Wednesday, December 5, 2012

KAMA ULIMISI MATOKEO YA JANA TAR 4 KATIKA UEFA......YOTE YAKO HAPA




Dinamo Zagreb1 - 1Dynamo Kiev

Paris Saint-Germain 2 - 1FC Porto


Montpellier1 - 1Schalke 04

Olympiakos2 - 1Arsenal


AC Milan0 - 1Zenit St Petersburg

Malaga2 - 2Anderlecht


Borussia Dortmund1 - 0Manchester City

Real Madrid4 - 1Ajax Amsterdam

KAMA LEO HUKUPITIA VICHWA VYA HABARI KWENYE MAGAZETI.......INGIA HAPA

KESI YA LULU DESEMBA 17 MWAKA HUU


Kesi ya mauaji ya marehemu Steven Kanumba inayomkabili mwigizaji wa bongo movie,  Elizabeth Michael (Lulu) imeendelea kutajwa katika mahakama ya Hakimu mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam huku suala la umri wa mshitakiwa huyo likiendelea kuwekwa kiporo.

Mbele ya hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama ya Hakimu mkazi Kisutu AUGUSTINA MMBANDO, Wakili wa Serikali KENNETH SEKWAO amesema upelelezi bado haujakamilika na kwa sasa ipo katika hatua ya kutajwa.

Mapema baada ya LULU kufunguliwa mashitaka ya mauaji ya msanii mwenzake STEVEN KANUMBA April mwaka huu, mawakili wanaomtetea waliwasilisha hoja ya kupinga umri wa mshitakiwa huyo na kutaka achukuliwe kama mkosaji mtoto kutokana na umri wake kuwa chini ya miaka 18 hali iliyolazimu suala hilo kupelekwa Mahakama Kuu ya Tanzania iliyoamua kulirejesha jambo hilo kwenye mahakama ya Kisutu.

Pamoja na kurejeshwa kwa suala hilo katika mahakama ya Hakimu mkazi Kisutu kumekuwa na ukimya wa muda sasa, kesi ya LULU imeahirishwa mpaka Disemba 17 mwaka huu ambapo itakwenda kwaajili ya kutajwa.

Zilizosomwa zaidi