Monday, November 5, 2012

HIZI NDIO KAULI 18 ALIZOZISEMA OBAMA KABLA YA UCHAGUZI LEO HII.


1. "I ran because your voices had been shut out of our democracy for way too long." 

2."We’re not going to turn Medicare into a voucher just to pay for another millionaire’s tax cut."

3."Change is turning the page on a decade of war so we can do some nation-building here at home." 

4."Change comes when we live up to this country’s legacy of innovation, by investing in the next generation of technology and manufacturing."

5."Change is a country where every American has a shot at a good education."  

6.“After all we’ve fought through together, we cannot give up on change now.” 

7."You know I tell the truth. You know that I’ll fight for you and your families every single day, as hard as I know how."

8."You may not agree with every decision I’ve made—Michelle doesn’t. But you know what I believe." 

9."The choice you make tomorrow is not just between two candidates or two parties. It’s a choice between two different visions of America."
10."We’ve made real progress these past four years. But Iowa, we’re here tonight because we’ve got more work to do." 

11."The war in Afghanistan is ending. Al Qaeda is on the run. And Osama bin Laden is dead."Obama 

12. "Today, our businesses have created nearly 5.5 million new jobs. The American auto industry is back. Home values are on the rise."
13. "In 2008, we were in the middle of two wars and the worst economic crisis since the Great Depression."

14. "When the cynics said we couldn't: You said 'Yes we can.' You said 'Yes we can,' and we did."Obama 

15. "To all of you who’ve lived and breathed the hard work of change: I want to thank you. You took this campaign and made it your own

16. "I've come back to Iowa one more time to ask for your vote. I came back to ask you to help us finish what we started." 

17. Happening now: President Obama speaks at the final rally of his final campaign. 

18. "We cannot turn back now. We need to keep moving this country forward." —First Lady Michelle Obama

RADIO CALL, FUNGUO ZA GARI ALIYOKUWA NAYO KAMANDA BARO IMEPATIKANA.

Polisi  mkoani Mwanza  wamefanikiwa kuipata simu ya upepo ‘radio call’ iliyokuwa ikitumiwa na aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, marehemu Liberatus Barlow ambayo ilichukuliwa baada ya kuuawa kwa kupigwa risasi usiku wa manane eneo la Minazi Mitatu Kitangiri.

Mbali na simu hiyo, jeshi hilo pia limefanikiwa kupata ufunguo wa gari la marehemu Barlow ambaye aliuawa wakati akimsindikiza mwanamke mmoja aliyeitwa Doroth Moses walipokuwa wakitoka kwenye kikao cha harusi ya ndugu yake.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Lili Matola, alisema jana kwamba vitu hivyo vilipatikana vikiwa vimefichwa katika shimo la majitaka katika nyumba moja iliyopo maeneo ya Nyashanya.
Pia jeshi hilo limefanikiwa kuwatia mbaroni watuhumiwa wengine wawili wanaodaiwa kuhusika katika mauaji hayo na Kamanda Matola alisema wataunganishwa kizimbani na wengine watano Novemba 15, mwaka huu.
Alisema watuhumiwa hao wawili (majina tunayahifadhi kwa sasa),  mmoja wao akiwa ni ndugu wa mtuhumiwa namba moja katika mauaji hayo, ndio waliotaja sehemu vilikokuwa vimefichwa vitu hivyo baada ya kuhojiwa.
Baada ya kuonyesha vilipokuwa vimefichwa, ilibidi kumtaarifu mwenye nyumba ambaye alitoa idhini ya kubomolewa kwa shimo hilo la majitaka na mmoja wa watuhumiwa aliingia na kutoa ‘radio call’ pamoja na funguo za gari la marehemu, alisema Kamanda Matola.
Alisema kuwa baada ya kutekeleza mauaji hayo, mtuhumiwa namba moja alitoa maelekezo ya wapi pa kuficha vifaa hivyo. Kabla ya kuficha simu hiyo, waliitenganisha na betri yake.
Kamanda Matola alisema katika msako waliofanya nyumbani kwa watuhumiwa hao, pia walikuta sare za moja ya kampuni ya ulinzi  pamoja na magwanda ya mgambo.
Alisema kuwa vitu vingine vilivyokamatwa ni kofia mbili, moja ikiwa ya polisi na nyingine ya kampuni ya ulinzi pamoja na vifaa mbalimbali vinavyotumika kwa ajili ya kufanyia uhalifu.
Alisema mmoja wa watuhumiwa aliwahi kuhukumiwa kifungo cha miaka 30 jela, alichokitumikia kuanzia mwaka 2006 baada ya kukutwa na makosa ya unyang’anyi kwa kutumia silaha. Hata hivyo, alisema aliachiwa huru mwaka 2010 baada ya kukata rufani Mahakama Kuu na kuachiwa huru.
Alisema katika mahojiano na polisi, mtuhumiwa huyo alisema alishawishiwa na kaka yake kufanya kazi hiyo ya ujambazi.
Mbali na watu hao, Matola alisema polisi pia inamshikilia mtu mmoja (jina tunalihifadhi) mkazi wa Nyakabungo akituhumiwa kufadhili kundi hilo la majambazi.

