Wednesday, December 26, 2012

NELSON MANDELA AREJEA NYUMBANI KUTOKA HOSPITALI

Former South African president Nelson Mandela looks on as he celebrates his birthday at his house in Qunu, Eastern Cape July 18, 2012. REUTERS/Siphiwe Sibeko
Baada ya kuugua kwa mda sasa, rais wa zamani wa Afrika kusini arejea nyumbani kwake baada ya kupata nafuu

MATOKEO YA MECHI ZILIZOMALIZIKA BACLAYS PREMIER YAKO HAPA

 

Everton2 - 1Wigan Athletic
Fulham1 - 1Southampton
Manchester United4 - 3Newcastle United
Norwich City0 - 1Chelsea
Queens Park Rangers1 - 2West Bromwich Albion
Reading0 - 0Swansea City
Sunderland1 - 0Manchester City
Aston Villa0 - 4Tottenham Hotspur

MOTO WATEKETEZA MAJENGO HUKO NIGERIA


Mlipuko mjini LagosMaafisa wa kuzima moto wakiendelea na kuzima moto katika ghala moja lililolipuka Lagos.
Moto mkubwa umetokea katika mji mkuu wa Nigeria Lagos.
Taarifa zinaarifu kuwa moto huo ulianza katika eneo la kuhifadhi baruti na kisha kuenea kwa haraka katika majengo mengine yaliyo karibu na ghala hilo.
Baadhi yamajengo yanaendelea kuteketea.
 

TAARIFA KAMILI YA PADRE ALIYEPIGWA RISASI JANA HUKO ZANZIBAR IKO HAPA

Father Ambros Mkenda wa Parokia ya Mpendae katika Kanisa Katoliki Mjini Zanzibar amepigwa risasi na watu wasiojulikana nje ya nyumba yake majira ya saa 12 jioni wakati akitokea kanisani

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mjini Magharibi Aziz Juma Mohammed amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambalo alisema Father amepigwa risasi na ameumizwa sehemu ya kichwa na amekuwa akitoka damu nyingi kichwani na tayari anapatiwa matibabu katika hospitali kuu ya Mnazi Mmoja.

Alisema jeshi la polisi linaendelea na uchunguzi wa tukio hilo ili kubaini wahusika walifanya uhalifu huo kwa madhumuni gani kabla ya kuchukuliwa hatua za kisheria.

“Sisi tunahesabu kuwa kitendo hiki ni kitendo cha kihalifu na tunawatafuta wahalifu waliofanya kitendo hiki kwa hivyo bado ni mapema kusema kwamba kitendo hiki kimefanywa na nani kwa kuwa bado uchunguzi wetu unaendelea na hadi sasa hakuna mtu tuliyemshika kuhusikana na tukio hili” alisema Kamanda.

Kamanda Aziz akisimulia tukio hilo alisema walipata taarifa majira ya saa 2 na kwenda katika eneo la tukio ambapo Father alikuwa akitokea kanisani na kutaka kuelekea nyumbani kwake wakati akiwa ndani ya gari ndipo aliposhambuliwa na watu wasiojulikana na kuanguka.

“Tumekuta mabaki ya risasi ndani ya gari yake na katika vioo vyake vya gari vimevunjika na tumekuta damu chini pale” alisema Kamanda.

Aidha Kamanda Azizi alisema Father Ambros yeye ni mhasibu pale kanisani na hivyo mara nyingi watu wananaamini kwamba katika siku za krismass mara nyingi sadaka hukusanywa fedha nyingi na hivyo wanamini kwamba alikuwa fedha mikononi na ndipo inawezekana waliamua kumpiga risasi wakitaka kuchukua fedha hizo.

Hata hivyo alisema uchunguzi wa awali ndio utakaoeleza ni suala gani lililopelekea kupigwa risasi lakini wanaendelea na uchunguzi huo ambapo uchunguzi ndio utakaojulikana sababu kamili ya tukio hilo.

Akizungumzia tukio hilo, Askofu Michael Hafidh wa Kanisa la Anglikan la Mkunazini amesema wamesikitishwa na wamepokea kwa mshituko mkubwa tukio hilo hasa kwa kuzingatia matukio kama hayo hayajawahi kutokea ya kuwahujumu viongozi wa dini.

Alisema tukio hilo ni miongoni mwa matukio ya kushtusha na yanaashiria hali mbaya ya kiusalama na kuwaomba viongozi wa serikali kuchukua hatua za tahadhari kubwa kwani matukio kama hayo yameanza kutokea kwa viongozi wa dini ambapo mwanzo ilianzia kwa Sheikh Soraga na baadae kutokea kwa Father Ambros.

“ Hii ni hali ya hatari katika nchi yetu na haipendezi lakini serikali lazima ijue sisi hatuwezi kujua wala hatuwezi kujilinda lakini serikali inapaswa kutulinda sisi ndio wananchi wake” alisema Askofu Hafidh.

Askofu Hafidh alisema hivi karibuni kumekuwepo vipeperushi vilivyosambazwa na watu vikiwatisha watu wenye imani ya kikristo ambapo alisema miongoni mwao walikuwa na khofu juu ya kusambazwa kwa vipeperushi hivyo na kuiomba serikali iongeze ulinzi.

