Thursday, November 29, 2012

HUU NDIO MSIMAMO WA LIGI KUU TANZANIA BARA





MP W D L F A D P

1 13 9 2 2 25 10 +15 29

2 13 7 3 3 17 11 +6 24

3 13 6 5 2 20 11 +9 23

4 Previous rank: 6 13 6 4 3 18 12 +6 22

5 Previous rank: 4 13 6 4 3 16 14 +2 22

6 Previous rank: 5 13 5 6 2 15 10 +5 21

7 Previous rank: 8 13 6 2 5 19 16 +3 20

8 Previous rank: 7 13 4 5 4 9 11 -2 17

9 Previous rank: 10 13 4 3 6 13 20 -7 15

10 Previous rank: 9 13 3 5 5 13 17 -4 14

11 13 4 2 7 9 14 -5 14

12 13 2 6 5 10 15 -5 12

13 13 2 3 8 9 20 -11 9

14 13 0 4 9 3 15 -12 4

Jumamosi hii Barclays Premier League itakuwa imesimama hivi

West Ham UnitedvChelsea

ArsenalvSwansea City

FulhamvTottenham Hotspur

LiverpoolvSouthampton

Manchester CityvEverton

Queens Park RangersvAston Villa

West Bromwich AlbionvStoke City

ReadingvManchester United

KWENYE MAZISHI YA SHARO MILIONEA HAPO JANA, HALI ILIKUWA HIVI.

UDOM KUWASAKA MACHANGUDOA

RAIS wa Serikali ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOSO), Paul Yunge, amesema kuwa wanafanya uchunguzi wa kina ili kuwanasa wanafunzi wa chuo hicho wanaojihusisha na biashara ya kujiuza kimwili ili wawachukulie hatua.

Yunge alifafanua kuwa, wanafunzi watakaobainika kujihusisha na vitendo hivyo watachukuliwa hatua kali za kinidhamu ili iwe fundisho kwa wengine.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma, Yunge alisema kazi ya kufanya uchunguzi tayari imeanza na wanategemea wakati wowote watabaini ukweli kuhusiana na jambo hilo.

Alifafanua kuwa, wanafunzi wanaojihusisha na vitendo hivyo wanakidhalilisha na kukishushia heshima chuo hicho ambacho kimsingi kinapaswa kuwa kioo.

“Ni aibu sana kama watu wamekuja UDOM kusoma na badala yake wanageuka na kufanya biashara ya kujiuza ambayo ni ya kudhalilisha utu wao pamoja na chuo kwa ujumla. Jambo hili lazima tulifanyie kazi,” alisema.

Yunge alidai kuwa wamefikia uamuzi huo baada ya taarifa hiyo kuripotiwa na vyombo vya habari, kitendo ambacho kimeisononesha nchi nzima ukiwemo uongozi wa chuo pamoja na wazazi wa wanafunzi hao.

Hatua ya serikali ya chuo kuanza uchunguzi imekuja baada ya baadhi ya vyombo vya habari wiki iliyopita kuripoti kuwa baadhi ya wanafunzi wa chuo hicho wanajiuza katika sehemu mbalimbali za mji wa Dodoma.

POLISI AFUKUZWA KAZI BAADA YA KUFANYA MAPENZI NA MTUHUMIWA


JESHI la Polisi mkoani Mbeya limemfukuza kazi askari wake Enock Daffa (22) kwa tuhuma za kufanya  mapenzi na mtuhumiwa wa kike mwenye umri wa miaka 25 katika Kituo cha Polisi cha Mji mdogo wa Tunduma, Wilaya ya Momba, mkoani hapa. 


Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Athuman Diwani, askari huyo alitenda kosa hilo Novemba 21,2012 na kwamba mtuhumiwa aliyefanya naye mapenzi alikuwa akikabiliwa na kosa la wizi.
Kamanda Athumani alisema kuwa mbali ya kufukuzwa kazi askari huyo tayari amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Mbozi ili sheria iweze kuchukua mkondo wake.

Aidha alisema kuwa hali kama hiyo haitaweza kuvumiliwa na Jeshi la Polisi na kwamba atakayebainika kufanya tukio kama hilo adhabu yake itakuwa ni kufukuzwa kazi.
Kamanda huyo alitoa wito kwa askari polisi kufanya kazi kwa kufuata sheria na kanuni za Jeshi la Polisi kama mwongozo unavyowaagiza ili kulinda maadili ya Jeshi la Polisi ambacho ndicho chombo kinachotumika na wananchi katika kuzisimamia sheria.
Akizungumzia tukio hilo, baba mzazi wa askari huyo alisema kuwa kitendo alichofaya mtoto wake si cha kiungwana ambacho pia kimetia fedheha familia yake pia kwa jeshi la Polisi ambalo limepewa dhamana ya kutunza usalama wa raia na mali zake.

KATIKA VURUGU ZA MALI, AU IMETUMA WANAJESHI


Waasi wa Mali
Waasi wa Mali
Muungano wa Afrika AU umeunga mkono mpango wa kuwatuma wanajeshi wa kutunza amani nchini Mali, kusaidia katika harakati za kupamabana na wanamgambo wa Kiislamu walioko Kaskazini mwa nchi hiyo.
Kamati kuu wa muungano huo, imeidhinisha uamuzi uliochukuliwa na Muungano wa Kiuchumi wa nchi za Magharibi mwa Afrika ECOWAS wa kutuma wanajeshi 3,000 kusaidia serikali ya Mali, kupambana na waasi hao.
Mpango huo sasa utawasilishwa kwa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa ili kuidhinishwa kabla ya mwisho wa mwaka huu.
Wapiganaji wa Kiisalmu na wa kabila la Toureq walichukua uthibit wa eneo la Kaskazini mwa nchi hiyo baada ya rais wa nchi kuondolewa madarakani kufuatia mapinduzi yaliyofanyika mwezi Machi mwaka huu.
Umoja wa Mataifa umeonya kuwa wapiganaji hao wa Kiislamu wanataka kutekelezwa kwa sheria kali za Kiislamu katika maeneo wanayoyathibiti.
Ripoti ya Umoja huo imesema visa vya ndoa vya lazima, vimeongezeka sawia na wasichana kulazimisha kufanya vitendo vya ukahaba na pia kesi za ubakaji zimeongezeka.
Muungano huo wa ECOWAS unatarajiwa kudumu kwa muda wa miezi sita, awamu ya kwanza ikiwa mpango wa kuwapa mafunzo na kujenga kambi Kusini mwa Mali, kabla ya kuanzisha mikakati ya kijeshi Kaskazini mwa nchi hiyo.
Nchi za Nigeria, Niger na Burkina Faso zimehaidi kutoa wanajeshi hao watakaotumwa nchini Mali.
Baada ya kuidhinisha mpango hupo, kamishna mkuu wa Usalama na Amani wa muungano wa Afrika, Ramtane Lamamra, ametoa wito kwa mataifa mengine ya Kiafrika kutoa wanajeshi zaidi na misaada zaidi ili kufanikisha mpango huu.
CHANZO: DW

Kama ulimisi matokeo ya Barclays Premier League cheki hapa


Chelsea0 - 0Fulham

Everton1 - 1Arsenal

Southampton1 - 1Norwich City

Stoke City2 - 1Newcastle United

Swansea City3 - 1West Bromwich Albion

Tottenham Hotspur2 - 1Liverpool

Manchester United1 - 0West Ham United

Wigan Athletic0 - 2Manchester City

Zilizosomwa zaidi