Saturday, December 15, 2012

KWA HABARI MBALIMBALI ZA KITAIFA,KIMATAIFA, MICHEZO NA BURUDANI.. TEMBELEA BLOG HII.

BAADHI YA MAENEO KUTOHAMIA DIGITAL

MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), imewatoa
 hofu wananchi wote wanaoishi katika maeneo ambayo bado 
kufikiwa na mfumo mpya wa mawasiliano wa digitali, akisema
 wataendelea kupata mawasiliano kupitia mfumo wao wa zamani 
wa analojia.
 Kauli hiyo ilitolewa jijini Dar es Salaam jana na Meneja wa 
Mawasiliano wa mamlaka hiyo, Innocent Mungi wakati akifafanua
 kuhusu wasiwasi uliojitokeza kwa wananchi hasa walioko mikoani.
Mungi alisema watazima mtambo wa zamani kule ambako huduma hiyo
 mpya ya digitali imefika, kwamba kwenye maeneo ambayo hayajafikiwa na
 mtambo huo, wataendelea kutumia televisheni zao kupitia mfumo wa zamani.
 Alibainisha kuwa, hadi sasa ni asilimia 24 sawa na mikoa 11 ya nchi ndiyo 
itafaidika na mawasiliano hayo ya digitali, ambapo kule kusikokuwa na mawasiliano hayo
 bado wataendelea kupata mawasiliano kwa kutumia satelaiti, madishi na usambazaji wa 
nyaya hadi hapo mfumo mpya utakapowafikia.

KITUO CHA POLISI CHACHOMWA MOTO, POLISI WAWILI WAFARIKI HUKO NGARA

VITENDO vya wananchi kujichukulia sheria mikononi vinaendelea kushika kasi ambapo askari wawili wa Jeshi la Polisi Wilaya ya Ngara mkoani Kagera, wanadaiwa kuuwa na wananchi wenye hasira kali jana.
Mauaji hayo yalifanyika baada ya wananchi hao kuvamia na kukichoma moto kituo cha polisi cha Mugoma wilayani humo baada ya askari hao kudaiwa kumpiga risasi fundi wa pikipiki.

Kwa mujibu wa mashuhuda, tukio hilo lilitokea mchana wakati askari kadhaa wa kitengo cha usalama barabarani walipofika kwa fundi pikipiki huyo na kutaka kuichukua pikipiki aliyokuwa akiitengeneza kwa madai kuwa ilikuwa na makosa.Kwamba fundi huyo aligoma na kueleza kuwa asubiriwe mwenye pikipiki ili kuepuka kudaiwa chombo hicho cha usafiri.

Mmoja wa mashuhuda hao, aliyatambulika kwa jina moja la Libela, alidai kuwa baada ya mvutano wa muda mfupi, askari hao walifyatua risasi na kumpiga fundi huyo mguuni na kifuani, hivyo kusababisha kifo chake.
Aliongeza kuwa, tukio hilo liliwapandisha hasira wananchi na kuwafukuza askari hao waliokimbilia katika kituo hicho cha polisi.

Lebela alifafanua kuwa, wananchi hao waliamua kukichoma moto kituo hicho hatua iliyosababisha askari waliokuwemo kutoka na kukimbia kila mmoja na muelekeo wake.

Alisema kuwa askari aliyetajwa kwa jina la Koplo Paschal alianguka wakati akijinusuru, hivyo kuvamiwa na wananchi waliokuwa na zana mbalimbali za jadi ambazo walitumia kumshambulia na kumuua papo hapo.
Wananchi hao pia wanadaiwa kumfuata askari mwingine anayetajwa kwa jina la Pc Alex aliyekuwa amekimbilia kwenye nyumba ya mwananchi mmoja na kumtoa kwa nguvu na kisha kuanza kumshambulia hadi kumuua.
STORY na Mbeki Mbeki,

RATIBA YA LEO BARCLAYS HII HAPA


Tottenham HotspurvSwansea City

West Bromwich AlbionvWest Ham United

MATOKEO YA MECHI ZA JANA KATIKA BARCLAYS PREMIER LEAGUE NA ENGLISH CHAMPIONSHIP YAKO HAPA.


Hull City2 - 0Huddersfield Town

Birmingham City2 - 2Crystal Palace

Blackpool2 - 0Blackburn Rovers

Bolton Wanderers2 - 0Charlton Athletic

Brighton & Hove Albion0 - 0Nottingham Forest

Bristol City0 - 2Derby County

Burnley1 - 1Watford

Cardiff City1 - 2Peterborough United

Leeds United2 - 0Ipswich Town

Middlesbrough2 - 0Wolverhampton Wanderers

Millwall1 - 0Leicester City

Barnsley0 - 1Sheffield Wednesday

HUYU NI NYOKA WA AINA YAKE.........

ALICHOKISEMA OBAMA KUHUSU MAUAJI YALIYOTOKEA KIKO HAPA

Rais Obama akifuta machozi baada ya taarifa za mauji ya watoto wadogoKufuatia ya moja kati ya mauaji makubwa kutokea katika historia ya Marekani, wanasiasa akiwemo Rais Barack Obama, wametaka sheria kuhusu umiliki wa bunduki nchini Marekani zibadilishwe, ili kuepusha maafa kama hayo siku za usoni.

   

Akizungumza baada ya mauaji ya watoto na watu wazima 26 katika shule moja ya msingi katika jimbo la Connecticut Ijumaa, Rais Obama aliyeonekana kujawa na huzuni, alitoa wito kuchukuliwe hatua ya maana kuzuwia mauaji kwa kutumia bunduki.
Hakutoa maelezo zaidi.
Taarifa zaidi zimejitokeza kuhusu yaliyotokea katika mauaji hayo katika shule ya msingi ya Sandy Hook mjini Newtown.
Mshukiwa mwenye umri wa miaka 20 - aliyeitwa Adam Lanza - alimuuwa mama yake nyumbani kwake, kabla ya kuelekea katika shule hiyo na kuwafyatulia risasi wanafunzi.
Walioshuhudia walisema walisikia zaidi ya milio mia moja ya risasi na kuwaona watoto waliokuwa wakihofia maisha yao wakilikimbia jengo.
Wanafunzi hao walikuwa kati ya umri wa miaka mitano na kumi.
Wakaazi wa Newton wamekesha wakiomboleza.
Rais Obama ametoa amri kuwa bendera zipepee nusu mlingoti kwenye majengo ya taifa.
Akizungumza juu ya mauaji hayo, waziri mkuu wa Australia, Julia Gillard, alisema tukio hilo limezidi kusikitisha kwa vile waliouwawa ni watoto.

RATIBA YA LEO BARCLAYS PREMIER LEAGUE IKO HIVI


Newcastle Unitedv/sManchester City

Liverpoolv/sAston Villa

Manchester Unitedv/sSunderland

Norwich Cityv/sWigan Athletic

Queens Park Rangersv/sFulham

Stoke Cityv/sEverton

STORI KWENYE MAGAZETI YA LEO TAR 15 DEC, ZIKO HAPA

Zilizosomwa zaidi