Tuesday, December 11, 2012

RATIBA YA LEO KATIKA SPANISH COPA DEL RAY HII HAPA,,,,,KWA HABARI ZAIDI INGIA HAPA.


Athletic Bilbaov/sEibar

Cordobav/sBarcelona

Mallorcav/sSevilla FC

Atletico Madridv/sGetafe

Celta Vigov/sReal Madrid

Matokeo kaika ligi ya Capitol One Cup kwa jana yako hapa, Arsenal yatolewa kwa panati



Bradford City(3)1 - 1(2)Arsenal

Norwich City1 - 4Aston Villa

SAKATA NDANI YA TANESCO LAENDELEA

MBUNGE wa Ubungo John Mnyika, ametaja majina ya watu 16 ndani ya Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) ambao amewahusisha na ufisadi ndani ya shirila hilo la umma.
Kati ya majina hayo ambayo ameyaita kuwa ni ya awamu ya kwanza wamo baadhi ya waliokuwa watendaji wa shirika hilo ambao wamesimamishwa kupisha uchunguzi unaofanywa na Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali (CAG).
 Alipoulizwa wiki iliyopita kuhusu uchunguzi huo, GAG Ludovick Utouh alisema uchunguzi huo umeshakamilika na kilichokuwa kikisubiriwa ni kuikabidhi ripoti hiyo kwa bodi ya Tanesco.

UMEWAHI KUONA MAJENGO YA SHULE YA KWANZA ILYIOJENGWA TANZANIA.....INGIA HAPA UIONE


MWAKA 1848, Mmishenari wa Kijerumani Dk Johan Ludwig Krapf,   alitembelea kijiji cha Magila kilichopo  Muheza mkoani Tanga akiwa katika safari zake za Afrika Mashariki.
Magila kuna  mlima ulio katika safu za milima ya Usambara ukipakana na mlima wa Magoroto ambao ndio  chanzo cha maji ya mto Mkurumuzi unaoelekea Muheza.
Historia inaonyesha  eneo la mlima   Magila wenye  miamba na mawe mengi, zamani kabla ya kuja wageni  lilitumika kuwatenga wagonjwa wa ukoma na magonjwa mengine yasiyotibika, kwa lengo la kuwazuia wasiwaambukize wengine.
Dk Krapf alipofika na kuwaona wagonjwa hao  waliokuwa wakiishi kwa madhila makubwa, alichonga msalaba katika mti wa mkuyu kwa imani kuwa Mwenyezi Mungu angewaponya wagonjwa hao.
Eneo hilo ndilo lililokuja kujengwa shule ya kwanza na Waingereza mwaka 1886. Alama ya msalaba huo ipo hadi na sasa na ndipo ilipo Shule ya Sekondari  Hegongo.
Hadi leo mahali hapo panaitwa Magila Msalabani. Kwa sasa Magila ni kata yenye vijiji vya vya Magila, Mikwamba, Misongeni na Mafleta.
Nilifika katika eneo hilo nilipokuwa wilayani Muheza hivi karibuni ili kuchunguza historia ya eneo hilo.
Hapo nikutana na Luteni Kanali mstaafu John Mhina ambaye amekamilisha kuandika kitabu kuhusu historia ya Magila Msalabani,  kinachoeleza historia ya kijiji hicho na ujio wa wazungu walioanzisha shule ya kwanza Tanganyika na kanisa.
Luteni Kanali Mhina aliyelitumikia Taifa kwa muda mrefu kama mwanajeshi , na baadaye kuwa Mbunge wa Muheza kutoka mwaka 1990 hadi 1995,  anasema harakati za kuanzisha shule katika kijiji hicho zilitokana na Wamishenari waliokuja Afrika Mashariki kutoka Ulaya kwaajili ya kueneza dini ya kikristo tangu miaka ya 1770.
Anawataja baadhi ya Wamishenari hao kuwa ni pamoja na David Livingstone, Charles Mackenzie, William Tozer na Edward Steer.
Anasema harakati hizo zilianzia tangu visiwa vya Zanzibar mwaka 1863 ambako pia walikomesha biashara ya utumwa na kuanza ujenzi wa kanisa la Anglikana la Mkunazini Zanzibar kwa miaka 10 tangu mwaka 1873.
Anasema wakati huo kulikuwa na shule iliyoanzishwa Zanzibar maeneo ya Kiungani na Kiinua mguu na Askofu William Tozer mwaka 1869. Hata hivyo,  anasema shule hiyo haikuwa rasmi na ilikuwa ikifundisha elimu ya dini kwa watumwa waliokombolewa.
CHANZO. MWANANCHI

HII NI NYINGINE KWA WANAFUNZI


AFYA YA NELSON MANDELA YAENDELEA VEMA

Former South African president Nelson Mandela looks on as he celebrates his birthday at his house in Qunu, Eastern Cape July 18, 2012. REUTERS-Siphiwe Sibeko
Raisi wa zamani wa Afrika kusini  Nelson Mandela, anendelea kupata matibabu
katika ugonjwa wake wa mapafu. Kwa sasa Mandela ana umri wa miaka 94

STORI KWENYE KURASA ZA MBELE KATIKA MAGAZETI YA LEO TAR 11 DEC ZIKO HAPA

Zilizosomwa zaidi