Friday, January 11, 2013
TAIFA STARS IMEKUBALI KICHAPO KUTOKA KWA ETHIOPIA
Mchezo wa kirafiki uliochezwa leo kati ya wenyeji Ethiopia na Taifa Stars
umemalizika kwa ushindi wa Ethiopia kwa magoli mawili yaliyofungwa na Fuad Ibrahim na Shimelis Bekele huku bao pekee la Stars lifungwa na Mrisho Ngassa
umemalizika kwa ushindi wa Ethiopia kwa magoli mawili yaliyofungwa na Fuad Ibrahim na Shimelis Bekele huku bao pekee la Stars lifungwa na Mrisho Ngassa
MATOKEO YA KIDATO CHA PILI NJE NJE...
Matokeo ya kidato cha pili yametangazwa leo na Naibu
waziri wa Elimu Bw.Philip Mulugo
kupitia vyombo vya habari na yako hivi:
Waliofanya mtihani 386,248
Waliofanya mtihani 386,248
Waliofaulu 249,325 (65%)
Waliofeli 136,923 (35%
HIVI NDIO VIWANGO VYA JOTO LEO TAR 11 JAN 2013
|
||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||
|
|
||||||||||||||||||||||||||||
|
|
||||||||||||||||||||||||||||
| |||||||||||||||||||||||||||||
HILI NDIO LA WANA HABARI NDANI YA KATIBA MPYA
Wanahabari wataka uhuru zaidi wa habari: JUKWAA la Wahariri Tanzania (TEF) limependekeza Katiba mpya ijayo itambue uhuru wa vyombo vya habari, haki ya kupata habari na uhuru wa kutoa habari.
OMBAOMBA ALIEJIFANYA MLEMAVU ATIMUA MBIO BAADA YA KUGUNDULIKA SIO MLEMAVU
Tukio hilo limetokea majira ya saa 8 mchana baada ya ya wanahabari kuzungukia maeneo hayo kushuhudia umati wa wananchi wakiendelea kumpa fedha mzee janja.
WABUNGE KENYA KULIPWA DOLA 107,000

Wabunge nchini Kenya
wamejizawadia dola 107,000 kama marupurupu katika mojawpao ya vikao
vyao vya mwisho vya bunge hilo kabla ya uchaguzi mkuu kufayika mwezi
Machi.
Wabunge wa Kenya ni miongoni mwa wabunge wanaopokea mishahara ya juu zaidi barani Afrika kila mmoja akipata dola elfu kumi na tatu kila mwezi.
Lakini mshahara wa mkenya wa kawaida ni takriban dola 1,700 kila mwezi.
Mswaada huu, ulipitishwa siku ya Jumatano na wabunge chini ya thelathini waliokuwa bungeni. Walikarabati bunge lao kwa kutumia dola milioni kumi na mbili kulingana na stakabadhi za bunge zilizotolewa hapo jana.
Malipo haya ni sawa na yale yaliyokuwepo katika mswaada walioupitisha mwezi Oktoba, lakini wakati huu wabunge hao pia wamependekeza marupurupu kwa rais ambaye atalipwa dola laki tatu sawa na makamu wa rais na waziri mkuu.
Alipotupilia mbali mswaada wa kwanza , Rais Kibaki lisema kuwa haiwezekani kwa wabunge kulipwa mamilioni ya dola wakati uchumi ungali umedumaa.
Tume ya kushughulikia mishahara ya wafanyakazi wa umme, iliambia wakenya kuwa hakuna uhakika ikiwa hatua yao inakuika katiba.
Mashirika ya kutetea haki za kibinadamu yameelezea kukerwa sana na hatua ya wabunge. Tayari waziri mkuu Raila Odinga amepinga mswaada huo akisema kuwa ni kama uhalifu dhidi ya wakenya na kwamba anashauriana na rais Mwai Kibaki kuhusu hatua itakayokuwa sawa kwa wakenya.
Kutoka bbc
Subscribe to:
Posts (Atom)
Zilizosomwa zaidi
-
Israel Magesa Wakili Magesa aliyeko (pichani) amefariki dunia ghafla leo asubuhi. Wakili Magesa, ambaye ni mmiliki wa kampuni y...
-
GARI aina ya Toyota VX linaloelezwa kuwa mali ya Serikali limekamatwa na polisi likiwa limebeba pembe za ndovu. ...
-
-
Jeshi la Polisi mkoani Mtwara limemkamata mbunge wa Mtwara Mjini (CCM), Hasnain Murji likimtuhumu kuchochea vurugu za kupinga mradi wa bo...
-
Nimepokea mwaliko wa kikao maalumu cha kikao cha fedha na uongozi wa tarehe 3/01/2014 kikao kufanyika tarehe 06/01/2013 saa nane mchana ...














