Monday, November 19, 2012

WAZAZI HAPA INAKUWAJE, PUNGUZENI UKATILI DHIDI YA WATOTO











BOB JUNIOR AKANA KUWA SHOGA

Baada ya fununu nyingi kusambaa mtaani kuwa staa wa Bongo Fleva, Raheem Nanji ‘Bob Junior’ kuwa ni Shoga sasa ameogea waziwazi.
 
Akizungumza kupitia kipindi cha runinga moja usiku wa Ijumaa iliyopita, Bob Junior alisema chanzo cha yeye kudaiwa ni shoga ni wimbo wake maarufu wa Oyoyo.

Alisema mara baada ya kuitoa video ya wimbo wake huo akiwa anakata sana mauno, watu walikuwa wakimpigia simu, wengine wakimtumia meseji kwamba, anaonekana ni ‘chakra’ maana anayaweza sana mauno.


“Watu wanasema mimi ni shoga, lakini si kweli. Kisa kilianzia kwenye ule wimbo wangu wa Oyoyo. Unajua katika video ya ule wimbo nilikata sana mauno, watu wakaamini mimi shoga.
"

“Wengine walikuwa wakinitumia hata meseji wakiamini hivyo. Kwa hiyo sababu kubwa ni ile video tu, watu wana mambo ya ajabu sana,” alisema Bob Junior huku watu  alioongozana nao usiku huo wakitingisha vichwa kukubaliana naye.


Ishu ya Bob Junior kuonekana ni chakra pia iliwahi kusababisha amfikishe kortini kwenye Mahakama ya Mwanzo Kinondoni, Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu akidaiwa kumtukana msanii huyo matusi ya nguoni likiwemo hilo la ushoga.


Katika kesi hiyo iliyofikishwa kwenye mahakama hiyo kwa mara ya kwanza Mei 4, 2011 na kusikilizwa na Hakimu Mfawidhi Mariam Masamalo, Wema alihukumiwa kulipa faini ya shilingi 40,000 au kwenda jela miezi 6 ambapo alifanikiwa kulipa.

AMANI CONGO BADO MATATANI

 
Wanajeshi wa Congo mjini GomaWanajeshi wa Congo mjini Goma
Serikali ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo, imetupilia mbali matakwa yaliyotolewa na wapiganaji wa waasi wa kuanzisha mazungumzo ya amani, na kukariri kuwa itaendelea kuulinda mji wa Goma, Mashariki mwa nchi hiyo.
Waasi wa M23 wamesemekana kuukaribia mji huo huku maelfu ya raia wakikimbia makwao.
Mapema hii leo, wapiganaji hao walitoa ilaani ya saa ishirini na manne kwa serikali ya nchi hiyo kuanzisha mazungumzo, ya amani la sivyo wataendelea na vita hivyo.
Baraza la usalama la umoja wa mataifa limelaaini hatua hiyo ya waasi wa M23 ya kuendelea na mapigano huku wakielekea mji wa Goma.
Mapigano hayo yametajwa kuwa mabaya zaidi tangu mwezi Julai Mwaka huu katika eneo hilo lenye utajiri mkubwa wa madini.
Barabara za mji wa Goma hazikuwa na raia kama kawaida na magari ya kijeshi na yale ya umoja wa mataifa ndiyo yaliyokuwa yakizunguka mji huo.

DAVID BEKHAM ATANGAZA KUACHA KUICHEZEA GALAXY

SEKRETARIETI CCM YAJA KIVINGINE

SEKRETARIETI mpya ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) imeapa kusimamia utekelezaji wa Ilani ya chama hicho tawala kwa kufuatilia mienendo ya watendaji wakuu wa Serikali wakiwamo mawaziri.

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye  alisema jana jijini Dar es Salaam kuwa mpango huo wenye lengo la kuongeza ufanisi wa Serikali, utawabana pia wakuu wa mikoa, wilaya na watendaji wengine wanaosimamia utekelezaji wa Ilani hiyo.

Alisema ikibainika mtendaji yeyote wa Serikali anabaronga katika uwajibikaji wake, sekretarieti hiyo itamjulisha Rais Jakaya Kikwete na kumshauri awafukuze kazi.

“Lengo ni kuhakikisha kila mmoja anawajibika kwa nafasi yake na endapo itabainika watendaji wanaboronga, sekretarieti haitasita kumfahamisha Rais ili awatimue ama kuwaondoa katika majukumu yao,” alisema.

Zilizosomwa zaidi