HAWA NDIO WABABE WA MAREKANI, MBABE ZAIDI KUJULIKANA KESHO.

MICHAKATO YA MAISHA

(Mr. Ponciano Vanpyeree.)
Ukiachana na mambo ya Shule, haya ni mambo ambayo kijana huyu anjihusisha nayo. 
Yeye anadai hii mambo iko damuni hivyo baada ya shule anafanya hivyo unavyoona hapo juu



RIPOT KUTOKA UN

Ripoti kutoka umoja wa mataifa inaonesha kuwa takribani
asilimia 70 ya watu wanaoishi maisha ya chini ya dola moja
 kwa siku ni wanawake.

HII NDIO BARABARA INAYOENDELEA KUJENGWA KATIKATI YA JIJINI MWANZA.


DIWANI, KATIBU WA CHADEMA MWANZA KUTIWA RUMANDE.

Mahakama yawatia ndani Diwani, Katibu wa CHADEMA

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimepata pigo kubwa baada ya Mahakama kuwaweka ndani Diwani wa Kata ya Kirumba jijini Mwanza, Dan Kahungu pamoja na Katibu wa Chadema Wilaya ya Ilemela, John Anajus kwa kosa la kukaidi amri halali ya mahakama, iliyozuia uchaguzi wa nafasi ya Meya na Naibu wake katika Manispaa hiyo.
Mbali na viongozi hao wa Chadema kupelekwa mahabusu ya Gereza Kuu la Butimba, pia Mahakama hiyo ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, imeagiza wakamatwe kisha kufikishwa mahakamani Mkurugenzi wa Oganaizesheni wa Chadema taifa, Benson Kigaila na aliyekuwa Meya wa Jiji la Mwanza ambaye pia ni mjumbe wa Kamati Tendaji ya chama hicho, Josephat Manyerere kwa kosa hilo hilo la kudharau amri ya mahakama.
Amri hiyo imetolewa hii leo na Hakimu Mkazi Mfawidhi mkoani Mwanza, Angelo Rumisha, kufuatia kesi namba 69/2012 iliyopo mahakamani hapo dhidi ya watuhumiwa sita kutoka chama hicho, ambapo alisema mara baada ya watuhumiwa hao kukamatwa mahakama itatoa hukumu yake kwa pamoja.

Akitoa  amri hiyo, Rumisha alisema mahakama haiwezi kutoa adhabu kwa baadhi ya watuhumiwa, na kwamba agizo la kutaka wakamatwe Manyerere na wenzake ni kutaka mahakama iheshimiwe, mara inapotoa amri zake halali kwa mujibu wa sheria za nchi.
Kupitia  kesi hiyo yenye namba 69/2012, Rumisha aliwataja wengine wanaotakiwa kukamatwa na jeshi la polisi kisha kufikishwa mahakamani hapo ni pamoja na Mkurugenzi huyo wa Oganaizesheni ya Chadema taifa, Kigaila, Katibu wa mwenezi wa Chama hicho wilaya ya Ilemela, Kalod Majura pamoja na mkuu wa Mdhamini wa Chadema.
Awali ilidaiwa mahakamani hapo na wakili wa upande wa mlalamikaji mahakamani hapo, Salum Magongo kwamba watuhumiwa wote kwa pamoja walishiriki  kikao cha kutangaza uamzi wa kumfukuza udiwani, Henry Matata wa Chadema (kata ya Kitangiri), kabla pingamizi lililokuwa limewasilishwa mahakamani na diwani huyo halijatolewa maamuzi na mahakama.
“Mteja wangu Henry Matata aliweka pingamizi mahakamani baada ya Kamati Tendaji ya Chadema kutangaza kumvua uanachama kinyume cha taratibu. Lakini watuhumiwa wote wa kesi hii walishiriki kuvunja sheria kwa kumtangaza kumfukuza udiwani”, alidai mahakamani hapo wakili Magongo.
Aidha, Wakili huyo aliendelea kudai kuwa, kwa kufanya hivyo washtakiwa hao walipuuza amri halali ya mahakama iliyotolewa na mahakama Septemba 15 mwaka huu, kinyume cha sheria na taratibu.
Hata hivyo, hakimu Rumisha aliamuru diwani huyo wa kata ya Kirumba, Kahungu pamoja na Anajus waende mahabusu katika gereza la Butimba, hadi hapo watuhumiwa wengine watakapokamatwa na jeshi la polisi kisha kuhukumiwa kwa pamoja.
Wadadisi wa mambo wanadai kwamba, kosa la kupatikana kudharau amri halali ya mahakama adhabu yake ni kwenda miezi sita, au kulipa faini, hivyo viongozi hao wa Chadema huenda wakahukumiwa kutumikia adhabu kadri itakavyoamriwa na mahakama

Zilizosomwa zaidi