“Tumeona hivi vipeperushi na kwa kweli tulikuwa na khofu juu ya vipeperushi hivi lakini ndio tunasema tunaelekea wapi katika maisha haya” alisema Akofu Hafidh.

“Sisi hatuamini kwamba kuna kisasi kwa viongozi wa dini lakini tunachukulia hilo ni tukio la kihalifu na pia hatuna vipeperushi vya aina yoyote vinavyoelezea kuwatisha viongozi wa dini kwa hivyo tunachukulia hayo ni matukio ya kihalifu na wala hatuamini kwamba matukio haya ni ya dini fulani” alisema Kamanda Azizi.

Akielezea kuhusiana na hilo Kamanda Aziz alisema jeshi la polisi limejipanga na kuzidisha ulinzi katika maeneo yote ya makanisa ambapo kumesambazwa polisi wa kutosha kwa kuwa wanajua wakati wa sherehe mambo ya kihalifu hujitokeza.

“Sisi kawaida huwa tunaweka ulinzi siku za sherehe zozote lakini kwanza makanisa yote yamewekwa ulinzi wa kutosha kabisa lakini wahalifu wanapotaka kufanya uhalifu huwezi kujua watatumia mbinu gani na saa ngapi na watafanya uhalifu huo wapi, lakini ulinzi upo wa kutosha” alisisitiza Kamanda Aziz

HUU NDIO UJUMBE WA PAPA BENEDICT WA 16 KWENYE TWITTRER

 


Papa akituma ujumbe wake wa Twitter
Papa Benedict wa 16 ametuma ujumbe wake wa kwanza kwenye akaunti yake yaTwitter. Ujumbe huu ulikuwa umesubiriwa kwa hamu sana.
Alionekana akibonyeza kwenye tabiti yake ya iPad na kutuma ujumbe huo
UJumbe wake ulikuwa unasoma hivi ''Marafiki wapendwa, nimefurahi sana kuwasiliana nanyi kupitia Twitter. Asanteni sana kwa ujumbe wenu na ninawabariki nyote.''
Msemaji wake alisema kuwa ujumbe wa Papa utafikia kila mtu amjuaye kwa kutumia akaunti zake zilizo kwenye lugha saba.

Akaunti ya papa iliyo kwenye lugha ya kiingereza tayari ina wafuasi zaidi ya laki sita.
Akaunti zake zote ambazo ni @pontifex zinafuatana moja baada ya nyingine.
Mwaka jana Papa alituma ujumbe wake wa kwanza kutoka Vatican kuweza kuzindua mtandao wake wa maelezo mbali mbali.
Papa ni kiongozi wa waumuni bilioni 1.2 wa kikatoliki na atakuwa akitia saini ujumbe wake wala hatoundika mwenyewe.

WATOTO WAKISHEREHEKEA KRISMASS DAR LIVE.



Ratiba ya English League Championship leo!!!

12:15Nottingham ForestvLeeds United
13:00Charlton AthleticvIpswich Town
15:00BarnsleyvBirmingham City
15:00Bolton WanderersvSheffield Wednesday
15:00Bristol CityvWatford
15:00BurnleyvDerby County
15:00Cardiff CityvCrystal Palace
15:00Huddersfield TownvBlackpool
15:00Hull CityvLeicester City
15:00MiddlesbroughvBlackburn Rovers
15:00Wolverhampton WanderersvPeterborough United

RATIBA YA BARCLAYS PREMIER LEAGUE LEO TAR 26 DEC HII HAPA.

 

15:00Evertonv/sWigan Athletic
15:00Fulhamv/sSouthampton
15:00Manchester Unitedv/sNewcastle United
15:00Norwich Cityv/sChelsea
15:00Queens Park Rangersv/sWest Bromwich Albion
15:00Readingv/sSwansea City
15:00Sunderlandv/sManchester City
17:30Aston Villav/sTottenham Hotspur
19:45Stoke Cityv/sLiverpool

INGIA HAPA UANGALIE PICHA MBALIMBALI ZA KRISMASS...




***Tunawatakia Heri ya Krismas ...**


Chukua Hii.

Mfano umepata nafasi ya kum-wish mtu mmoja tu Heri ya Christmas na Mwaka mpya kati ya watu wako wengi na wa karibu uwapendao.

Utampa nafasi hii ya kwanza na ya heshima nani na kwanini? 

Je atakuwa ni

1. Baba
2. Mama
3. Kaka
4. Dada
5. Girlfriend/Boyfriend
6. Teacher/Lecturer
7. Pastor

Who else... Specify here... Unaweza mtaja jina pia kumwonyesha umuhimu wake kwako.

#MERRYCHRISTMAS


Marry X-Mass mdau wangu wa ukweli.
Sherehekea sikuku hii kwa kiasi.
Sponsored by farajadogeje.blogspot.com


Salamu za Xmas zinaendelea kumiminika,

Kuna hii hapa all the way from BUKOBA - Unaizungumziaje?

Vipi mipangoz leo, unampango wa ku-spend siku wapi? Swali la kizushi hapa? Unafikiri kwanini kibongobongo PILAU ndio msosi mkubwa wa sikukuu/sherehe?

On behalf of Royal Media Services, We wish you all the peace, joy, and love of the season! Merry Christmas!!!


EA BREAKFAST.....MERRY CHRISTMASS TO YOU AND YOURS...nini unachokithamini kuhusu siku hii?

Zilizosomwa zaidi