/01/2014 kikao kufanyika tarehe 06/01/2013 saa nane mchana ...












