Wednesday, December 12, 2012

HII NDIO RIPOTI KUTOKA UNDP.

United Nation Development Program imesema kuwa jumla ya watu million 2.5 kwa mwaka 2011 walikuwa wameathirika kwa ugonjwa wa UKIMWI This

HII NAYO INAKUHUSU MDAU WANGU WA UKWELI

STORI YA NGASSA KUHAMIA SUDANI IKO HAPA......KWA HABARI ZAIDI INGIA HAPA

VIONGOZI wa Simba na Azam wamesema uamuzi wa winga Mrisho Ngassa kugoma kwenda kufanyiwa vipimo vya afya kama hatua ya awali ya kujiunga na klabu ya El-Merreikh ya Sudan imeiaibisha nchi.
Mbali na kuiaibisha nchi, klabu hizo kwa pamoja zinaona kitendo hicho kuwa ni utovu wa nidhamu na usumbufu kwa viongozi wa timu hiyo ya Sudan waliokuja nchini kukamilisha zoezi hilo.
Simba na Azam zilitangaza kukubaliana kumuuza Ngassa kwa ada ya Dola 100,000 (Sh157 milioni). Katika makubaliano ya mkataba wa mchezaji huyo, El Merreikh ilidaiwa kuwa tayari kumpa Ngassa mkataba wa miaka miwili wenye thamani ya Dola 75,000 (Sh118 milioni).
Jana alipaswa kufanyiwa vipimo vya afya jijini Dar es Salaam chini ya viongozi wa timu hiyo ya Sudan, lakini katika hali ya kushangaza hakutokea.
Akikaririwa na vyombo mbalimbali vya habari juzi, Ngassa alisema hayuko tayari kujiunga na El Merreikh kwa vile siyo Simba wala Azam iliyomshirikisha katika zoezi hilo.
Hata hivyo kauli ya Ngassa inapingana na aliyoitoa wakati akiwa na kikosi cha Timu ya Taifa Bara (Kilimanjaro Stars), akiitaka Simba iache kumbania kuchezea timu hiyo ya Sudan.
Makamu Mwenyekiti wa Simba Godfrey Nyange alisema wamesikitishwa na kitendo alichofanya Ngassa na kwamba watamwita ili kumhoji.“Hatufahamu nini kimempata mpaka sasa. Kwanza hao viongozi wa El Merreikh yeye binafsi ndiye aliyeongea nao na kufikia makubaliano,” alisema Nyange.
Nyange alisema wameshangazwa na uamuzi wa Ngassa wa kubadilika ghafla. “Pengine kuna kitu hapa, amebadilika ghafla,” aliongeza Nyange aliyeteuliwa kuzungumzia suala hilo pia kwa niaba ya Azam.
Alisema kitendo hicho kimeiaibisha Simba na Taifa kwa jumla kwani ni sawa na kuwafungia milango wachezaji wengine wenye nia ya kucheza soka la kulipwa nje ya nchi.
Wakati huohuo, Juma Nyoso ameendelea kuisisitizia klabu yake ya Simba kusitisha mkataba wake haraka ili ajiunge na timu ya Coastal Union ya Tanga.
Uongozi wa Simba ulimpeleka Nyoso kujifua na kikosi cha timu ya vijana kwa madai ya kushuka kiwango na utovu wa nidhamu.Hata hivyo beki huyo anayecheza nafasi ya kati, aligoma kutekeleza agizo hilo la kwenda kujiunga na kikosi B.
CHANZO; MWANANCHI GAZETI

HAPO VIPI

WAFANYAKAZI NGORONGORO KUFUKUZWA KAZI

WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Balozi Hamis Kagasheki ametangaza kuwachukulia hatua za kinidhamu maofisa wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) waliokwamisha mradi wa kuwasaidia wafugaji wa hifadhi hiyo ulioahidiwa na Rais Jakaya Kikwete mwaka 2008.
Akizungumza na wananchi wa Tarafa ya Ngorongoro na viongozi wa NCAA mara baada ya kuelezwa kuhusu kukwama kwa mradi huo, Balozi Kagasheki alisema lazima hatua kali zichukuliwe dhidi ya viongozi hao.
“Haiwezekani mradi ulioahidiwa mwaka 2008 leo hii ukwame, waliohusika kuukwamisha ni lazima wakae pembeni. Ninakwenda Dar es Salaam ila wakae wakijua kuwa barua zao zinakuja” alisema Kagasheki na kuongeza;
“Kabla sijaondolewa wizarani kutokana na matatizo kama haya, mtaondoka ninyi kwanza.…, kukwama kwa mradi huu kutawafanya wananchi wamchukie Rais Kikwete na wanasiasa,” alisema Balozi Kagasheki.

HIKI NDIO KICHANGA KILICHOTUPWA JIJINI DAR


Kichanga hicho cha jinsi ya kike, kinakadiriwa kuwa na umri wa
siku mbili, kimekutwa katika machimbo ya mchanga maeneo ya
Majohe, Gongo la Mboto.
Polisi wanaendelea na juhudi za kumtafuta muhusika

RATIBA YA MICHUANO YA LEO BARANI ULAYA IKO HAPA.



















































Mdau wangu wa ukweli bado nipo na hii, naomba mchango wako wa mawazo katika hili. 'HII TABIA YA WAGOMBEA WA URAIS, UBUNGE NA MADIWANI KUKATAA MATOKEO YA UCHAGUZI BAADA YA KUSHINDWA KATIKA UCHAGUZI HUSIKA, INALETA PICHA GANI KATIKA SIASA'

MKURUGENZI MTENDAJI BUNDA AZOMEWA.

KAIMU Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Bunda, Dinah Rweyemamu juzi alipatwa na wakati mgumu pale alipozomewa na wananchi wakimshinikiza ashuke jukwaani kufuatia wananchi hao kutoridhika na majibu aliyokuwa akiyatoa kwa maswali yao.
Dinah alifikwa na zahama hiyo muda mfupi baada ya Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa, Abdallah Bulembo kumwita jukwaani ajibu maswali hayo yaliyoelekezwa kwake  wakati wa mkutano wa hadhara wa chama hicho uliofanyikia katika eneo la kituo cha zamani cha mabasi mjini Bunda.
Swali lililomletea kizaazaa kaimu mkurugenzi huyo ni lile lililotolewa na Alfred Ndowa aliyetaka kujua sababu za kukithiri kwa michango kwa shule za msingi na sekondari hasa wakati wa kuandikisha wanafuzni wa darasa la kwanza.
Bulembo alimwita Dinah jukwaani ambapo katika kujibu alisema dhamana ya kutokuwapo au kuwapo kwa michango mashuleni imo mikononi mwa kamati zao za shule.Kufuatia kauli hiyo ,wananchi walianza kumzomea kaimu mkurugenzi huyo wakisema hajui kitu na kumtaka Bulembo amshushe.

WAMISRI KUPIGIA KURA KATIBA


Maandamano hasimu kuhusu kura ya maoni juu ya katiba mpya
Wananchi wa Misri wanaoishi katika nchi za kigeni, wameanza 
kupigia kura ya maoni rasimu juu ya katiba ambayo imezua hali 
ya mvutano nchini humo

BADO HAUJACHELEWA, HIZI NDIO STORI KWENYE MAGAZETI YA LEO TAR 12 DEC

Asante sana Mdau wangu wa Ukweli kwa kuendelea kuitembelea Blog hii.

Zilizosomwa zaidi