Friday, November 16, 2012

STORI KWENYE MAGAZETI YA LEO TAR 17 NOV, HIZI HAPA. KWA HABARI ZAIDI INGIA FARAJADOGEJE.BLOGSPOT.COM

BALAA LINGINE HILI HAPA; DAUDI BALALI KUJITOKEZA. Ingia farajadogeje.blogspot.com kwa habari zaidi



Wote tunafahamu kuwa aliyekuwa gavana wa benki kuu ya Tanzania Daudi Balali alifariki dunia tarehe 16.05.2008 huko Boston, Marekani na kuzikwa huko huko.


Lakini kwa watumiaji wa Twitter watakuwa wanamfahamu Daudi Balali wa kwenye mtandao huo ambaye ameendelea kumuumiza vichwa vya watu wengi kuwa ni nani huyu aliye nyuma ya akaunti hiyo na akiendelea kudai kuwa bado yupo hai? 


October 1 alitweet, “Nitakutana na Rais Kikwete na ujumbe wake wiki hii hapa Marekani."

Anavyoonekana ni msomi haswaa na anaishi nje ya nchi. Ni mtu makini, ana hoja, anaijua siasa ya Tanzania na yupo consistent! Hivi karibuni mtu huyo alidai kuwa amekuja Tanzania na kulala kwenye hoteli iliyo karibu na ofisi yake ya zamani.


“In Dar es Salaam, Hyatt Regency Dar es Salaam, The Kempinski Kilimanjaro Hotel. Feels good to be close to my former office, BoT,” alitweet November 13.

Kutokana na kile anachokiandika anaonekana kuwa ni kada mzuri wa CCM na leo ameibuka na kutabiri anguko la CHADEMA kwa kutweet, “Chadema will die by disintegration. Zitto Kabwe and 3 other prominent members will move to CCM,the rest will form 2 new political parties."

Anasema CHADEMA itavunjika ambapo Zitto Kabwe na wanachama wengine watatu wa chama hicho watahamia CCM na wengi wataanzisha vyama viwili vipya vya siasa.
Hata hivyo anadai ameamua kuondoka nchini mapema na kurudi Gaithersburg, Maryland kutokana kuhofia usalama wake.

“I am leaving Dar es Salaam tonight instead of Wednesday on security reasons.”

Mwisho ameendelea kusisitiza kuwa kweli yupo hai kwa kutweet:

I AM REAL. TAKE IT OR LEAVE IT. TWITTER IS THE MESSENGER. THE SURPRISE IS YET TO COME.

LEO KATIKA BARCLAYS PREMIER LEAGUE RATIBA IKO HIVI.


Arsenalv/sTottenham Hotspur

Liverpoolv/sWigan Athletic

Manchester Cityv/sAston Villa

Newcastle Unitedv/sSwansea City

Queens Park Rangersv/sSouthampton

Readingv/sEverton

West Bromwich Albionv/sChelsea

Norwich Cityv/sManchester United

DRC KUULINDA MJI WA GOMA.

Wanajeshi wa CongoGavana wa jimbo la kivu kaskazini Julien Paluku amesema wapiganaji hao wa waasi wa M23 walikuwa wamempigia simu kumjulisha kuwa watawasili leo usiku mjini Goma.
Paluku amesema wanajeshi 150 wa waasi wameuawa lakini msemaji wa waasi hao amekanusha habari hizo.
Mapigano hayo ndiyo mabaya zaidi tangu mwezi Julai mwaka huu katika eneo hilo lenye utajiri mkubwa wa madini.
Zaidi ya watu laki tano wamehama makwao tangu mwezi Aprili mwaka huu, wakati wanajeshi kadhaa walipoasi kutoka kwa jeshi la Serikali.
Mapigano hayo yamekuwa yakiendelea karibu na kijiji cha Kibumba takriban kilomita 30 Kaskazini mwa Goma.

HII NI CHANGAMOTO NYINGINE KWA ELIMU VIJIJINI.

BAADHI ya wanafunzi wa shule za msingi  na sekondari  mkoani Lindi, wameulalamika  utaratibu wa mgao wa walimu ambao wake za vigogo na walimu wenye sifa, wanarundikwa katika shule za mijini.
Utaratibu huo unasababisha kukosekana kwa uwiano katika utaoji wa elimu baina ya shule za mijini na vijijini.
Wanafunzi hao walitoa malalamikoa hayo juzi kupitia Baraza la Watoto la Wilaya ya Kilwa, lilipokuwa likizungumza na timu ya waandishi wa habari waliotembelea baraza hIilo kwa  ufadhili wa Shirika la Save the Children.
Akizungumza kwa  niaba ya baraza la watoto la wilaya hiyo, Idrisa  Samli,  alisema moja ya  kero na sababu zinazochangia  kuzohofisha morali ya watoto kutopenda shule, ni pamoja na kitendo cha watendaji na viongozi  wa halmashauri  hiyo, kutoa upendeleo kwa ndungu na wake zao, kufundisha shule za mijini.
Samli alisema kitendo hicho  ndiyo chanzo cha kukithiri kwa tatizo la utoro miongoni mwa wanafunzi na tofauti katika uatoaji wa elimu kati ya shule za mjini na vijiji .
Alielezea kushangazwa kwake kuona viongozi wa elimu katika wilaya hiyo, hawalichukulii suala hilo kama sehemu ya matatizo yanayochangia kushusha  kiwango cha taluuma.
Baraza hilo limeuomba uongozi wa wilaya,  kuangalia uwezekano wa kuwapunguza walimu wanaofundisha  mijini na kuwapeka vijiji ambako kuna  upungufu mkubwa wa walimu.
Limesema hatua hiyo itasaidia kuleta wiano wa walimu na wanafunzi katika shule za mijini na vijijini.

HALI BADO TETE HUKO GAZA.

Zilizosomwa zaidi