Saturday, December 1, 2012

ALICHOKISEMA JAJI MKUU KUHUSU KESI YA LEMA KIKO HAPA.

JAJI Mkuu, Mohamed Chande Othman ameeleza sababu za kutokuwa kwenye jopo la majaji waliopangwa kusikiliza kesi ya aliyekuwa mbunge wa Chadema mkoani Arusha, Godbless Lema.
Jaji mkuu, alitoa maelezo haya jana katika mahojiano maalumu kwenye mahafali ya 12 ya Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto (IJA).
“Ngoja nitolee ufafanuzi suala hilo ili jamii itambue utaratibu wa uendeshaji wa Mahakama ya Rufani, ambayo ina majaji 16 nchini,” alisema Jaji Othman.
Jaji Othman alisema kimsingi hajajitoa kushughulikia kesi hiyo, ila siku ambayo kesi hiyo inatajwa, atakuwa nchini India kuhudhuria Mkutano Mkuu wa 13 wa Majaji Wakuu Duniani.
Maelezo hayo ya Jaji Chande yamekuja siku tatu baada kuripoti kuwa, mkuu huyo wa mhimili wa Mahakama nchini amejitoa kusikiliza kesi hiyo na nafasi yake imechukuliwa na Jaji Bernard Luanda.
“Kwanza ifahamike kwamba, jaji wa Mahakama ya rufani hana ubia na kesi yoyote kwa mujibu wa utaratibu. Jaji yeyote kati ya majaji 16 wa mahakama ya rufani nchini ana mamlaka ya kusikiliza kesi yoyote ya rufani,” alieleza Jaji Othman.
Jaji Othman alifafanua kuwa, rufani ya Lema ni miongoni mwa kesi tatu za uchaguzi zilizobaki ambazo kwa mujibu wa taratibu za kisheria, huanza kusikilizwa baada ya muda wa mwaka mmoja na hukumu yake ni lazima itolewe ndani ya mwaka mmoja tangu kuanza kwake.
“Hivyo basi, kwa vile Jaji yeyote wa Mahakama ya Rufaa anaweza kuisikiliza kesi hiyo, hakukuwa na sababu inisubiri mimi,” alisema.
Jaji Othman alitaja kesi nyingine za uchaguzi zitakazoanza kufanyiwa vikao vya rufani na jopo la majaji wa Mahakama ya Rufani kuwa, ni ile ya Jimbo la Ubungo kati ya Hawa Ng’umbi na John Mnyika ambayo itakuwa chini ya jopo la majaji watatu; Jaji Nathalia Kimaro, Jaji Salum, Salum Masati na Jaji Katherine Oriyo.
Nyingine ni ya Jimbo la Ilemela ya Yusuph Yussuph Masengela Lupilya na wenzake wawili dhidi ya Highness Kiwia na wenzake wawili, ambayo itakuwa chini ya jopo la Majaji Januari Msofe, Jaji Beard Luanda na Jaji Salum Massati.
Alisema rufani ya Lema haijaanza kusikilizwa kwa jaji yeyote, hivyo yeye asingeweza kujitoa kwa kuwa hajapangiwa.
“Kinachotatiza hapa ni kwamba, watu wanaifungamanisha rufani hii na ile ya Arusha ambayo mimi nilikuwa miongoni mwa jopo la majaji kama mwenyekiti.

SHERIA ILIYOANZISHWA KENYA DHIDI YA MADEREVA IKO HAPA

Mwanamke akata bara-bara nchini KenyaSheria mpya ya Kenya ya kuzuwia madereva kuendesha magari kihatari, imeanza kutekelezwa jana Jumamosi ya Tar 1 Dec.
Dereva akikutwa na makosa ataikabili adhabu kali pamoja na kifungo cha maisha.
Madereva wa mabasi ya abiria, yaani matatu, wamekuwa wakigoma tangu Alhamisi mjini Nairobi na kwengineko, kulalamika juu ya sheria hiyo.
Wengi wanasema kuwa hawamudu faini kubwa.
Lakini serikali imeazimia kupunguza vifo vinavyotokana na ajari za barabarani.
Mwaka uliopita Wakenya zaidi ya 3,000 wamekufa kwenye ajali za barabarani.

Leo Barclays Premier League Ratiba iko hivi.


Norwich Cityv/Sunderland                                         

HAYA NDIO MATOKEO YA BACLAYS PREMIER LEAGUE HAPO JANA TAR 1 DEC



West Ham United3 - 1Chelsea

Arsenal0 - 2Swansea City

Fulham0 - 3Tottenham Hotspur

Liverpool1 - 0Southampton

Manchester City1 - 1Everton

Queens Park Rangers1 - 1Aston Villa

West Bromwich Albion0 - 1Stoke City

Reading3 - 4Manchester Unite
Anderson celebrates with Ashley Young after netting at Reading

BENITEZ, ASUASUA CHELSEA

Baada ya Chelsea kukubali kichapo cha magoli 3-1 kutoka kwa  West Ha, kocha wa timu hiyo  Rafael Benitez aonekana kutokubalika kwa asilimia 100. ikumbukwe tu kuwa hiyo ndio match yake ya kwanza kuchezwa tangu alipoingia kuifundisha timu ya Chelsea.
Rafael Benitez is exasperated on the touchline against West Ham

KAMA ULIMISI STORY KWENYE MAGAZETI YA LEO, CHEKI KWA HAPA.

Zilizosomwa zaidi